Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Semenyo kutua Liverpool au Manchester City?

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool iko tayari kuchuana na Manchester City na kuongeza kasi ya kumfukuzia mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo, 25, kutoka Ghana. (Telegraph)
Tottenham imepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Leon Goretzka mwenye umri wa miaka 30 na klabu yake ya Bayern Munich. (Team talk)
Fulham imefufua tena azma ya kumsajili mshambuliaji wa PSV wa Marekani Ricardo Pepi, 22, ambaye klabu hiyo ya Uholanzi inakadiria thamani yake kuwa takriban euro milioni 40. (Mail)
Crystal Palace na Newcastle United wanapigana vikumbo kuwania saini ya kiungo wa AZ Alkmaar Kees Smit, 19, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa wababe wa La Liga, Real Madrid. (Athletic)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham inamsaka mshambuliaji mpya mwezi Januari, huku mshambuliaji wa Manchester City Mmisri Omar Marmoush, 26, mshambuliaji wa Porto na Uhispania Samu Aghehowa, 21, na mshambuliaji wa Juventus wa Uturuki Kenan Yildiz, 20, wakiwa chaguo lao. (Standard)
Sunderland ina nia ya kumsajili mchezaji wa klabu ya Lille Ayyoub Bouaddi, 18, na kiungo wa wa Monaco mwenye umri wa miaka 21 Lamine Camara. (Team talk)
Manchester City iko tayari kumtoa mlinzi Nathan Ake, 30, mwezi Januari ikiwa watapokea ofa ya zaidi ya £21m. (Sport - kwa Kihispania)
Eintracht Frankfurt wameanzisha mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Nottingham Forest Arnaud Kalimuendo, 23, ambaye wanamwona kama chaguo kubwa, iwapo uhamisho wa mshambuliaji wa Newcastle United Will Osula, 22, hautafanyika. (Florian Plettenberg)
Ajax imemtambua mlinzi wa Burnley Quilindschy Hartman, 21, kama mmoja wa walengwa wao wakuu katika usajili wa Januari. (Fabrizio Romano)
Liverpool inatarajiwa kuwasilisha dau la pauni milioni 60 kumsajili kiungo wa Real Madrid Eduardo Camavinga, 23. (Fichajes - kwa Kihispania).
Klabu ya Girona inayoshiriki Ligi Kuu ya Uhispania maaru Serie A, iinataka kumsajili mlinda lango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen baada ya Aston Villa kusitisha mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Sport - kwa Kihispania)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid haina nia ya kumtoa kwa mkopo kiungo Franco Mastantuono mwenye umri wa miaka 18 mwezi Januari huku Xabi Alonso akitaka kumweka karibu. (Fabrizio Romano)
West Ham huenda ikamruhusu kiungo wa Brazil Lucas Paqueta kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari iwapo ofa inayokubalika itatolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Football Insider)
Chelsea wanatarajia kuwa na dirisha tulivu la usajili la Januari na ingawa The Blues wanataka kuongeza beki mpya wa kati, wachezaji wapya wanaowasili wanaweza kujiunga na msimu ujao wa joto. (Standard)















