Vita vya Ukraine: Rais Zelensky alifikaje Washington?

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Vlodymyr Zelensky aliwasili Washington kwa ndege ya Jeshi la Anga la Marekani

Hatua za ajabu zilizochukuliwa kumsafirisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutoka Ukraine hadi mji mkuu wa Marekani ni ishara ya jinsi uhusiano huo ulivyo muhimu kwa nchi zote mbili.

Baada ya kuzuru eneo la vita mashariki mwa Ukraine siku ya Jumanne, safari ya Bw Zelensky kuelekea Washington DC ilianza kwa treni ya usiku moja kuelekea Poland kabla ya kupanda ndege ya Jeshi la Wanahewa la Marekani, ikiripotiwa kuungwa mkono na ndege ya kijasusi ya Nato na ndege ya kivita ya F-15.

Taarifa za ziara hiyo ya Washington zilianza kusambaa mapema wiki hii, lakini haikuthibitishwa hadi mapema Jumatano asubuhi, wakati maafisa wa Marekani walihisi kuwa kiongozi wa Ukraine alikuwa njiani salama kuelekea mji mkuu wa Marekani.

Ziara hiyo ilikuwa imejadiliwa kwa miezi lakini matayarisho ya mwisho yalifanywa haraka - marais hao wawili walizungumza kuihusu tarehe 11 Disemba na mwaliko ukatolewa kwa Bw Zelensky siku tatu baadaye. Mara tu ziara hiyo ilipothibitishwa ndipo mipango ya mwisho inakaanza kutekelezwa.

Kisichoshanza, hakuna taarifa rasmi kuhusu safari iliyotolewa - usalama ni mkali karibu na ziara za rais hata wakati wa amani, lakini kwa kiongozi wa wakati wa vita hatari ni kubwa zaidi.

Kutokana na tishio la makombora ya Urusi kufanya usafiri wa anga nchini Ukraine kumekuwa hatari sana, Bw Zelensky anaonekana kuchukua safari ya siri ya treni kupitia Ukraine hadi Poland, ambako alionekana mapema Jumatano katika kituo cha reli katika mji wa mpakani wa Przemysl.

Picha kutoka kwa Televisheni ya Poland zilionyesha msafara akiwemo Bw Zelensky akitembea kwenye jukwaa na garimoshi la Ukraine la bluu na njano kwa nyuma.

Kisha kikundi hicho kiliingia kwenye msafara wa magari yanayosubiri, ikiwa ni pamoja na Chevrolet Suburbans nyeusi - mfano unaopendwa na serikali ya Marekani. Viongozi na maafisa wengi wa nchi za Magharibi wamesafiri kwa treni kumtembelea Bw Zelensky mjini Kyiv, lakini hii ilikuwa mara yake ya kwanza nje ya nchi tangu vita vya Urusi kuanza.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais Zelensky alirekodiwa katika kituo cha reli nchini Poland
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Muda mfupi baadaye, data ya ndege ilionyesha ndege ya Jeshi la Anga la Marekani Boeing C-40B - inayodhaniwa kumsafirisha Bw Zelensky - ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa Rzeszow umbali wa kilomita 80 (maili 50) kuelekea magharibi.

Ndege hiyo ilielekea kaskazini-magharibi kuelekea Uingereza, lakini kabla haijaingia kwenye anga ya juu ya Bahari ya Kaskazini, ndege ya kijasusi ya Nato ilichunguza eneo hilo. Bahari hiyo inajulikana kusimamiwa na manowari za Urusi.

Na ndege ya kivita ya Marekani F-15, iliyopaa kutoka kambi moja nchini Uingereza, ilisindikiza ndege ya Bw Zelensky katika sehemu ya safari yake.

Hatimaye, takriban saa sita mchana mjini Washington - karibu saa 10 baada ya kupaa na saa nyingi zaidi za safari kwa rais wa Ukraine - ndege ilitua karibu na Washington.

Alipofika, alipewa ulinzi wa Siri - kama ilivyo kwa wakuu wote wa nchi wanaomtembelea - lakini hali ya Bw Zelensky kama kiongozi wa nchi iliyopigana na Urusi ilimaanisha maafisa wa usalama walikuwa waangalifu zaidi.

"Tunafahamu sana kwamba Urusi ina mali katika nchi hii na inaweza kujaribu kufanya kitu," afisa mmoja mkuu aliambia ABC News. "Tunajua ni kiko hatarini."

Licha ya wasiwasi huo, ziara hiyo ilionekana kupita vizuri. Siku ya Alhamisi alisimama kwa muda nchini Poland alipokuwa akielekea nyumbani kukutana na mwenzake, Andrzej Duda.

Na kufikia Ijumaa alikuwa amerejea kwenye dawati lake mjini Kyiv, akichapisha video fupi kwenye Telegram: "Tunajitahidi kupata ushindi," alisema.