Biden amuonya Putin asitumie silaha za kimbinu za nyuklia

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Marekani Joe Biden ameionya Urusi isitumie silaha za kemikali au silaha za kimkakati za nyuklia katika vita nchini Ukraine.
Akizungumza wakati wa mahojiano na CBC News, Bw Biden alisema hatua ya aina hiyo "itabadilisha sura ya vita; tofauti na kitu chochote kile tangu Vita ya pili ya Dunia".
Hakusema ni vipi Marekani itajibu iwapo silaha za aina hiyo zitatumika.
Rais wa Urusi Vladimir Putin aliviweka vikosi vya nyuklia vya nchi yake katika hali ya tahadhari "maalumu" kufuatia uvamizi wake katika Ukraine mwezi Februari.
Aliwaambia wakuu wa ulinzi ni kwasababu ya ‘’kauli za uchokozi’ za Magharibi.
Silaha za nyuklia zimekuwepo kwa karibu miaka 80 na nchi nyingi zinaziona kama njia kukomeshwa kwake kama njia inayotoa hakikisho kwa usalama wa taifa lao.
Urusi inakadiriwa kuwa na na vilipuzi vya nyuklia takriban 5,977, kulingana na Shirikisho la wanasayansi wa Marekani.
Hatahivyo, huenda isiwe na uwezekano wa kutumia silaha hizo.
Silaha za mbinu za nyuklia ni zile zinazoweza kutumiwa katika masafa mafupi, tofauti za silaha za "kimkakati" za nyuklia ambazo zinaweza kupiga katika masafa marefu na kusababisha vita kamili vya nyuklia.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika mahojiano ya dakika 60 na mwandishi wa shirika la habari la CBS Scott Pelley katika Ikulu ya White House, Rais Biden aliulizwa ni nini angemwambia Putin iwapo anaangalia uwezekano wa kutumia silaha za maangamizi nchini Ukraine.
"Usifanye, usifanye, usifanye," lilikuwa jibu la Rais Biden.
Bw Biden aliylizwa pia ni athari zipi zitakuwa kwa Bw Putin iwapo mstari huo utavukwa?
"Unafikiri nitakwambia iwapo ninajua ni nini? Bilas haka, sitakuambia. Itakuwa na athari," Alijibu Bw Biden.
"Watatengwa zaidi katika dunia kuliko ilivyowahi kushuhudiwa. Na itategemea ni kwa kiwango gani cha kile watakachofanya ndicho kitakachoamua jibu litakalotokea’.’
Vita vya Ukraine havijaisha pamoja na matumaini ya Kremlin.
Katika siku za hivi karibuni, Ukraine inasema imechukua upya zaidi ya kilomita za mraba 8,000 (au maili za mraba 3,088) za eneo katika jimbo la Kaskazini – mashariki la Kharkiv.
Licha ya kurudi nyuma, Rais Putin amesisitiza kwamba mafanikio ya Ukraine kukabiliana na mashambulio hayataizuia Urusi kuendelea na operesheni zake katika mashariki mwa nchi.

Chanzo cha picha, EPA/RUSSIAN DEFENCE MINISTRY PRESS SERVICE















