Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Nani atamrithi Semenyo Bournemouth?

Chanzo cha picha, Getty Images
Bournemouth inamchukulia mshambuliaji wa Tottenham Wales Brennan Johnson, 24, kama mbadala wa Antoine Semenyo, 25, ikiwa mshabuliaji huyo wa Ghana ataondoka katika klabu hiyo mwezi Januari. (Sky Sports)
Hata hivyo, wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Crystal Palace, ambao wanaandaa dau la pauni milioni 35 kumsajili mshindi huyo wa Ligi ya Europa. (Mail)
Bournemouth pia inavutiwa na winga wa Leicester City wa Leicester City Abdul Fatawu, 21, ambaye amewahi kuhusishwa na Crystal Palace, Everton na Sunderland. (Mail)
Barcelona inataka kumsajili beki wa Bournemouth na Argentina Marcos Senesi kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Sport - kwa Kihispania)
Liverpool wako tayari kusubiri hadi msimu wa joto kumsajili beki wa Crystal Palace, 25, Muingereza Marc Guehi, badala ya uhamisho wa Januari. (MaIL- usajili unahitajika)
Everton wanafikiria kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Manchester United na Muingereza Kobbie Mainoo, 20 na mchezaji mwenzake na mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24. (i Paper - usajili unahitajika)
Manchester United wana ndoto ya kumrejesha kiungo wa Scotland Scott McTominay, 29, Old Trafford kutoka Napoli. (Caught offside)

Chanzo cha picha, Getty Images
Conor Gallagher anatazamiwa kuondoka Atletico Madrid mwezi Januari, huku Manchester United, Tottenham na Newcastle zikimuwania kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25. (Team talk)
Everton wamefutilia mbali uhamisho wa mshambuliaji wa Wolves wa Norway Jorgen Strand Larsen, 25, ambaye pia amekuwa akihusishwa na West Ham. (Football Insider)
Leeds wameungana na Flamengo katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Lazio wa Argentina Taty Castellanos, 27. (Calcio Mercato - kwa Kiitaliano)
Klabu za EPL Manchester United, Arsenal, Newcastle na Brentford zinamfuatilia winga wa Hoffenheim mwenye umri wa miaka 19 wa Ivory Coast Bazoumana Toure. (Caught offside)















