Vita vya Ukraine: Magharibi yalaani mipango ya Urusi ya kura ya maoni kuhusu Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters
Mataifa ya Magharibi yamelaani mipango ya Moscow ya kufanya kile kinachoitwa kura ya maoni ya dharura katika sehemu za Ukraine ambazo kwa sasa ziko chini ya udhibiti wa Urusi.
Kura hizo zimeitishwa na maafisa wanaoungwa mkono na Urusi katika mikoa minne ya Ukraine kuuliza iwapo wanapaswa kuwa sehemu ya Urusi.
Marekani, Ujerumani na Ufaransa zimesema kamwe hazitatambua matokeo ya kura kama hizo "za udanganyifu".
Muungano wa kijeshi wa Nato ulisema mipango hiyo inaashiria kuongezeka kwa vita.
Mipango ya kuendesha uchaguzi kwa siku tano, kuanzia Ijumaa, imetangazwa katika mikoa ya mashariki ya Luhansk na Donetsk - pamoja na Zaporizhzhia na Kherson kusini.
Quartet inawakilisha karibu 15% ya eneo la Ukraine - au eneo lenye ukubwa wa Hungary, kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters.
Pendekezo kwamba kura halali na za haki zinaweza kuendeshwa katikati ya vita lilipuuzwa mara moja na nchi za Magharibi.
Unaweza kusoma;
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alikashifu mipango ya Urusi ya kura za "uzushi", huku Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akisema "Ikiwa wazo la kura ya maoni ya Donbas halikuwa la kusikitisha sana lingekuwa jambo la kuchekesha," Bw Macron aliwaambia waandishi wa habari mjini New York, ambako anahudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan alisema Marekani haitatambua kamwe kura hizo, na kuzitaja kuwa ni "kudharau kanuni za uhuru na uadilifu wa eneo".
''Kura yoyote ya maoni iliyopangwa na vikosi vya wavamizi inakiuka sheria za kimataifa na haitakuwa na nguvu ya kisheria'', Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) lilisema katika taarifa yake.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwashukuru washirika wake kwa msaada wao.
Bw Zelensky anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video baadaye siku ya Jumatano.
Kulikuwa na ripoti kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin angetoa hotuba yake mwenyewe, Jumanne jioni - uwezekano wa kujadili kura zilizopangwa, au uhamasishaji wa wanajeshi nchini Ukraine.
Lakini hakuna hotuba iliyotolewa. Mipango ya kuandaa kura ndani ya siku chache inaonekana kama msukumo wa Bw Putin kuharakisha utwaaji wa Urusi wa Ukraine.
Hatua hii inakuja baada ya mashambulizi makubwa ya Kiukreni, ambapo Kyiv inadai kuwa imechukua tena kilomita za mraba 8,000 (maili za mraba 3,088) mwezi huu.
Kuimarisha udhibiti wake juu ya ardhi ya Ukraine kunaweza kuiwezesha Urusi kutoa madai kwamba eneo lake - sio tu jeshi lake - lilikuwa likishambuliwa na silaha za Magharibi huku uhasama ukiendelea.
Hii ni kwa sababu mataifa kadhaa ya magharibi yamekuwa yakiipatia Ukraine silaha za kusaidia katika ulinzi wake.
Inahofiwa kuwa hii inaweza kusababisha kuzidi kwa mzozo ambao tayari umemwaga damu.
Viongozi wanaounga mkono Urusi katika mikoa minne ya Ukraine wameunga mkono kura za maoni. Mkuu wa utawala wa wakala wa Urusi huko Luhansk, Leonid Pasechnik, alisema ni "ndoto yetu ya pamoja na mustakabali wetu wa pamoja".
Naibu mkuu wa Baraza la Usalama la Urusi, Dmitry Medvedev, alisema kuwa kura hizo zitarejesha "haki ya kihistoria" na kuwa haiwezi kutenguliwa.
Tawala za wakala wa Urusi zimekuwa zikifanya kazi Donetsk na Luhansk tangu mwaka 2014. Maeneo hayo yalitambuliwa kuwa huru na Bw Putin siku tatu kabla ya kuanza uvamizi wake tarehe 24 Februari.
Mashambulizi yaliyofuata yalishuhudia Urusi ikichukua udhibiti kamili wa Luhansk kwa muda - ingawa Ukraine sasa imepata eneo fulani.
Hatua za hivi punde zaidi za kutaka "kura za maoni" zifanane na hatua ya Urusi kutwaa rasi ya kusini ya Crimea mwaka 2014.
Kura pia iliitishwa huko katika jaribio la kuhalalisha utawala wa Moscow, hata hivyo kura hiyo pia, ilibandikwa jina la 'haramu' na kulaaniwa na jumuiya ya kimataifa.














