"Sio hatari sana." Kauli mpya za Putin kuhusu vita vya Ukraine

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa msururu wa kauli kuhusiana na vita na Ukraine. Hasa, alisema kuwa Shirikisho la Urusi "linaendeleza shughuli zake katika mwelekeo sahihi" na sio karibu na "mpaka wa hatari".
Kiongozi huyo wa Kremlin alitoa taarifa zake katika mfumo wa programu ambayo inatangazwa kwenye kituo cha TV cha serikali ya Urusi "Russia-1".
Kuhusu "mpaka wa hatari"
Alipoulizwa na mwandishi wa habari nini Urusi inapaswa kufanya ili kuondokana na "makali ya hatari" wakati wa vita, Putin alijibu kwa njia isiyo moja kwa moja, kwamba Shirikisho la Urusi "linafanya shughuli zake katika mwelekeo sahihi."
"Sidhani kama hiyo ni hatari. Nadhani tunafanya shughuli zetu kwa njia sahihi, tunalinda masilahi ya kitaifa, masilahi ya raia wetu, watu wetu. Na hatuna njia nyingine zaidi ya kulinda wananchi." - alisema.
Alipoulizwa ikiwa Shirikisho la Urusi lingeweza kufanya vinginevyo, alijibu kuwa "haiwezekani". "Tuna falsafa tofauti na mtazamo tofauti kwa watu," Putin alisema.

Chanzo cha picha, KREMLIN.RU
Kuhusu mazungumzo
Pia, Putin alikumbusha tena kwamba Urusi inaonekana kuwa "wazi kwa mazungumzo" kuhusu mwisho wa vita. Lakini alibaini kwamba mamlaka ya Ukraine ilikataza mazungumzo naye.
"Tuko tayari kujadiliana na washiriki wote katika mchakato huu kuhusu masuluhisho yanayokubalika. Lakini hii ni biashara yao, sio sisi tunaokataa kufanya mazungumzo, bali wao."
Wakati huo huo, rais wa Urusi alishutumu Magharibi kwa nia ya "kueneza Urusi ya kihistoria".
Sera ya "Gawanya na Kutawala. Hiyo ndiyo ambayo wamejaribu kufanya kila wakati, na wanajaribu kuifanya sasa. Na lengo letu ni lingine - umoja wa watu wa Kirusi, "alisema.
Kuhusu raia "wasio wazalendo" Urusi
Rais wa Shirikisho la Urusi alisema kuwa hawashutmu hasa Warusi hao ambao hawakuunga mkono vita dhidi ya Ukraine.
"Hakuna kitu cha kushangaza kwa mtazamo kwamba mtu hakuwa na tabia ya uzalendo wa kweli. Kwa sababu katika jamii yoyote kuna watu ambao wanafikiria kwanza juu ya masilahi yao binafsi, mipango fulani ya kibinafsi. Kusema kweli, mimi siwashutumu - kila mtu ana haki ya kuchagua," alisema.
Wakati huo huo, Putin ana hakika kwamba 99.9% ya Warusi wako tayari "kuweka kila kitu kando kwa maslahi ya nchi yao."

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkuu wa Kremlin kwa mara nyingine tena aliibua suala la kuipatia Ukraine mifumo ya makombora ya kupambana na ndege wa Marekani wa PATRIOT.
Ikulu ya White House ilitangaza uhamisho wa mifumo hii mipya zaidi ya ulinzi wa anga wakati wa ziara ya Rais Volodymyr Zelenskyi mnamo Desemba 21.
Baada ya hapo, Putin alisema kwamba Urusi itaharibu mifumo hii kwa urahisi.
"Bila shaka, "tutaiharibu" kwa asilimia 100%," alisema.
Alitoa kauli kama hiyo mnamo Desemba 22. Putin alisema kwamba Shirikisho la Urusi litaharibu mifumo ya Marekani na pia aliuita "wa kizamani" ikilinganishwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi.
"Wanaotupinga wanachukulia kuwa hii ni silaha ya kujihami. Oh sawa. Tukumbuke hilo tu. Na siku zote kutakuwa na njia mbadala. Kwa hiyo wanaofanya hivyo wanafanya bure. Ni kuchelewesha migogoro tu, hiyo tu,” alisema.















