Vichwa vya habari vya magazeti: 'Maisha katika huduma' na 'tulikupenda ma'am'

Magazeti ya Uingereza yamechapisha toleo lao la kwanza kwenye kurasa zao za mbele tangu kifo cha Malkia. Hizi ni baadhi ya kurasa zao za mbele za kihistoria

The Times, the Guardian, the i, na the Daily Star yote yalitumia picha ya siku ya kutawazwa kwa Malkia mwaka 1953 kwa ajili ya kuomboleza kifo chake.

The Guardian liliacha picha ya kuvutia ya Malkia mpya aliyevikwa taji ionekane – zaidi ya jina lake na tarehe za enzi - huku the Times likiongeza maneno: "Maisha katika huduma."

Gazeti la The Times lilianza ukurasa wake wa mbele kwa picha ya kuvutia ya Malkia kutoka kwenye tukio la kutawazwa kwake katika mwaka 1953, iliyoambatana na maneno : "Maisha katika huduma." Ukurasa wa nyuma wa gazeti ulibeba nukuu kutoka katika matangazo yake ya krismasi katika mwaka 1957, ambayo yalikuwa ya kwanza kutangazwa kwa njia ya televisheni: "Siwezi kuwaongoza katika mapambano. Siwapatii sheria au kusimamia haki lakini ninaweza kufanya kitu kingine: Ninaweza kuwapatia moyo wangu na kujitolea kwangu kwa ajili ya visiwa hivi vyote vya zamani, na kwa undugu wa mataifa yetu."

 Katika taarifa yake kuu, mwandishi wake, Valentine Low anasema "historia itatoa hukumu yake katika ukamilifu wa muda lakini ni vigumu kukubali kuwa yeye atakumbukwa kwa jingine lolote lile isipokuwa mmoja wa wafalme bora zaidi katika historia yetu".

 Kwingineko, walikumbuka jinsi Malkia - "mwenye mwangaza unaong’ara ndani ya jicho lake " – wakati mmoja aliwashauri waheshimiwa wa eneo "wakati wa baadhi ya ziara au wengine" sio kuzungumza na mwandishi wa masuala ya ufalme wa the Times: alikuwa kutoka the Times, alisema, na tutamuweka tu katika gazeti.

 The Sun linawakumbusha wasomaji wake jinsi tu dunia ilivyokuwa tofauti miaka 70 iliyopita -Ilikuwa ni miaka saba tu baada ya Vita ya Pili vya Dunia, Uingereza ilikuwa bado ni himaya, na bendi ya Beatles ilikutana miaka mitano baadaye, lilisema.