Kwanini wakati mwingine kinyesi chako huelea?

Muda wa kusoma: Dakika 4

Fumbo la kwanini kinyesi chako wakati mwingine huelea juu ya maji ya choo huku kingine kikizama chote bila kuacha alama inaweza kuwa fursa ya kuelewa afya ya bakteria wanaoishi tumboni mwetu.

Kabla ya kuendelea, Nagarajan Kannan ana swali: "Wewe kinyesi chako kiko upande gani huzama huelea?

Ni jambo la kushangaza lakini ni kwa mtindo huu wa fikira ndio umeamsha shauku ya mkurugenzi wa maabara ya Mayo Clinic huko Rochester, Minnesota.

Sehemu kubwa ya kazi yake ni kusoma mifumo ya seli na molekuli inayosababisha saratani ya matiti.

Lakini katika nyakati chache za mapumziko, Kannan amejikuta akichunguza– kwanini haja kubwa wakati mwingine huelea.

Wengi wetu labda tumeshakutana na hali hii mara moja:Kinyesi kinagoma kuondoka, kinaelea juu ya maji ya choo wakati mwingine, hata hivyo, kinyesi huzama bila dalili yoyote.

Fumbo la kushangaza kabisa.

Hata hivyo, jibu la hili fumbo la kinyesi linatoa mwanga wa kushangaza kuhusu kinachoendelea ndani ya miili yetu na afya ya bakteria wanaoishi ndani yake, anasema Kannan.

Awali ilifikiriwa kwamba sababu ya haja kubwa kuelea mara kwa mara ilikuwa ni kiwango cha mafuta kilichokuwa ndani yake.

Lakini katika miaka ya 1970, baadhi ya madaktari bingwa wa magonjwa ya tumbo kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota, katika muda wao wa ziada, walijiamulia kuifanyia utafiti kwa mfululizo wa majaribio.

Baada ya kupima kinyesi cha wahudhuriaji 39 – na kwa baadhi yao wenyewe kwa kipimo kizuri – walipataja jibu kwamba si mafuta, bali gesi.

Kwa nadharia sahihi, kiasi cha gesi kilichopo ndani ya kinyesi kinaweza kutofautiana kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba kinaweza kuelea juu ya maji au kuzama kama jiwe (pamoja na kuteleza kidogo katikati ya choo).

Utafiti ulionyesha kwamba kama gesi kwenye kinyesi kinachoelea ingeondolewa, kingezama.

Sababu ya tofauti hiyo, walihitimisha kwamba, ilikuwa uzalishaji mwingi wa methane. Kwa maneno mengine, kutokwa na gesi kupita kiasi.

Katika miaka iliyopita, sayansi ya tiba imebaini umuhimu mkubwa wa microbiota katika nyanja nyingi za afya zetu – kuanzia unene hadi magonjwa ya moyo.

Kannan alidhani kuwa mabadiliko katika mfumo wa bakteria trilioni 100, fangasi, na vijidudu vingine vidogo vinavyoishi tumboni huenda vinahusika na namna kinyesi chetu kitakavyoelea au kuzama.

Unaweza pia kusoma

"Sehemu kubwa ya kinyesi kimsingi inajumuisha chembe za chakula zilizobadilishwa na kutengeneza wingi wa bakteria," anasema.

Ili kujaribu nadharia hiyo, yeye na wenzake katika Kliniki ya Mayo walichunguza kinyesi cha panya.

Panya hawa hawana vijidudu kwenye matumbo yao.

Katika vipimo vya kuelea kwa kinyesi vilivyotengenezwa na watafiti hao, kinyesi kutoka kwa panya hawa kilizama majini papo hapo, huku karibu 50% ya kinyesi kutoka kwa panya walio na vijidudu vya utumbo vikielea, kabla ya kuzama chini. Walipochunguza kwa makini, sababu ikawa wazi.

"Kinyesi kisicho na vijidudu kimejaa chembe ndogo ndogo za chakula ambazo hazijamezwa na kuwa na msongamano mkubwa wa kinyesi kuliko kinyesi kilichojaa vijidudu," anasema Kannan.

Kisha wataalamu waliwapandikizia baadhi ya panya hao wasio na vijidudu kinyesi kutoka kwa panya wa kawaida ambao kinyesi kilikuwa kimeelea - kumaanisha kwamba walipokea bakteria wa utumbo.

Panya hao ambao hapo awali hawakuwa na wadudu walianza pia kutoa kinyesi kilichoelea.

Hata pale panya walipowekewa bakteria kutoka kwa binadamu, pia kilielea.

"Inaonekana kwamba mara baada ya vijidudu hivyo kuanzishiwa,ilionekana wazi kinyesi cha panya kilipanda juu' bila kujali aina ya wafadhili," anasema Kannan.

Yeye na wenzake pia walifanya uchunguzi wa kinasaba wa spishi za bakteria kwenye kinyesi kutoka kwa panya ambao walikuwa wakielea na kugundua walikuwa na viwango vya juu vya spishi 10 za bakteria zinazojulikana kuwa huzalisha gesi.

Iliyotawala miongoni mwao ilikuwa Bacteroides ovatus, ambayo inajulikana kuzalisha gesi kupitia uchachushaji wa wanga na imehusishwa na kuwepo gesi tumboni iliyopita kiasi wagonjwa hasa binadamu.