Vichwa vya habari vya magazeti: 'Maisha katika huduma' na 'tulikupenda ma'am'

Magazeti ya Uingereza yamechapisha toleo lao la kwanza kwenye kurasa zao za mbele tangu kifo cha Malkia. Hizi ni baadhi ya kurasa zao za mbele za kihistoria

B
Maelezo ya picha, Gazeti la The Times lilianza ukurasa wake wa mbele kwa picha ya kuvutia ya Malkia kutoka kwenye tukio la kutawazwa kwake katika mwaka 1953, iliyoambatana na maneno : "Maisha katika huduma." Ukurasa wa nyuma wa gazeti ulibeba nukuu kutoka katika matangazo yake ya Krismasi katika mwaka 1957, ambayo yalikuwa ya kwanza kutangazwa kwa njia ya televisheni: "Siwezi kuwaongoza katika mapambano. Siwapatii sheria au kusimamia haki lakini ninaweza kufanya kitu kingine: Ninaweza kuwapatia moyo wangu na kujitolea kwangu kwa ajili ya visiwa hivi vyote vya zamani, na kwa undugu wa mataifa yetu."
G
Maelezo ya picha, "Mioyo yetu imevunjika," linasema Daily Mail likiwa na picha ya Malkia ya 1952, wakati alipokuwa Bintimfalme Elizabeth. " Jinsi gani ya kutafuta maneno?" mwandishi wa Makala maalumu Sarah Vine gazeti anauliza. "Majonzi yetu ni hisia mia moja tofauti , zote ni ngumu kuzifahamu."
G
Maelezo ya picha,  Daily Telegraph limechapisha upya jumbe binafsi za Malkia za rambirambi kwa familia za wahanga wa mashambulio ya 9/11 : "Majonzi ni gharama tunayolipa kwa upendo." Rais wa Marekani Joe Biden alielezea kuhusu kauli hiyo katika rambi rambi zake na kukumbuka jinsi alivyosimama katika mshikamano na Marekani katika "siku zake za giza".
G
Maelezo ya picha, Magazeti kadhaa, ikiwa ni pamoja na the Guardian, yalichagua kuweka picha ya Malkia ya mwanzo wa enzi yake. Picha yenye nguvu, iliyochukuliwa na Sir Cecil Beaton, inamuonesha Malkia akiwa amevaa taji lake huku akiwa amebeba fimbo ya enzi katika siku ya kutawazwa kwake.
G
Maelezo ya picha, The Mirror lilichagua picha ya hivi karibuni zaidi ya Malkia, inayoonesha wasifu wake maarufu. Gazeti hilo liliamua dhidi ya kichwa cha habari , na badala yake lilisema tu : "Asante
G
Maelezo ya picha, Magazeti mengi, likiwemo the Sun, yalitumia picha hiyo hiyo ya rangi nyeupe na nyeusi ya Malkia katika miaka yake ya baadaye akiwa mwenye fikra, na tabasamu laini . "The Sun na wasomaji wetu tulikupenda," linasema gazeti. "Tunajivunia kuwa ulikuwa Malkia wetu."
G
Maelezo ya picha, The i pia lilitumia picha kutoka katika siku ya kutawazwa kwake ,kama linavyosema nchi itaingia siku 10 za maombolezo kwa ajili ya mtawala aliyetawala kwa muda mrefu zaidi.
g
Maelezo ya picha, Likiwa na picha moja ya rangi nyeupe na nyeusi iliyojaa kwenye ukurasa wake wa kwanza, the Daily Express linasema: "Malkia wetu mpendwa amefariki." Gazeti linasema dunia inaomboleza "kumpoteza Malkia wa kutia moyo ".
G
Maelezo ya picha, Ulifanya wajibu wako , Ma'am" linasema Daily Star. Lilibadilisha rangi yake ya juu ambayo kwa kawaida huwa nyekundu na kuwa nyeusi na kuchagua picha sawa ya siku ya kutawazwa kwake kama yalivyofanya magazeti mengine mengi.

The Times, the Guardian, the i, na the Daily Star yote yalitumia picha ya siku ya kutawazwa kwa Malkia mwaka 1953 kwa ajili ya kuomboleza kifo chake.

The Guardian liliacha picha ya kuvutia ya Malkia mpya aliyevikwa taji ionekane – zaidi ya jina lake na tarehe za enzi - huku the Times likiongeza maneno: "Maisha katika huduma."

Gazeti la The Times lilianza ukurasa wake wa mbele kwa picha ya kuvutia ya Malkia kutoka kwenye tukio la kutawazwa kwake katika mwaka 1953, iliyoambatana na maneno : "Maisha katika huduma." Ukurasa wa nyuma wa gazeti ulibeba nukuu kutoka katika matangazo yake ya krismasi katika mwaka 1957, ambayo yalikuwa ya kwanza kutangazwa kwa njia ya televisheni: "Siwezi kuwaongoza katika mapambano. Siwapatii sheria au kusimamia haki lakini ninaweza kufanya kitu kingine: Ninaweza kuwapatia moyo wangu na kujitolea kwangu kwa ajili ya visiwa hivi vyote vya zamani, na kwa undugu wa mataifa yetu."

 Katika taarifa yake kuu, mwandishi wake, Valentine Low anasema "historia itatoa hukumu yake katika ukamilifu wa muda lakini ni vigumu kukubali kuwa yeye atakumbukwa kwa jingine lolote lile isipokuwa mmoja wa wafalme bora zaidi katika historia yetu".

 Kwingineko, walikumbuka jinsi Malkia - "mwenye mwangaza unaong’ara ndani ya jicho lake " – wakati mmoja aliwashauri waheshimiwa wa eneo "wakati wa baadhi ya ziara au wengine" sio kuzungumza na mwandishi wa masuala ya ufalme wa the Times: alikuwa kutoka the Times, alisema, na tutamuweka tu katika gazeti.

 The Sun linawakumbusha wasomaji wake jinsi tu dunia ilivyokuwa tofauti miaka 70 iliyopita -Ilikuwa ni miaka saba tu baada ya Vita ya Pili vya Dunia, Uingereza ilikuwa bado ni himaya, na bendi ya Beatles ilikutana miaka mitano baadaye, lilisema.