Tetesi za Soka Jumamosi: Garnacho kutimka United? mbadala wake aanza kusakwa

Muda wa kusoma: Dakika 3

Winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 20, ameonyesha dalili za kuondoka katika majira ya joto kwa kuiuza nyumba yake yenye thamani ya pauni milioni 3.85 miezi 12 tu baada ya kuinunua. (Sun)

Wolves wameshangaza baada ya kuibuka kutaka kumsaini winga wa Manchester United na England Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 25, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Chelsea, majira ya joto. (Football Transfers)

Mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Rayan Cherki, 21, ana kipengele kwenye mkataba wake cha kuuzwa kwa pauni milioni 25, huku Manchester United na Tottenham Hotspur wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomnyatia. (GiveMeSport)

Manchester United pia wanamnyatia mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria kutoka Atalanta Ademola Lookman, mwenye umri wa miaka 27, ili kutatua tatizo lao la uhaba wa mabao. (Caught Offside)

Sporting wako tayari kushusha bei ya mshambuliaji wao wa Sweden Viktor Gyokeres kutoka pauni milioni 85 (euro milioni 100) hadi takribani pauni milioni 59 (euro milioni 70), huku Arsenal na Manchester United wakiwa bado wanaonyesha nia ya kumsajili (Athletic - inahitaji usajili)

Juventus wanapambana kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 26, katika majira ya joto lakini Manchester United wako tayari kushindana na klabu hiyo ya Italia kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Napoli ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray. (Teamtalk)

Arsenal hawana tena nia ya kumsajili mshambuliaji wa Newcastle na Sweden Alexander Isak, 25, ambaye anatarajiwa kupewa mkataba mpya na klabu ya Magpies. (Chronicle)

Bayer Leverkusen wanavutiwa na kipa wa Espanyol Joan Garcia, mwenye umri wa miaka 23, huku pia Arsenal wakifuatilia maendeleo yake. (Bild)

Inter Milan hawana nia ya kumsajili kiungo wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, atakapoondoka Manchester City kwa uhamisho wa bure majira ya joto kutokana na umri wake. (Calciomercato)

Real Madrid wako tayari kuongeza mkataba wa beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 32, zaidi ya mwaka 2026 licha ya kuwaniwa na vilabu vya Ligi kuu ya Suadi arabia, Saudi Pro League. (Florian Plettenberg)

Chelsea hawana mpango wa kumuuza kiungo wa Argentina Enzo Fernandez majira ya joto, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akiwa sehemu muhimu ya mipango yao. (Fabrizio Romano)

Xabi Alonso ameridhika kuendelea kuwa kocha wa Bayer Leverkusen, akiwa na umri wa miaka 43 yuko tayari kusubiri fursa ya kumrithi Carlo Ancelotti kama kocha wa Real Madrid. (Relevo)