Ndege ya kivita ya F35-C: Marekani inapigania kuifikia ndege hiyo ilioanguka kabla ya China

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbio dhidi ya wakati zinaendelea kwa Jeshi la wanamaji la Marekani kufikia mojawapo ya ndege zake za kivita ilioanguka - kabla ya jeshi la China kufika mbele yake.
Ndege hiyo ya F35-C yenye thamani ya $100m (£74m) ilianguka Kusini mwa bahari ya China baada ya kile Jeshi la wanamaji la Marekani linaelezea kama "bahati mbaya" wakati ilipokuwa ikipaa kutoka kwa meli inayobeba ndege za kijeshi ya Marekani USS Carl Vinson.
Ndege hiyo ya kivita ndiyo mpya zaidi katika Jeshi la Wanamaji la Marekani, na imejaa vifaa vya kuainishwa. Hivyobasi yeyote atakayefika mbele kuiokoa ndege hiyo atakuwa mshindi .
Wanamaji saba walijeruhiwa wakati ndege hiyo ilipoanguka siku ya Jumatatu baada ya kugonga eneo moja la meli ya Vinson wakati wa mazoezi ya kijeshi.
Kwa sasa ipo chini ya bahari, lakini kinachotokea baadaye ni siri. Jeshi la Wanamaji la Marekani hatahivyo limekatgaa kusema ni wapi ndege hiyo ilipoanguka na itachukua muda gani kuitoa majini
China inadai umiliki wa karibu eneo lote la Bahari ya kusini mwa taifa hilo na imezidi kuchukua hatua za kudai madai hayo katika miaka ya hivi karibuni, ikikataa kutambua uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya 2016 ikisema hauna msingi wa kisheria.

Chanzo cha picha, TED ALJIBE
Wataalamu wa usalama wa taifa wanasema jeshi la China litakuwa "na hamu sana" kuifikia wa kwanza ndege hiyo huku meli ya uokoaji ya Marekani ikionekana kuwa itachelewa siku 10 kutoka eneo la ajali.
Hiyo imechelewa sana, anasema mshauri wa ulinzi Abi Austen, kwa sababu betri ya sanduku jeusi katika ndege hiyo itakufa kabla ya wakati huo, na hivyobasi kufanya kuwa vigumu kupata ndege.
"Ni muhimu sana Marekani kuifikia kwa haraka ," anasema. "F-35 kimsingi ni kama kompyuta inayoruka. Imeundwa kuunganisha mashambulizi - kile Jeshi la Wanahewa linachokiita 'kuunganisha vitambuzi kwa wapiga risasi'."
Uchina haina teknolojia hiyo kwa hivyo iwapo itaipata mbele ya Marekani huenda ikapiga hatua kubwa mbele, anasema.
Alipoulizwa kama kulikuwa na mwangwi wa Vita Baridi hapa, anasema: "Yote ni kuhusu nani mwenye uwezo mkubwa wa kijeshi

Je, ni nini maalum kuhusu F-35C?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Ina mfumo wa unaowezeshwa na mtandao unaoruhusu ushiriki wa taarifa inazokusanya ikiwa hewani,
- Ndege ya kwanza ya Jeshi la Wanamaji la Marekani "inayoweza kuonekana chini" ikiw na nadhodha anayoiwezesha kufanya kazi bila kutambuliwa katika anga ya adui.
- Ina mabawa makubwa na zana thabiti zaidi za kutua zinazoifanya "kufanya mashambulizi inapopaa kutoka meli ya ndege za kivita baharini
- Ina injini ya kivita yenye nguvu zaidi duniani yenye kasi ya hadi 1,200 mph,
- Inaweza kubeba hadi makombora mawili kwenye mbawa zake na manne ndani yake
- Bi Austen, mshauri wa zamani wa Mwenyekiti wa Wakuu wa jeshi Marekani na mwanadiplomasia mkuu wa zamani wa Nato na Umoja wa Ulaya, alisema anaamini kwamba jaribio lolote la China kujaribu kudai haki ya kuokoa ni "kuijaribu" Marekani.
- Hakuna shaka China inaitaka ndege hii, ingawa ujasusi wa mtandao unaweza kumaanisha kuwa tayari wana ujuzi fulani wa mambo ya ndani, mpangilio na ufanyaji kazi wake, anasema Bryce Barros, mchambuzi wa masuala ya China .
- "Nadhani wangetaka kuona sehemu halisi za ndege, ili kuelewa vyema jinsi ilivyopangwa na kupata udhaifu wake."
- Jeshi la Wanamaji la Marekani lilikubali katika taarifa kwamba operesheni ya uokoaji ilikuwa inaendelea kufuatia "makosa" ndani ya USS Carl Vinson.
Je uokoaji huo utafanyika vipi?
Timu ya wasimamizi wa Jeshi la Wanamaji la Marekani la uokoaji na uogeleaji itapeleka mifuko kwenye kifusi hicho cha ndege ambayo itawekwa hewa ili kuweza kufura kwa leno la kuibeba ndege hiyo .
Ndege hiyo inaelekea ilikuwa na angalau makombora kadhaa yaliyobebwa kwenye mbawa zake au kwenye ghuba ya silaha za ndani jambo ambalo linaweza kutatiza uokoaji.

Kuna mfano wa michezo hii ya kijeshi ya paka na pan
Mnamo 1974, katika kilele cha Vita Baridi, CIA iliitoa kwa siri manowari ya Kirusi kutoka kwenye sakafu ya bahari karibu na pwani ya Hawaii kwa kutumia mitambo yake.
Miaka miwili kabla, jeshi la China liliokoa kwa siri manowari ya Uingereza HMS Poseidon ambayo ilizama kwenye pwani ya mashariki ya China.
Na inaaminika kuwa China ilipata mabaki ya helikopta ya siri ya Marekani ambayo ilianguka katika uvamizi wa boma la Osama bin Laden mwaka 2011.
Bwana Barros alisema: "Tuna uhakika wanajeshi wa China walipata kuona vifaa na programu za ndani wakati huo."
Operesheni kuu ya uokoaji iliyoshikilia Rekodi ya Dunia ya Guinness ilikuwa ni kuinua mabaki ya ndege ya usafirishaji ya Wanamaji wa Marekani kutoka sakafu ya bahari ya Ufilipino mnamo Mei 2019. Ilikuwa katika kina cha takriban 5,638m (18,500 ft).
Chaguo jingine, bila shaka, ni kuiharibu ndege hiyo ili kuizuia kuingia katika mikono ya Beijing.
"Jambo rahisi kufanya itakuwa kuishambulia !" Alisema afisa mmoja wa kijeshi.
Lakini hiyo haifikiriwi kuwa njia inayozingatiwa.ya.












