Unalifahamu Jiji linalopenda 'ukorofi' duniani?

Berline

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakazi wa Berline wana sifa ya kuwa watu wanaochukulia vitu na mambo kawaida kwa ujumla, kusema wazi wanatajwa kuwa wakorofi kwa jinsi wanavyozungumza. Lakini kwa lugha ya upendo namna hii ya kuzungumza inaitwa "Berliner Schnauze", na jinsi utakavyochukulia kuhusu hilo inategemea mtazamo wako.

Wanaoathirika zaidi ni wapita njia ambao sio wenyeji wa mji huu, ambapo kuzungumzishwa kwa ukali kwa vitu ambavyo hawajui ama hawakujua kwamba walikosea.

Vyovyote vile, mwenyeji anaweza kukuongelesha kwa ukali bila kukutahadharisha, kwa kawaida bila kuchochewa, akikueleza wazi anachojisikia kwa namna ambayo haujawahi kuifikiria.

Berlin

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwenye karatasi, Berliner Schnauze ni lahaja ya Kijerumani inayozungumzwa ndani na na maeneo ya karibu na mji wa Berlin.

Dk Peter Rosenberg, mtaalam mzaliwa wa Berlin Magharibi ambaye ameifahamu Berliner Schnauze kunatokana na miaka ya masomo na uzoefu wa maisha, anauelezea kama "schlagfertig", au mchezo wa lugha wenye akili za haraka. Anasema kuwa ni lugha ya mazungumzo ya Berlin - inayotegemea na maoni au muitikio.

Hakika, kuna tofauti katika matamshi, sarufi kati ya Berliner Schnauze (uzungumzaji wa Berline) na Hochdeutsch, au Kijerumani (Kijerumani sanifu kinachozungumzwa kote nchini Ujerumani).

Kwa mfano, Berliner Schnauze hutumia "j" ambapo Kijerumani fasaha hutumia "g". Lakini wengi hawafikirii kuhusu sarufi na sintaksia linapokuja suala la Berliner Schnauze. Ni tofauti na ni mtazamo unategemea hali fulani.

Berlin

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Alessandra Morisse, "Urberlinerin", au mtu ambaye amekulia katika jiji au mji huu wa Berline, anaelezea Berliner Schnauze kama lahaja na mtazamo.

"Inamaanisha kutopindapinda kwenye kuongea, uamifu wa kikatili na kwa uhuru," alisema.

"Tunasema tunachomaanisha, ambacho kinaweza kuwa mbaya kwa wengine, lakini mara tisa kati ya 10, tunamaanisha vizuri."

Sieglinde Tuschy alihamia Berlin mwaka wa 1987 lakini asili yake anatokea Franconia, eneo la kusini-kati mwa Ujerumani lililoko ndani ya jimbo la Bavaria. Kama Morisse, Tuschy anaelezea Berliner Schnauze kama lahaja na "Lebenseinstellung", au mtazamo kuelekea maisha, wa Berliners waliozaliwa na kukuzwa. Ni ya moja kwa moja, ya haraka, ya kijanja, ya kuchekesha, na, kama Rosenberg alivyosema, "schlagfertig" au lugha yenye ukali fulani, kama kupigwa "Ohrfeige" - kofi usoni.

Kwa kweli huwezi kujifunza lahaja hii, hata kama umeishi hapa kwa miongo kadhaa

"Huwezi kujifunza lahaja hii, hata kama umeishi hapa kwa miongo kadhaa," Tuschy alisema. "Jambo moja la uhakika: Ukiwa mwenyeji na unatumia namna hii ya kuzungumza ama kuwaislisha jambo (Berliner Schnauze), unajikutana unawaweka mbali wale wasio Berlin."

Berlin

Chanzo cha picha, Getty Images

Francesca Kuehler, ambaye alikulia Colorado na ameishi Dublin, Accra, na Berlin tangu 2007, ana hisia kali zaidi kuhusu Schnauze.

"Unajua jinsi wakati mwingine unaweza kunung'unika juu ya maneno au maoni ya uchokozi kuhusu mgeni?" anauliza. "Schnauze sasa tofauti, badala ya kunung'unika, unasema kwa sauti ya kubwa kiasi kwamba mtu unayemsema ama kumzungumzia anasikia. Na ni kwa makusudi."

Berliner Schnauze sio simulizi inayokuja na ubaya kwa kila mtu. Rosenberg, kwa mfano, ana kumbukumbu nzuri za Berliner Schnauze, ikiwa ni pamoja na moja ambayo ilianzia wakati wake akicheza kwenye timu ya soka ya Kampuni alipokuwa anafanya kazi.

Wachezaji wengi walikuwa "wanaojituma na kufanya kazi za kutumia nguvu" au vibarua wa aina fulani, na Rosenberg alikuwa msomi pekee kwenye timu.

Wenzake mara nyingi walikuwa wakimuuliza nini alichofanya kama msomi na kumalizia kwa swali, "Musst du da morgen wieder hin?" (Je, ni lazima urudi huko kesho?).

Rosenberg alieleza kuwa uundaji huu wa swali ulikuwa njia ya Berliner Schnauze ya kusema, "Unachofanya ni kitu kikubwa sana."

Berlin

Chanzo cha picha, Getty Images

Ilikuwa (lugha) iliyokaa vizuri sana," Rosenberg alitabasamu. Waliuliza tu kwa uzuri, 'Je, ni lazima urudi huko kesho?' Hiyo ni kawaida sana."

Licha ya umaarufu (au sifa mbaya) ya Berliner Schnauze, Rosenberg anaamini kwamba matumizi yake yamepungua kidogo. Kuanguka huku kunaonyesha mwelekeo wa jumla kati ya lahaja na lugha za kieneo.

Walakini, huko Berlin, imechochewa sio tu na mchanganyiko wa tamaduni za kimataifa, lakini na Wajerumani kutoka kote nchini kuhamia mji mkuu.

Tuschy amegundua mtindo huu pia, akisema ni nadra kumsikia Berliner Schnauze tena. Ukisikia, kwa kawaida huwa ni dereva wa basi, fundi au mtu anayefanya kazi kwenye duka la kuoka mikate. Kama Rosenberg, Tuschy anadhani ni kutokana na ongezeko la wakazi kutoka nje ya Berlin.

"Hiyo inachanganya lugha," alisema. "Na kwa hivyo, inapungua kiasi ingawa haijafa kabisa."