Malkia Elizabeth II: Mipango ya kuuaga mwili na mazishi

.
Maelezo ya picha, Picha ya taji la kifalme

Malkia amefariki na hivyobasi kuhitimisha huduma yake ya muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza. Alifariki kwa amani akiwa amezungukwa na watu wa familia yake katika kasri la Balmoral nchini Uskochi. Siku zijazo, haya ndio matarajio ya mazishi yake huku taifa la Uingereza likitoa heshima yake ya mwisho.

Mwili wake utaagwa katika ukumbi wa Westminister

Baada ya jeneza lake kurudi mjini London, mwili wa Malkia utalazwa katika ukumbi wa Westminister kwa takriban siku nne kabla ya mazishi yake ili kuruhusu raia wa Uingereza kuutazama mwili wake na kuuaga. Ukumbi huo ndio wa zamani zaidi ikilinganishwa na kumbi nyingine Westminister, katikati ya serikali ya Uingereza. Mtu wa mwisho wa familia ya Ufalme huo kuwekwa katika hali hiyo alikuwa mamake Malkia mwaka 2002, wakati zaidi ya watu 200,000 walipopanga foleni kutazama jeneza lake.

.
Maelezo ya picha, Picha za mwili wa mamake Malkia ukiwa amelazwa

Jeneza la Malkia litawekwa katika eneo la juu, linalojulikana kama Catafalque, chini ya dari lililojengwa na mbao. Kila kona ya eneo hilo litalindwa na wanajeshi kutoka vitengo vyake ambao wanahudumia familia ya Kifalme. Atasafirishwa hadi katika ukumbi wa Westminister kutoka Kasri la Buckingham katika msafara utakaokuwa ukiendeshwa polepole wakiambatana na gwaride la kijeshi la familia ya Kifalme.

Maandamano

Watu wataweza kuutazama msafara huo wakati utakapokuwa ukipita barabarani huku skrini kubwa zikionesha matukio hayo ambazo zinatarajiwa kuwekwa katika bustani za kifalme. Jeneza lake litafunikwa kifalme na litakapowasili Westminister litawekewa taji la Kifalme orb na fimbo.

G

Mara tu jeneza hilo litakapowekwa ndani ya ukumbi huo, ibada fupi itafanyika. Baadaye raia wataruhusiwa kuingia.

Je mazishi ya Malkia yanafanyika lini?

Mazishi ya serikali ya Malkia yanatarajiwa kufanyika huko Westminster Abbey chini ya wiki mbili. Siku kamili itathibitishwa na Kasri la Buckingham.

Abbey ni kanisa la kihistoria ambapo wafalme na malkia wa Uingereza wanatawazwa, ikiwa ni pamoja na kutawazwa kwa Malkia mnamo 1953, na ambapo aliolewa na Prince Philip mnamo 1947.

Westminster Abbey

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Westminister

Hakujakuwa na ibada ya mazishi ya mfalme katika kanisa la Abbey tangu Karne ya 18, ingawa mazishi ya mamake Malkia yalifanyika huko mnamo 2002.

Wakuu wa nchi kutoka kote ulimwenguni watakuwa wakisafiri kwa ndege kuungana na washiriki wa Familia ya Kifalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia. Wanasiasa wakuu wa Uingereza na mawaziri wakuu wa zamani pia watakuwepo.

Siku itaanza huku jeneza la Malkia likibebwa kutoka Ukumbi wa Westminster hadi eneo la Westminster Abbey kwenye Gari la Jeshi la Wanamaji la Kifalme.

Unaweza pia kusoma:

kanisa

Gari hilo lilionekana mara ya mwisho mnamo 1979 katika mazishi ya mjombake Mwanamfalme Philip, Lord Mountbatten, likiwa na mabaharia 142 kutoka Jeshi la Wanamaji la Kifalme.

Wajumbe wakuu wa Familia ya Kifalme, pamoja na Mfalme mpya, wana uwezekano wa kuambatana na msafara huo.

Ibada hiyo huenda ikaendeshwa na Dean wa Westminster David Hoyle, huku Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby akitoa mahubiri. Waziri Mkuu Liz Truss anaweza kuitwa kutoa mahubiri.

Abbey

Baada ya ibada ya mazishi, jeneza la Malkia litatolewa kwa msafara wa kutembea kutoka Westminister Abbey hadi Wellington Arch, kwenye bustani ya Hyde Park Corner ya London kabla ya kuelekea Windsor kupitia gari la kubeba maiti.

Jeneza la Malkia litafanya safari yake ya mwisho alasiri hiyo hadi St George's Chapel katika kasri la Windsor.

Mfalme na washiriki wakuu wa Familia ya Kifalme wanatarajiwa kujumuika na msafara katika Quadrangle ndani ya Kasri la Windsor kabla ya jeneza kuingia St George's Chapel kwa ibada.

kanisa

St George's Chapel ni kanisa linalochaguliwa mara kwa mara na Familia ya Kifalme kwa ajili ya harusi, ibada za kawaida na mazishi. Ni mahali ambapo Duke na Duchess wa Sussex, Prince Harry na Meghan, walifunga ndoa na ambapo mazishi ya marehemu mume wa Malkia Prince Philip yalifanyika.

Kanisa

Chanzo cha picha, AFP

Jeneza la Malkia litashushwa ndani ya Jumba la Royal Vault kabla ya kuzikwa katika kanisa la ukumbusho la King George VI, lililoko ndani ya St George's Chapel.

Banner of the Queen