Samsung inatarajia faida kuongezeka kwa zaidi ya 1,400%
Wasiwasi waibuka juu ya ripoti za Orban kuzuru Moscow
Sunak akubali kuwajibika kwa kushindwa kwa kihistoria kwa chama cha Tory
Chama cha Labour chashinda uchaguzi mkuu wa Uingereza
Hezbollah yarusha roketi 200 na ndege zisizo na rubani nchini Israel
Biden akabiliwa na shinikizo la wafadhili anaposisitiza kusalia kwenye kinyang'anyiro
Keir Starmer atarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza
Moja kwa moja
Na Ambia Hirsi & Yusuf Jumah & Dinah Gahamanyi
Eto'o atozwa faini ya $200,000 huku akiepuka malipo ya kupanga matokeo
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Samuel Eto'o alichaguliwa kuwa rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon mnamo Desemba 2021
Shirikisho la soka barani Afrika limemtoza faini ya $200,000 rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto'o, kwa ukiukaji wa maadili, lakini ikapata ushahidi wa kutosha kuendelea na mashtaka yanayohusiana na madai ya upangaji matokeo.
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lilianzisha uchunguzi kuhusu mwenendo wa Eto'o mwezi Agosti mwaka jana baada ya kupokea "taarifa zilizoandikwa kutoka kwa wadau kadhaa wa soka wa Cameroon".
Jopo la nidhamu lilibaini kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne "amekiuka kwa kiasi kikubwa kanuni za maadili, uadilifu na uanamichezo" za Caf kwa kutia saini mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya kamari ya 1XBET.
Mawakili wa Eto'o wamesema watakata rufaa kupinga hukumu hiyo.
Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer atangaza baraza la mawaziri
Kufuatia ushindi wa
kishindo wa uchaguzi wa Labour, Waziri Mkuu Keir Starmer ametangaza uteuzi
kadhaa muhimu kwa Baraza lake jipya la Mawaziri.
Angela Rayner ameteuliwa kuwa naibu waziri mkuu na katibu wa
serikali kwa usawa, makazi na jamii.
Rayner, mwanasiasa mashuhuri wa Chama cha Labour, anatazamiwa
kuchukua jukumu muhimu katika kuendesha ajenda ya serikali kuhusu usawa wa
kijamii na mageuzi ya makazi.
Rachel Reeves pia aliweka historia kwa kuwa kansela mwanamke wa
kwanza Uingereza wa Hazina.
David Lammy aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya
nje, akisimamia uhusiano wa kimataifa wa Uingereza wakati wa kipindi muhimu
kilichoangaziwa na changamoto za kiuchumi za kimataifa na mivutano ya
kijiografia.
Yvette Cooper ameteuliwa
kuwa Waziri wa mambo ya ndani, aliyepewa jukumu la kusimamia usalama wa ndani
wa taifa, uhamiaji, na sheria na utulivu.
John Healey atahudumu kama Waziri wa ulinzi, wadhifa unaohusika
na mkakati wa ulinzi wa nchi na vikosi vya jeshi.
Kwengineko:
Kundi la wanasiasa maarufu wa Concervertive wamepoteza viti vyao - ikiwa ni pamoja na Penny Mordaunt, Grant Shapps na Jacob Rees-Mogg - ingawa Jeremy Hunt ameweza kuhifadhi kiti chake.
Kiongozi wa chama cha Liberal Demecratic Sir Ed Davey anakodolea macho matokeo bora zaidi ya chama chake kwa karne moja, huku BBC ikitoa viti vingi vya rangi ya njano katika hali nzuri tangu 2019.
Kumekuwa na tukio ambalo halikutarajiwa kwa Labour huko Islington Kaskazini, ambapo kiongozi wake wa zamani Jeremy Corbyn ameshinda kama mtu huru
Kiongozi wa mageuzi nchini Uingereza Nigel Farage ameshinda kiti cha ubunge, baada ya kugombea kwa mara ya nane ya kugombea akiwaambia waliompigia kura kuwa chama chake "kitapambana na Labour" katika uchaguzi
Kiongozi wa Kenya akabiliana na vijana wenye hasira kwenye mjadala mtandaoni
Chanzo cha picha, @WillianRuto
Maelezo ya picha, Kikao hicho cha saa tatu kinanuiwa kuwa fursa kwa vijana kuzungumza moja kwa moja na Rais Ruto.
Rais wa Kenya William Ruto ameomba msamaha kwa ukatili
wa polisi katika kongamano la mtandaoni na waandamanaji wanaopinga ushuru
kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Alikuwa akimjibu Kevin Monari, mmoja wa viongozi wa
maandamano ambaye alimweleza jinsi alivyotekwa nyara na vikosi vya usalama.
Maandamano ya hivi majuzi yalimlazimu Bw Ruto kuondoa mswada
wake wa fedha uliozua utata na ambayo yametikisa urais wake. Mazungumzo hayo
yalipangwa kupitiajukwaa la za X - Twitter Space , kipengele kinachoruhusu watumiaji
kupangisha mazungumzo ya moja kwa moja ya sauti na wengine kwenye jukwaa
lililojulikana kama Twitter.
Kipindi cha X cha Bw Ruto, kilichopewa jina la
#EngageThePresident, kilianza kwa zaidi ya saa moja kuchelewa, huku kikiwa na
matatizo ya kiufundi - na kilipangwa kudumu kwa saa tatu.
Baadhi ya Wakenya kwenye X waliapa kususia mazungumzo ya
rais na kupanga Nafasi sambamba ili kukabiliana na mazungumzo hayo - kwani
hawakutaka adhibiti wa ni nani angeweza kuzungumza.
Hata hivyo, mijadala ndani ya X Space ya rais, ambapo watu
125,000 wanasikiliza, yamekuwa ya wazi - wengine wakimwita mwongo na kumshutumu
kwa kukosa huruma - shutuma ambazo amezikanusha
Katika picha: Uhamisho wa madaraka kwa amani (na haraka) Uingereza
Makabidhiano ya mamlaka katika siasa za Uingereza ni ya haraka kikatili, ikiwa ni saa chache kati ya Rishi Sunak kujiuzulu na Keir Starmer kualikwa kuunda serikali.
Wote wawili walikuwa na mikutano ya faragha na Mfalme, waliunganishwa na wenzi wao kuwashukuru wafuasi na waliozungumza kwa muda kadhaa huku wakiwa wamesimama nje ya milango ya Nambari 10.
Mmoja alitoka katika Barabara ya Downing kwa mara ya mwisho, wakati mwingine akiwa ndio anaingia kwa mara ya kwanza kama Waziri mkuu.
Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Mchakato ulianza wakati Sunak alikutana na Mfalme Charles kujiuzulu - jadi maelezo ya mazungumzo kati ya mfalme na mawaziri wakuu yanafichwa.
Chanzo cha picha, NO 10 DOWNING STREET
Maelezo ya picha, Dakika chache baada ya kuondoka Buckingham Palace, Sunak na mkewe Akshata Murty waliwashukuru wale waliomfanyia kazi ndani ya Downing Street, kabla ya kuelekea nje kutoa hotuba yake ya mwisho.
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Keir Starmer kisha alikutana na Mfalme, ili kualikwa kuunda serikali mpya katika sherehe inayojulikana kama "kumbusu mikono" - ingawa kwa akaunti zote hakuna pete au nambari zinazopigwa busu tena kama sehemu yake.
Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Starmer na mkewe Victoria pia walilakiwa na wafanyakazi wa kusubiri baada ya kuingia nambari 10 kwa mara ya kwanza, kufuatia hotuba yake ya kwanza kama waziri mkuu.
Kwengineko:
Kundi la wanasiasa maarufu wa Concervertive wamepoteza viti vyao - ikiwa ni pamoja na Penny Mordaunt, Grant Shapps na Jacob Rees-Mogg - ingawa Jeremy Hunt ameweza kuhifadhi kiti chake.
Kiongozi wa chama cha Liberal Demecratic Sir Ed Davey anakodolea macho matokeo bora zaidi ya chama chake kwa karne moja, huku BBC ikitoa viti vingi vya rangi ya njano katika hali nzuri tangu 2019.
Kumekuwa na tukio ambalo halikutarajiwa kwa Labour huko Islington Kaskazini, ambapo kiongozi wake wa zamani Jeremy Corbyn ameshinda kama mtu huru
Kiongozi wa mageuzi nchini Uingereza Nigel Farage ameshinda kiti cha ubunge, baada ya kugombea kwa mara ya nane ya kugombea akiwaambia waliompigia kura kuwa chama chake "kitapambana na Labour" katika uchaguzi
Ujerumani yakabidhi mfumo wa tatu wa ulinzi wa anga wa Patriot kwa Ukraine
Chanzo cha picha, Getty Images
Mfumo wa tatu wa makombora ya kupambana na ndege ya Patriot kutoka Ujerumani umewasili Ukraine, Balozi wa Ujerumani nchini Kyiv Martin Jaeger amesema.
Ujerumani imehamisha mifumo miwili ya kwanza ya ulinzi wa anga ya Patriot na risasi zake kwa Ukraine mnamo 2023.
Kupelekwa kwa Ukraine kwa mfumo wa tatu wa Patriot, pamoja na IRIS-T, mitambo ya Gepard, makombora na risasi, kulitangazwa mnamo Juni 11 na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.
Hapo awali, Ikulu ya White House ilithibitisha kuwa makombora mapya ya Patriot yatatumwa Ukraine kama kipaumbele.
Ukraine mara nyingi imekuwa ikihusisha vifo vya Urusi na mafanikio ya kimaeneo na uhaba wa risasi na makombora ya ulinzi wa anga unaosababishwa na kucheleweshwa kwa msaada wa kijeshi wa nchi za Magharibi.
Unaweza pia kusoma:
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Nitapambana hadi muamini katika kile ambacho serikali inaweza kufanya, asema Starmer
Chanzo cha picha, POOL
Starmer anasema ikiwa angeuliza watu sasa ikiwa wanaamini Uingereza itakuwa bora kwa watoto wao, wengi
wangekataa.
Lakini, ameendelea
kusema, serikali yake itapambana kuwashawishi “mpaka mtakapoamini tena”.
Anasema
serikali yake haitatachoshwa na mafundisho.
Starmer anakubali kwamba mabadiliko yanaweza
kuchukua muda
Starmer anasema "kubadilisha nchi si kama kugeuza swichi" kwani
anakubali ulimwengu "una hali tete zaidi".
"Itachukua muda," anaongeza lakini anasema kazi ya kubadilisha
itaanza mara moja.
Starmer ameuambia
umati sasa kwamba kwa muda mrefu sana, jicho la upofu limegeuzwa huku
"mamilioni ya watu wakiingia kwenye ukosefu mkubwa wa usalama".
Amesema
kuwa watu wanafanya kazi kwa bidii na
kufanya jambo sahihi, lakini "kamera zinapoacha kufanya kazi, maisha yao
yanapuuzwa".
"Nataka kusema kwa uwazi sana kwa watu hao - sio
wakati huu," anasema.
Kwengineko:
Kundi la wanasiasa maarufu wa Concervertive wamepoteza viti vyao - ikiwa ni pamoja na Penny Mordaunt, Grant Shapps na Jacob Rees-Mogg - ingawa Jeremy Hunt ameweza kuhifadhi kiti chake.
Kiongozi wa chama cha Liberal Demecratic Sir Ed Davey anakodolea macho matokeo bora zaidi ya chama chake kwa karne moja, huku BBC ikitoa viti vingi vya rangi ya njano katika hali nzuri tangu 2019.
Kumekuwa na tukio ambalo halikutarajiwa kwa Labour huko Islington Kaskazini, ambapo kiongozi wake wa zamani Jeremy Corbyn ameshinda kama mtu huru
Kiongozi wa mageuzi nchini Uingereza Nigel Farage ameshinda kiti cha ubunge, baada ya kugombea kwa mara ya nane ya kugombea akiwaambia waliompigia kura kuwa chama chake "kitapambana na Labour" katika uchaguzi ujao.
Habari za hivi punde, Rais William Ruto ateua kikosi kazi huru cha kufanya ukaguzi wa madeni ya umma.
Chanzo cha picha, Reuters
Akihutubia taifa siku ya Ijumaa kutoka Ikulu, alibainisha
kuwa deni la umma linaendelea kuwa sehemu kubwa ya ushiriki na mazungumzo
nchini Kenya.
"Leo nimeteua kikosi kazi huru cha kufanya ukaguzi wa
kina juu ya deni la umma na kuripoti kwetu katika miezi mitatu ijayo,"
alisema.
Rais Ruto
amesema idadi ya washauri serikalini itapunguzwa kwa asilimia 50.
"Idadi ya
washauri katika serikali itapunguzwa kwa asilimia 50 ndani ya utumishi wa umma
kwa haraka," alisema.
Rais wa
Kenya William Rito amesema bajeti zilizokuwa
zimetengewa ofisi ya Mke wa Rais na Naibu Mke wa Rais, na Mke wa Waziri Kiongozi zimeondolewa.
Amesema pia kwamba kwamba mpango
wa kuwaajiri maafisa wakuu wa utawala umesitishwa na idade ya washauri wa
serikali imepunguzwa kwa 50%, huku akithangaza kukatwa kwa 50% ya bajeti ya
ukarabati wa majengo ya serikali.
Baada ya malalamiko kuhusu ziara
za viongozi wa kiserikali na bunge nje ya nchi kutoka kwa umma wa Wakenya, Rais
Ruto ametangaza kuwaziara zisizo muhimu za viongozi zimesitishwa.
Katika hotuba hiyo Bw Ruto ametangaza kuwa
utoaji wa michango ya pesa za misaada kwa
viongozi wa serikali al maarufu Harambee umesimamishwa na badala yake serikali
itaweka mfumo wa utoaji wa misaada hiyo.
Amesema mabadiliko haya yanalenga kuboresha
huduma za serikali kwa umma na kuhakikisha wananchi wanapata huduma kamili
wanazohitaji kutoka kwa serikali.
Haya
yanajiri huku Rais William Ruto akitoa mwaliko wa
mazungumzo yaliyopewa jina la "Engage" mtandaoni kupitia X Space kati
yake na vijana, wengi wao "Gen Z," ambao wamekuwa wakiandamana
kupinga nyongeza ya ushuru tangu tarehe 18 Juni.
Maandamano hayo ambayo yamegeuka na kuwa maandamano ya kuipinga serikali
kutokana na masuala ambayo hayajashughulikiwa, yamesababisha vifo vya zaidi ya
watu 40, huku mamia wakijeruhiwa au kukamatwa.
Kenya - Rais Ruto atoa mwaliko wa majadiliano ya X Space na Gen Z
Chanzo cha picha, EPA
Rais William Ruto ametoa mwaliko wa mazungumzo yaliyopewa jina la "Engage" mtandaoni kupitia X Space kati yake na vijana, wengi wao "Gen Z," ambao wamekuwa wakiandamana kupinga nyongeza ya ushuru tangu tarehe 18 Juni.
Maandamano hayo ambayo yamegeuka na kuwa maandamano ya kuipinga serikali kutokana na masuala ambayo hayajashughulikiwa, yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 40, huku mamia wakijeruhiwa au kukamatwa.
Baadhi ya vijana wanaonekana kutovutiwa na mazungumzo hayo na badala yake wameamua kuandaa mjadala sambamba wa X unaoitwa "Rage".
Haya ni matukio ambayo hayajawahi kushuhudiwa, huku zama za kidijitali zikifafanua upya mienendo ya mikutano ya kisiasa.
Mchambuzi anayataja kuwa mgongano wa kihistoria wa vizazi kupitia teknolojia.
Baada ya usiku wa kusikitisha kwa Conservatives, hapa kuna taswira ya ni wanachama gani wa chama cha Tory ambao waliponea katika uchaguzi mkuu wa Uingereza .
Wanachama wa baraza la mawaziri la Sunak walioponea katika uchaguzi mkuu
Maelezo ya picha, Michael Gove,Chris Heaton-Harris na Alistair Jack hawakugombea kutetea viti vyao ilhali David Cameron na Lord True wabunge wa kuteuliwa(Life Peers)
Keir Starmer ni nani?
Yeye ni mgeni katika siasa, kiukweli
Sir Keir alianza maisha yake ya kitaaluma kama wakili katika miaka ya 1990, na aliteuliwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma, mwendesha mashtaka mkuu wa uhalifu nchini Uingereza na Wales, mwaka wa 2008.
Alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika eneo bunge la Holborn na St Pancras kaskazini mwa London mnamo 2015, na alichukua uongozi wa Labour baada ya uchaguzi mkuu mbaya wa chama wa 2019, akiahidi kuanza "awamu mpya" baada ya uongozi wa mrengo wa kushoto wa Jeremy Corbyn.
Sir Keir alichaguliwa tena katika eneo bunge hilo Alhamisi, akisema katika hotuba yake ya ushindi watu walikuwa "tayari kwa mabadiliko" na kuahidi "kukomesha siasa za kuigiza".
"Mabadiliko yanaanza hapa hapa kwa sababu hii ni demokrasia yako, jamii yako, maisha yako ya baadaye," alisema. "Umepiga kura. Sasa ni wakati wa sisi kufanya kazi." Soma zaidi ili kufahamu ahadi za chama chake
Samsung inatarajia faida kuongezeka kwa zaidi ya 1,400%
Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni ya Samsung Electronics inatarajia faida yake kwa miezi mitatu hadi Juni 2024 kupanda mara 15 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Kuongezeka kwa kasi kwa Akili Mnemba (AI) kumeongeza bei za chipu za hali ya juu, na hivyo kuongeza utabiri wa kampuni katika robo ya pili.
Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ya Korea Kusini ndio mtengenezaji mkubwa zaidi duniani wa chipu za data , simu za rununu na televisheni.
Tangazo hilo lilisongesha hisa za Samsung hadi zaidi ya 2% wakati wa saa za mapema za biashara huko Seoul.
Kampuni hiyo pia iliripoti kuongezeka kwa zaidi ya mara 10 kwa faida yake kwa miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu.
Katika robo hii, ilisema inatarajia faida yake kupanda hadi 10.4tn won ($7.54bn; £5.9bn), kutoka 670bn iliyopata mwaka jana.
Wasiwasi waibuka juu ya ripoti za Orban kuzuru Moscow
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Viktor Orban amekuwa mkosoaji mkubwa wa uungaji mkono wa Magharibi kwa Ukraine
Viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya wameelezea wasiwasi wao kuhusu ripoti za vyombo vya habari kwamba Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban huenda atakutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow siku ya Ijumaa.
Bw Orban - ambaye nchi yake sasa inashikilia urais wa zamu wa EU - ndiye mkuu pekee wa serikali ya kitaifa ya umoja huo kuwa na uhusiano wa karibu na Kremlin kufuatia uvamizi wake Ukraine mnamo 2022.
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisema Bw Orban "hakuwa na mamlaka ya kuwasiliana na Urusi kwa niaba ya EU", huku Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk akiomba ufafanuzi.
Vyombo kadhaa vya habari viliripoti kuhusu ziara ya Bw Orban, vikinukuu vyanzo vyao.
Gazeti la Financial Times lilisema maafisa mmoja wa Hungary na wawili wa Umoja wa Ulaya wamethibitisha ripoti za vyombo vya habari kwamba Bw Orban atakutana na rais wa Urusi siku ya Ijumaa.
Radio Free Europe/Radio Liberty, shirika la vyombo vya habari linalofadhiliwa na serikali ya Marekani, lilinukuu chanzo cha serikali ya Hungary.
Pia ilisema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary Peter Szijjarto ataandamana na Bw Orban.
Hungary na Urusi hazikujibu ombi la BBC la kuthibitisha ripoti hizo.
Mnamo Jumatatu, kulingana na shirika la habari la AFP, Bw Orban aliahidi "habari za kushangaza kutoka sehemu za kushangaza".
Sunak akubali kuwajibika kwa kushindwa kwa kihistoria kwa chama cha Tory
Rishi Sunak amesema anakubali kuwajibika kwa kushindwa kwa kihistoria katika uchaguzi mkuu wa chama cha Conservative.
Sir Keir Starmer amekiongoza chama cha Labour kwa ushindi mkubwa na atachukua nafasi ya Bw Sunak kama waziri mkuu wa Uingereza.
Bw Sunak aliwaambia wafuasi wake: "Watu wa Uingereza wametoa uamuzi mzito usiku wa leo, kuna mengi ya kujifunza... na ninawajibika kwa kushindwa huko."
Akizungumza katikati mwa London, Sir Keir alisema "mabadiliko yanaanza sasa", na kuongeza "Najihisi vizuri, lazima niwe mkweli".
Huku zaidi ya viti 500 kati ya 650 vikiwa vimetangazwa, Labour inakadiriwa kuunda serikali ijayo, yenye wingi wa viti 166.
Tories imeandikisha matokeo mabaya zaidi katika historia yao. Wamepoteza zaidi ya viti 170 na wanatabiriwa kubakia na wabunge 136 pekee.
Sir Keir aliwaambia wafuasi wa chama cha Labour waliokuwa wakishangilia kuwa nchi hiyo inaamka kwa "mwanga wa jua wa matumaini" ambao "unaangazia kwa mara nyingine tena nchi yenye fursa baada ya miaka 14 ya kurejesha mustakabali wake."
Habari za hivi punde, Chama cha Labour chashinda uchaguzi mkuu wa Uingereza
Chanzo cha picha, Getty Images
Chama cha Labour kimeshinda rasmi uchaguzi mkuu wa Uingereza 2024 baada ya kufikisha viti 326 vinavyohitajika.
Akizungumza mjini London, waziri mkuu mtarajiwa Keir Starmer anasema "mabadiliko yanaanza sasa".
"Nahisi vizuri, lazima niseme ukweli," aliuambia umati wa watu waliokuwa wakishangilia.
Akizungumza muda mfupi kabla ya Sir Keir, Waziri
Mkuu anayeondoka Rishi Sunak alikubali kushindwa, na kuwaambia Tories wenzake
ilikuwa "uamuzi wa kutisha"
Kwengineko:
Kundi la wanasiasa maarufu wa Concervertive wamepoteza viti vyao -
ikiwa ni pamoja na Penny Mordaunt, Grant Shapps na Jacob Rees-Mogg - ingawa
Jeremy Hunt ameweza kuhifadhi kiti chake.
Kiongozi wa chama cha Liberal Demecratic Sir Ed Davey
anakodolea macho matokeo bora zaidi ya chama chake kwa karne moja, huku BBC
ikitoa viti vingi vya rangi ya njano katika hali nzuri tangu 2019.
Kumekuwa na tukio ambalo halikutarajiwa kwa Labour huko
Islington Kaskazini, ambapo kiongozi wake wa zamani Jeremy Corbyn ameshinda
kama mtu huru
Kiongozi wa mageuzi
nchini Uingereza Nigel Farage ameshinda kiti cha ubunge, baada ya kugombea kwa mara ya nane ya kugombea akiwaambia waliompigia
kura kuwa chama chake "kitapambana na Labour" katika uchaguzi ujao.
Hezbollah yarusha roketi 200 na ndege zisizo na rubani nchini Israel
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Roketi na ndege zisizo na rubani za Hezbollah zilisababisha mioto kadhaa kaskazini mwa Israel
Kundi la Hezbollah kutoka nchini Lebanon limerusha zaidi ya roketi 200 na ndege zisizo na rubani kaskazini mwa Israel, kujibu mauaji ya mmoja wa makamanda wake wakuu.
Jeshi la Israel limesema kuwa afisa wake mmoja aliuawa katika shambulio hilo ambalo lilizua mioto kadhaa.
Jeshi pia lilisema lililenga "miundo ya kijeshi" ya Hezbollah na shabaha zingine kusini mwa Lebanon kujibu shambulio hilo.
Vyombo vya habari vya Lebanon vimeripoti kuwa mtu mmoja aliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Israel katika mji wa Houla.
Kamanda wa Hezbollah aliyeuawa katika shambulizi la anga la Israel karibu na mji wa Tiro, kusini mwa Lebanon, Mohammed Nimah Nasser, alikuwa mmoja wa viongozi waandamizi wa kundi hilo kuuawa katika mzozo huo
Jeshi la Israel lilisema Nasser aliamuru Kitengo cha Aziz cha Hezbollah, ambacho kinahusika na kurusha roketi kutoka kusini-magharibi mwa Lebanon, na kumshutumu kwa kuongoza "idadi kubwa ya mashambulizi ya kigaidi".
Pia ilimtaja kama "mwenzake" wa Taleb Sami Abdullah, kamanda wa kitengo kingine ambaye mauaji ya mwezi uliopita yaliifanya Hezbollah kurusha zaidi ya roketi 200 na makombora kaskazini mwa Israel kwa siku moja.
Biden akabiliwa na shinikizo la wafadhili anaposisitiza kusalia kwenye kinyang'anyiro
Chanzo cha picha, Reuters
Rais Joe Biden anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wafadhili wakuu wa chama cha Democratic huku akikabiliwa na siku chache muhimu katika kampeni yake ya kuchaguliwa tena.
Baadhi ya wafadhili wanaonya hadharani kuwa watazuia mchango wao iwapi Bw Biden hatabadilishwa kama mgombeaji wa chama kufuatia utendaji wake mbaya wa mjadala wiki jana.
Wanajumuisha Abigail Disney, mrithi wa familia ya Disney, mtayarishaji wa filamu wa Hollywood Damon Lindelof, wakala wa Hollywood Ari Emanuel, na mfadhili na mjasiriamali Gideon Stein.
Bwana Biden anatafuta kuinua ugombea wake wikendi hii, pamoja na mahojiano adimu ya televisheni siku ya Ijumaa na mkutano wa hadhara huko Wisconsin.
Shinikizo kwa Bw Biden, 81, kujiuzulu limeongezeka kufuatia mjadala ulioshuhudia matukio kadhaa ambapo alipoteza mtiririko wa mawazo yake mengi na hakueleweka.
Ingawa alikiri kwamba "alifeli" usiku huo, ameapa kusalia kama mgombea wa chama chake kukabiliana na Donald Trump katika uchaguzi wa urais wa Novemba.
Keir Starmer atarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza
Chama cha Labour kinakaribia kupata ushindi wa
kishindo huku Conservetive kikikabiliwa na hali mbaya zaidi katika uchaguzi
mkuu kuwahi kushuhudiwa, matokeo ya awali yanaashiria.
Sir Keir Starmer anaelekea Downing Street akiwa na
idadi kubwa ya wabunge 160, kulingana na makadirio ya BBC na viti zaidi ya 160
vilivyotangazwa, vichache kiasi kuliko ilivyotabiriwa na kura ya maoni.
Katika hotuba yake ya ushindi wa eneo bunge,
kiongozi huyo wa chama cha Labour alisema ni "wakati wa sisi kutoa".
Conservertive wanatabiriwa kuishia na wabunge 154, idadi
ya juu kidogo kuliko ilivyotabiriwa na kura ya maoni, lakini bado ni matokeo
yao mabaya zaidi kuwahi kutokea.
Chama cha Kitaifa cha Scotland sasa kinatabiriwa kupunguzwa hadi wabunge sita pekee.
Kiongozi wa mageuzi wa Uingereza Nigel Farage ameshinda kiti cha ubunge katika jaribio lake la nane, mjini Clacton, na kuahidi "hii ni hatua ya kwanza tu ya jambo ambalo litawashangaza nyote".
Chama cha Liberal Democrats pia kinatazamiwa kufaidika kutokana na kuporomoka kwa uungwaji mkono wa wahafidhina na wanatabiriwa kupata wabunge 56, upungufu wa wabunge 61 waliotabiriwa na kura ya maoni lakini bado ni matokeo yao bora zaidi tangu 2010.