Hizi ndio helikopta za kisasa zaidi za mapigano za mapigano duniani

G

Chanzo cha picha, PA Media

Helikopta ni miongoni mwa ndege zinazotumika katika vita katika maeneo mbali mbali ya dunia yenye vita.

 Ndege za kisasa zaidi zinatengenezwa na nchi kadha, lakini inapokuja katika , ndege hizi 9 zina ubora wa kipekee, kuanzia silaha zinazotumiwa, teknolojia zinazotumia na bei yake ni ya kipekee zaidi.

Katika Makala hii fupi tunaangazia kuhusu nini hasa kinachozifanya ziwe za kipekee na pia kufahamu zinatengenezwa katika nchi gani.

1. AH-64E Apache Guardian

e

Ndege hii aina ya helikopta inayofahamika kama Apache iliundwa na kutengenezwa nchini Marekani na inaelezewa kama ndege ya kisasa zaidi ya mapigano ambayo imewahi kutengenezwa hadi sasa.

Kwa mara ya kwanza, jeshi la Marekani liliitumia katika mwaka 2011, ikiwa na uwezo wa kuwqabeba watu wawili pekee.

 Na ndege hii ina uwezo wa kubeba silaha, zikiwemo silaha nzito, mabomu na makombora ya kushambulia adui.

 Na ndege hizi zina uwezo wa kuwa kubeba silaha, zikiwemo silaha nzito, mabomu na makombora ya kumshambulia adui.

Miongoni mwa nchi ambazo Marekani imeuzia silaha hizi ni pamoja na Saudi Arabia na Taiwan, huku nchi za India, Indonesia, Iraq na Korea Kusini zikiripotiwa pia kuagiza silaha hizi

G

2. Bell AH-1Z Viper

Ndege hizi zilitengenezwa pia nchini marekani kuanzia ile ya zamani ya AH-1W Siper Cobra ambayo hutumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani.

 Ndege hiyo ilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka mwaka 2010 na mwaka 2012 utengenezaji wake rasmi ukaanza.

Ndege hii ni moja ya ndege ambazo zinaweza kupigana kwa kushitukiza katika uwanja wa mapambano. Huwa zina uwezo wa kubeba mabomu, makombora ya kuzuia mashambulio ya makombora ya masafa na mitambo ya kuzuwia mashambulio ya vifaru.

g

Chanzo cha picha, Russian Army

3. Kamov Ka-52 Hokum-B

Helikopta ya mapigano aina ya jet Ka-52 ilitengenezwa na Urusi mwaka 2008 ana akaanza kutumiwa na jeshi la Urusi.

Ndege hii ina kasi kubwa ikilinganishwa na helikopta nyingine zilizotengenezwa kwa ajili ya vita kutokana na mbawa zake ambazo zimewekwa juu ya nyingine.T

Wakati ndege hii inapokuwa katika maeneo ya vita, huwabeba watu wawili pekee, rubani na msaidizi wake.

Getty

Chanzo cha picha, RT

4.Mil Mi-28 Havoc 

Helikopta inayofahamika kama Mi-28 pia ilitengenezwa na Urusi katika miaka ya mwisho ya 1970, lakini ilianza kutumiwa katika huduma mwaka 2006.

 Ndege hii ni tofauti na nyingine , kwani inapokuwa na tatizo au inapogongana na ndege nyingine ina mfumo ambao rubani anaweza kunusurika.

 Ndege hiyo ina makombora mazito yenye uwezo wa kuangamiza vifaru na magari mengine ya kivita, pia inaweza kuyapiga kwa mabomu na bunduki zinazoshuka kwa kasi kubwa.

Taarifa zinasema kuwa, mbali na Urusi ndege hizi pia hutumiwa na Kenya, ambayo ilinunua ndege hizi kutoka Moscow.

5. Eurocopter Tiger 

Helikopta hii inayofahamika kama Tiger yenye uwezo wa kumbeba rubani na msaidizi wake pekee ilitengenezwa kwa ushirikiano baina ya Ufaransa na Ujerumani.

Ilivumbuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1984 lakini ilianza kutumiwa rasmi mwaka 2002.

Ndege hii kwa sasa inatumiwa nan chi kama vile Australia na uhispania, ndege hizi zimetumiwa katika vita vya Afghanistan, Libya na Mali.

 Sawia na hizi, miongoni mwa helikopta za kisasa zaidi dunaini ni Z-10 zilizoptengenezwa na uchina katika miaka ya 2009-2010, Denel AH-2 Rooivalk iliyotengenezwa na Afrika Kusini, na Agusta A129 Mangusta iliyotengenezwa na Italia mwaka 1992 na Mil Mihind iliyotengenezwa na Urusi mwaka 1991.

Ndege hizi ziko katika nafasi ya 6 hadi ya 9.