Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 01.11. 2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Sporting imeafikia makubaliano ya kumruhusu meneja Ruben Amorim kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Manchester United wakati wa mapumziko ya kimataifa ya Novemba. (Telegraph - Subscription Required)
United italipa fidia kuwezesha idadi ya wafanyikazi wa Amorim kuungana naye Old Trafford. (ESPN),
Mshambulizi wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26, na kiungo wa kati wa Denmark Morten Hjulmand, 25, hawajafurahishwa na uamuzi wa Amorim kuondoka Sporting baada ya kukataa ofa ya kuondoka klabuni hapo msimu uliopita. (Ojogo - In Portugal )
Lakini Gyokeres huenda akajiunga na Amorim katika klabu ya Manchester United iwapo makubaliano yataafikiwa. (Soka365),

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Bayern Munich na Ujerumani Jamal Musiala, 21, anasema ana furaha katika klabu hiyo ya Bundesliga huku akihusishwa na uhamisho wa kujiunga na Manchester City. (Goal),
Manchester United wanaweza kushindana na Liverpool kwa ajili ya kumnunua beki wa pembeni wa Wolves wa Algeria Rayan Ait-Nouri. (GiveMeSport)
Brentford itadai pauni milioni 60 kumnunua mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, katika dirisha la uhamisho la Januari huku Arsenal ikiwa na nia ya kutaka kumnunua. (Football Insider),
Steven Gerrard anakabiliwa na shinikizo la kufutwa kazi kama meneja wa Al-Ettifaq baada ya kiwango duni cha klabu hiyo ya Saudia kusababishwa na kutolewa kwao katika kombe wiki hii. (Sun),

Chanzo cha picha, Getty Images
Kikundi cha uwekezaji wa michezo duniani kinafahamika kuwa kilitoa ofa ya 45% ya hisa katika Crystal Palace. (Mail),
Aston Villa wako kwenye mazungumzo na fowadi wa Uingereza Morgan Rogers, 22, kuhusu mkataba mpya. (Athletic - Subscription Required)
Real Madrid wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Aurelien Tchouameni, 24. (Relevo - In Spanish)
Real Madrid wako tayari kulipa £84m kwa Enzo Fernandez au wamtoe Tchouameni kwa Chelsea kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 23. (Fichajes, kupitia TeamTalk), nje

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wanafuatilia hali ya Rafael Leao huko AC Milan kwa nia ya kumnunua winga huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 25 msimu wa joto. (Sport - In Spanish)
Liverpool wamemtambua mlinzi wa Bournemouth na Hungary Milos Kerkez, 20, kama mgombea katika kutafuta beki mpya wa kushoto. (TeamTalk), nje
Athletic Bilbao wanatumai kukubaliana mkataba mpya na winga wa Uhispania Nico Williams, 22, huku kukiwa na hamu kutoka kwa Barcelona. (Sport - in Spanish),
Getafe wanatazamia kutaka kumnunua beki wa Tottenham Mhispania Sergio Reguilon, 27, ambaye mkataba wake unamalizika Juni 2025. (Fichajes - In Spanish ).
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












