Haya ni matukio 6 ya ucheshi wa Malkia Elizabeth II

Queen laughing

Chanzo cha picha, Max Mumby/Indigo

Jukumu la Malkia katika maisha ya umma lilikuwa la ratiba iliyopangwa bila kupoteza muda na mara nyingi alionekana kuwa na uso wa umakinifu. Lakini katika miaka yake ya baadaye ya maisha yake, alitupatia sehemu yake ya ucheshi.

Kuanzia kutushirikisha katika mkate uliopakwa jamu na muigizaji wa kufikirika -Paddington Bear hadi kujitokeza bila kutarajiwa ndani katika picha ya wachezaji wa mpira wa magongo wa Australia, tunaangalia baadhi ya nyakati zake za ucheshi zaidi.

Aliposheherekea Jubilee yake kwa kunywa chai na Dubu anayeitwa Paddington

Maelezo ya video, Tazama: Malkia alipokutana na Paddington Bear katika sherehe kwenye kasri lake

Kama sehemu ya sherehe za Jubilee yake ya miaka 70 ya utawala wake mwezi Juni (Platnum Jubilee), Malkia alionekana kwenye video akinywa chai na mnyama aina ya dubu anayejulikana kama Paddington Bear, katika 'mchoro' ambao ulifungua hafla ya BBC kwenye Kasri lake. 

Wakati sherehe zilipokuwa karibu kuanza, Paddington alitoa kitafunio chake alichokipenda - mkate uliopakwa jamu. "Kila mara hutunza mmoja kwa ajili ya dharura," alimwambia Malkia, akitoa mmoja kutoka kwenye kofia yake maarufu nyekundu.

"Hata mimi pia" alijibu Malkia, akifungua mkoba wake maarufu mweusi na kutoa mkate wake. 

 Alipokutana na muigizaji James Bond

Maelezo ya video, Tazama: 'Good evening Mr Bond' - wakati Malkia alipokutana na 007 (muigizaji huyo)

Kama sehemu ya ufunguzi wa sherehe za michezo ya Olympiki za London 2012, Malkia aliingia kwa namna ya kipekee kwa usaidizi wa Muigereza mwingine maarufu - James Bond.

Katika mchezo wa kuigiza uliobuniwa na muongozaji Danny Boyle, Malkia alimpokea mgeni kutoka 007 (James Bond) katika Kasri ya Buckingham, kabla ya wawili hao kuondoka pamoja kwa kutumia helikopta.

Halafu baadaye alionekana akitua kwa parachuti ndani ya uwanja wa Olympiki huku akisalimia umati wa watu uliokuwa unamshangiliwa.

Kushiriki 'chalenji' ya michezo ya Invictus Games 'fighting talk'

Maelezo ya video, Malkia na Mwanamfalme Prince Harry wakiunga mkono 'chalenji' kutoka kwa Barack na Michelle Obama kuhusu Invictus Games.

Mwaka 2016, Malkia alionekana katika video nyingine iliyosambaa sana - safari hii akiwa na mjukuu wake Mwanamfalme Harry kupigia debe michezo ya maaluu ya kimataifa kwa maveterani na watoa huduma waliojeruhiwa inayoitwa - Invictus Games.Wawili hao walitazama ujumbe wa video kutoka kwa rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na Michelle Obama, ambao walionekana kumpatia Prince Harry changamoto ya mchezo huo.Malkia hakufadhaika. "Oh kweli, tafadhali," alisema.

Kukata keki na kwa upanga

Maelezo ya video, Malkia alisisitiza kukata keki kwa upanga huko Cornwall.

Katika maisha yake Malkia ameshiriki matukio mengi ya kukata keki, lakini katika mara hizo, mara moja alitumia upanga maalumu wa sherehe. Alijaribu mbinu isiyo ya kawaida katika hafla ya hisani huko Cornwall.

Mtu wa kujitolea alipomkumbusha kuwa kisu cha kawaida kinapatikana, Malkia hakukatishwa tamaa.

"Najua kipo," alijibu, akiendelea kushika upanga. "Hii sio kitu cha kawaida."

Alipovamia picha ya wachezaji wa mpira wa magongo wa Australia

The Queen and Jayde Taylor

Chanzo cha picha, @_JaydeTaylor

Mnamo 2014, wachezaji wawili wa mpira wa magongo wa Australia walipigw ana butwaa wakati Malkia alionekana akitabasamu kwa nyuma walipopiga picha yao wakati wa Michezo ya Jumuiya ya Madola huko Glasgow.

Jayde Taylor (kushoto) alichapisha picha ya kwanza kwenye Twitter na kusema: "Ahhh Malkia kavamia picha yetu ya selfie!", na tweet hiyo kusambaa sana mitandaoni.

Akicheka na kundi la nyuki

The Queen and the Duke

Chanzo cha picha, Chris Young / PA Media

Malkia aliandamana na mumewe, marehemu Duke wa Edinburgh, katika maelfu ya shughuli rasmi.

Lakini wakati wa ukaguzi wa kijeshi huko Windsor Castle mwaka 2003, kundi la nyuki lilivamia na kuharibu shughuli za kawaida za matukio. Wanandoa hao wa kifalme walishuhudia tukio la kufurahisha, lililonaswa kwenye kamera na mpiga picha Chris Young.

"Ilikuwa tukioa la kibinadamu," aliambia BBC. "Alikuwa akicheka kwa nguvu kama msichana mdogo na alifurahia pia."

BBC