Sababu tatu za kutokwa na damu kwenye kinyesi

Muda wa kusoma: Dakika 3

Inaweza kuonekana kuwa jambo dogo, lakini tunapoliona, linaweza kusababisha wasiwasi mkubwa.

Watu wengi hufadhaika wanapoona damu kwenye kinyesi chao, wakidhani ni tatizo kubwa, kama saratani ya tumbo.

Hata hivyo, kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha kutokwa na damu kwenye mfumo wa usagaji chakula, baadhi zikiwa mbaya zaidi kuliko nyingine.

Fermín Mearín, mkurugenzi wa kituo kinachobobea katika magonjwa ya usagaji chakula nchini Hispania, aliieleza BBC sababu za kawaida zaidi za damu katika kinyesi.

Bawasiri

Hii kawaida husababisha damu kuonekana, baada ya kutoa haja ndogo au kutoa kinyesi.

"Hii inaonesha kuwa damu inatoka sehemu ya ndani ya mwili na kwamba chanzo chake kiko kwenye njia ya haja kubwa," anasema Dk. Mearin.

Tatizo la aina hii mara nyingi halitambuliwi hadi uchunguzi ufanyike.

kupasuka kunaweza kubainika kupitia uchunguzi makini. Ni nyufa ndogo katika njia ya haja kubwa inayotokea kwa watu wenye matatizo ya kupata haja kubwa au wenye kinyesi kigumu, na ni hali ya maumivu sana.

Maumivu makali ya tumbo na kuhara

Kuonekana kwa uvimbe kwenye utumbo husababisha maumivu makali na kujaa hewa tumboni.

"Kwenye kesi hii, pamoja na kuvimba kwa tumbo, mara nyingi unakabiliwa na kuhara na maumivu ya tumbo," anasema Mearín. Mara nyingi, matatizo haya huathiri utumbo mkubwa, pia saratani ya utumbo inaweza kutokea, katika baadhi ya kesi, kuathiri utumbo mdogo.

Kinyesi cheusi

Iwapo kinyesi ni cheusi inaweza kuashiria kutokwa na damu ndani ya mwili.

Katika hali hii, inahitajika kufanya mfululizo wa uchunguzi wa mfumo wa usagaji chakula ili kubaini chanzo cha kutokwa na damu.

Katika hali nyingi, kuwepo kwa damu hakumaanishi kuwa kuna tatizo kubwa kiafya.

Katika baadhi ya nchi, kuna programu maalumu za uchunguzi wa saratani ya utumbo mkubwa kwa jamii za wazee.

Programu hizi zinaonesha kuwa kuwepo kwa damu kwenye kinyesi ni ishara ya hatari inayoweza kuwa saratani ya utumbo mkubwa.

Iwapo damu inatambuliwa kwenye kinyesi cha mtu, hufanyiwa upimaji tena, jambo ambalo linawasababishia wasiwasi wengi.

"Watu hufika hapa wakiwa wameshtuka, lakini mara nyingi sio hatari ya saratani," anasema Mearin.

Madaktari hufanya uchunguzi kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 au wenye historia ya kifamilia ya saratani ya utumbo mkubwa ili kuchunguza viungo vya ndani, hasa utumbo mkubwa.

Ingawa ni muhimu kujua rangi ya kinyesi, pia ni muhimu kuelewa kuwa baadhi ya vyakula vinaweza kuathiri muonekano wake.

Kwa mfano, kula nyanya kunaweza kufanya kinyesi kuwa chekukundu, wakati kula chokoleti nyeusi kunaweza kuifanya kiwe cheusi.

Hata hivyo, ikiwa damu ipo kwenye kinyesi, ni muhimu kushauriana na daktari haraka ili kuchukua hatua zinazofaa.