Kasri la Balmoral: Nyumba ya Scotland iliyopendwa na Malkia

Chanzo cha picha, Getty Images
Mapenzi ya Malkia katika nyumba yake ya Balmoral huko Royal Deeside yalijulikana sana.
Alitumia majira mengi ya kiangazi katika shamba la ekari 50,000 huko Aberdeenshire, kwa kawaida akiwa na mume wake mpendwa Philip pamoja na familia yake.
Ikiwa imezungukwa na mashamba, Kasri la Balmoral ndipo alipotumia mapumziko mengi kufurahia kuanzia kutembelea babu na bibi yake Mfalme George V na Malkia Mary akiwa mtoto mdogo, hadi miezi ya mwisho ya maisha yake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Aliandaa sherehe nyingi za kifalme huko na alifurahia kutazama matukio kwenye uwanja wa Michezo ya Braemar iliyo karibu na washiriki wengine wa Familia ya Kifalme.
Alitumia muda mwingi wa miaka ya mwisho ya Philip kukaa pamoja naye huko Balmoral - walibaki huko pamoja wakati wa marufuku ya kutotoka nje na walitumia kumbukumbu ya miaka 73 ya harusi Novemba 2020.
Balmoral imekuwa moja ya makazi ya Familia ya Kifalme ya Uingereza tangu 1852, wakati ardhi hiyo nakasri la asili liliponunuliwa kutoka kwa familia ya Farquharson na Prince Albert, mume wa Malkia Victoria.
Nyumba hiyo kipindi hicho ilionekana kuwa ndogo sana na Jumba la sasa la Balmoral liliamuriwa kujengwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jumba lenyewe ni mfano wa usanifu wa Kiskoti na imeainishwa katika Historia ya Mazingira ya Scotland kama jengo lililoorodheshwa la kitengo A. Kasri mpya ilikamilishwa mnamo 1856 na kasri ya zamani ilibomolewa muda mfupi baadaye.
Inabaki kuwa mali binafsi ya Malkia na sio sehemu ya ardhi ya taji la umalkia
Ni shamba linalofanya kazi, ikijumuisha sehemu ya kutungua ndege grouse moors, misitu na mashamba, pamoja na mifugo kama ng'ombe na farasi.
Familia ya Kifalme ilikuwa Balmoral wakati Princess Diana alipofariki mnamo Agosti 31, 1997.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jumapili asubuhi baada ya kifo chake, Malkia na Mwanamfalme Charles akiwa watoto na wake William na Harry walihudhuria ibada ya kanisa karibu na Crathie Kirk.
Wakiwa njiani kuelekea nyumbani waliangalia heshima na ujumbe wa maua ulioachwa na umma.
Hizi ni baadhi ya picha zingine za Malkia na familia yake huko Balmoral kwa miaka mingi:

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images















