Uchaguzi wa Uingereza: Nini kimefanyika na nini kinachofuata?
Na Graeme Baker & Matt Murphy,
BBC News, Washington DC & London

Chanzo cha picha, Reuters
Chama cha Labour kimeshinda uchaguzi mkuu wa Uingereza na Sir Keir Starmer atakuwa waziri mkuu mpya.
Matokeo hayo yanahitimisha miaka 14 ya serikali ya kihafidhina, ambapo mawaziri wakuu watano tofauti wameongoza nchi.
Rishi Sunak, Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, alikubali mwendo wa saa 04:40 asubuhi, akikiri kwamba Labour walishinda na kusema kwamba amempigia simu Sir Keir kumpongeza.
Katika hotuba yake ya ushindi dakika chache baadaye, kiongozi wa chama cha Labour aliahidi "upya wa kitaifa" na kwamba angeweka "nchi kwanza, kisha chama kuwa cha pili".
Mwendesha mashtaka mkuu wa zamani na wakili wa haki za binadamu ana sababu ya kuwa na furaha - chama chake kitashinda wingi wa kura katika Bunge.
Kwa upande mwingine, Robert Buckland, waziri wa zamani wa Conservative ambaye alipoteza kiti chake, alielezea kama "Armageddon ya uchaguzi" kwa Tories.
Umekuwa usiku mrefu wa matokeo na kuna hatua nyingi zaidi zijazo. Fahamu nini kinatokea, na inamaanisha nini.
Ushindi mkubwa wa Labour
Bunge la Uingereza lina wabunge 650. Kila moja ya "viti" vyao inawakilisha eneo bunge - au sehemu fulani nchini.
Utabiri wetu wa hivi punde wa BBC unasema Labour watashinda viti 410, Conservatives watachukua 144 na Lib Dems wa mrengo wa kati watachukua 58. Reform UK, mrithi wa Chama cha Brexit, wanatazamiwa kutwaa viti vinne.
Wingi wa viti 170 unaotarajiwa katika Bunge la House of Commons wa Labor ni idadi kubwa sana lakini bado ni pungufu ya wingi wa viti 179 walivyoshinda chini ya Tony Blair katika uchaguzi wa 1997.
Lakini kwa mtazamo zaidi, ushindi wa Conservatives katika uchaguzi wa 2019 chini ya Boris Johnson - unaoonekana kama matokeo mazuri - uliwafanya kupata viti vingi - 80.
Kumbusho: Ikiwa chama kinashikilia kura nyingi, inamaanisha kwamba hakihitaji kutegemea vyama vingine kupitisha sheria. Wingi wa viti unamaanisha urahisi zaidi wa kupitisha sheria .
Vigogo waanguhswa(Baadhi waponea)
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati maeneo yametangaza matokeo yao moja kwa moja kwenye runinga - huku wagombea wote wakiwa wamesimama karibu na kila mmoja jukwaani - kumekuwa na nyakati muhimu.
Labda iliyojulikana zaidi ilikuwa kushindwa kwa Liz Truss. Waziri mkuu huyo wa zamani alihudumu kwa siku 49 pekee katika 10 Downing Street kabla ya kuondolewa na chama chake. Alipoteza kiti chake mapema Ijumaa asubuhi kulipopambazuka katika eneo bunge lake la Kusini Magharibi mwa Norfolk.
Jacob Rees-Mogg, katibu wa zamani wa biashara wa Conservative alikuwa mmoja wa majina makubwa kushindwa. Alipoteza kiti chake cha East Somerset na Hanham kwa Labor.
Aliambia BBC kwamba hawezi "kumlaumu mtu mwingine yeyote isipokuwa mimi" kwa kushindwa huko lakini alipata "afueni " kutokana na ukweli kwamba Conservatives watakuwa "angalau upinzani rasmi" - akimaanisha hofu kwamba huenda hata angepoteza fursa hiyo.
Grant Shapps, katibu wa ulinzi, alionekana kuchanganyikiwa baada ya kupoteza kiti chake kusini mwa Uingereza.
Kiongozi wa Bunge Penny Mordaunt, ambaye alichuana na Rishi Sunak kwa uongozi wa chama kabla ya kuwa waziri mkuu, pia alipoteza kiti chake.
Jeremy Hunt, ambaye anahudumu kama katibu wa Fedha - Uingereza sawa na waziri wa fedha - alishikilia kiti chake lakini kwa wingi wa kura nyingi zilizopunguzwa.
Bw Sunak pia alishinda kiti chake mjini Yorkshire kwa kura nyingi za takriban 12,000 - lakini alitumia hotuba yake kukubali na kuthibitisha kuwa chama chake kilishindwa katika uchaguzi.
Lakini ngoja, bado tunasubiri matokeo katika mashindano mengine makubwa.

Chanzo cha picha, PA Media
Waziri Mkuu mpya ndani ya siku moja
Mambo yanaenda kasi sana katika siasa za Uingereza - kuna muda mfupi sana kati ya matokeo ya uchaguzi na kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya.
Rishi Sunak atakuwa nje ya 10 Downing Street - sawa na Ikulu ya White House - ya Marekani ndani ya saa 24, na Sir Keir Starmer atachukua hatamu haraka baadaye.
Lakini kuna mchakato. Bw Sunak atawasilisha kujiuzulu kwake kwa Mfalme, na Sir Keir ataalikwa rasmi na mfalme kuunda serikali ijayo katika mkutano ambao kwa kawaida hufanyika katika Jumba la Buckingham.
Keir Starmer ni nani?
Yeye ni mgeni katika siasa, kiukweli
Sir Keir alianza maisha yake ya kitaaluma kama wakili katika miaka ya 1990, na aliteuliwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma, mwendesha mashtaka mkuu wa uhalifu nchini Uingereza na Wales, mwaka wa 2008.
Alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika eneo bunge la Holborn na St Pancras kaskazini mwa London mnamo 2015, na alichukua uongozi wa Labour baada ya uchaguzi mkuu mbaya wa chama wa 2019, akiahidi kuanza "awamu mpya" baada ya uongozi wa mrengo wa kushoto wa Jeremy Corbyn.
Sir Keir alichaguliwa tena katika eneo bunge hilo Alhamisi, akisema katika hotuba yake ya ushindi watu walikuwa "tayari kwa mabadiliko" na kuahidi "kukomesha siasa za kuigiza".
"Mabadiliko yanaanza hapa hapa kwa sababu hii ni demokrasia yako, jamii yako, maisha yako ya baadaye," alisema. "Umepiga kura. Sasa ni wakati wa sisi kufanya kazi."
Ahadi zake kuu ni zipi?
Baadhi ya ahadi za sera ambazo Leba imefanya hadi sasa ni pamoja na:
Huduma ya afya: Punguza orodha za wanaosubiri za NHS(Huduma ya Kitaifa ya Afya) kwa kuwahudumia zaidi ya watu 40,000 zaidi kila wiki, inayofadhiliwa na kukabiliana na kukwepa kodi na kufunga 'mianya' ya kodi.
Uhamiaji: Zindua ‘Kamandi usalama wa mpakani’ ili kukomesha magenge ya watu wanaosafirisha watu kwa magendo kutumia vivuko vidogo vya mashua.
Makazi: Jenga nyumba mpya 1.5m kwa kurekebisha sheria za upangaji na kuanzisha mpango wa kuwapa wanunuzi wa kwanza "kipau mbele" katika maendeleo mapya ya makazi.
Elimu: Kuajiri walimu 6,500, watakaolipwa na kumaliza misamaha ya kodi kwa shule za binafsi.
Nigel Farage hatimaye awa mbunge

Chanzo cha picha, Reuters
Chama cha waasi katika uchaguzi huu kilikuwa Reform UK, mrithi wa mrengo wa kulia wa Chama cha Brexit na Chama cha Uhuru cha Uingereza.
Nigel Farage, kiongozi wake, hatimaye alishinda kiti katika jaribio lake la nane - lakini makadirio ya awali ya chama chake ya viti 13 yalibadilika hadi vinne. Hiyo bado ni bora kuliko UKIP na Brexit Party ilivyowahi kufanya, na Bw Farage amekuwa akisherehekea.
Mgao wa kura wa chama hicho unaonekana kuwa karibu 14%.
Mageuzi yalizua utata wakati wa kampeni kuhusu kauli za kuudhi zilizotolewa na baadhi ya wagombea na wanaharakati wake.
Bw Farage atajumuika katika Bunge la House of Commons na aliyekuwa naibu mwenyekiti wa chama cha Conservative Lee Anderson, mwanzilishi wa Reform UK Richard Tice na Rupert Lowe.
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah












