Je, Hezbollah italiweka jeshi la Israel kwenye mtihani mgumu?

xc

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Hezbollah wa Lebanon wakiwa kwenye gari la kurushia roketi, katika kijiji cha Armta, kusini mwa Lebanon, Mei 21, 2023.

Gazeti la Uingereza la Times, limeandika juu ya mapigano kati ya Israel na Hezbollah ya Lebanon. Roger Boyes, mwandishi wa makala hiyo, anauliza maswali kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

Vita hivi vinaweza kulipeleka wapi eneo hilo? Je, ni kiasi gani cha athari kwa jeshi la Israel na uwezo wake? Je, vita hivi vitaujaribu uwezo wa Israel? Je, Israel itafaulu mtihani huu ikiwa itauingia?

Mwandishi huyo anasema: “Vitengo vya kigaidi vya Hezbollah, ambavyo wanachama wake huvaa vitambaa vyekundu, vimeahidi kuendeleza vita dhidi ya Israel.

Pia vimeonyesha kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii kuhusu walipuaji wa kujitoa mhanga 1,500 ambao wametangaza kuwa tayari kuivamia Milima ya Golan, ambayo inakaliwa kwa mabavu na Israel.

“Mvutano huu unaibua mabadiliko Mashariki ya Kati - ambayo yanaweza kusababisha kupanuka kwa mzozo katika eneo hilo, wakati ambapo juhudi za Israel zenye lengo la kuwaondoa Hamas huko Rafah zimeanza kupungua huku macho yakielekea kaskazini, kwenye mstari mrefu wa mpaka na Lebanon.

Hezbollah ilitangaza haitaacha kushambulia maeneo ya Israel, hadi makubaliano ya amani ya kusitisha mapigano huko Gaza yaafikiwe.

Netanyahu bado hajajibu swali la mustakbali wa Gaza baada ya vita, huku majenerali wake wakikataa wazo la ukaliaji wa kijeshi wa Ukanda huo kwa muda mrefu, kwa sababu unaweza kusababisha kudhoofika kwa uwezo wa jeshi la Israel.

Au mgogoro huo ukadumu kwa muda mrefu, na ikiwa Hamas haitoendelea kuwa na nguvu za kijeshi na kisiasa, itaendelea kuwa tishio kama kikundi cha wahalifu au kikundi cha mamluki .

Mwandishi anadokeza, kupanuka kwa mzozo huo na kuanza vita vya moja kwa moja na Hezbollah, na kufanya operesheni ndefu zaidi ya kijeshi kwa kutuma wanajeshi, ambao wengi wao wanatoka vikosi vya akiba, wakiwa tayari wamechoka, utakuwa mtihani kwa Israel.

Kwa upande mwingine, wanachama wa Hezbollah wana silaha mafunzo na vifaa bora zaidi ikilinganishwa na Hamas, jambo ambalo linaleta changamoto kwa majeshi ya Israel na kuuweka uwezo wao wa kupambana katika mtihani mgumu.

Mzozo wa Biden na Netanyahu

df

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Kuna tofauti za wazi kati ya Biden na Netanyahu kuhusu hatima ya Gaza baada ya vita
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Gazeti la Kiarabu la Al-Quds, limechapisha makala ya Gilbert Al-Ashqar, inayojadili kwa kina hali ya kisiasa ya Israel na uhusiano wa Marekani na Israel.

Operesheni ya 'Mafuriko ya Al-Aqsa' iliigeuza hali ya kisiasa ya Israel kuwa hasara kwa Netanyahu na kambi tawala pamoja na Baraza la vita aliloliunda baada ya uvamizi wa Hamas.

Lakini ujanja wa kisiasa uliofanywa na Netanyahu ili kupunguza hasira za watu wa Israel, baada ya shambulio hilo, ilikuwa ni uundaji wa "baraza la vita," lililojumuisha wakuu wawili wa zamani wa jeshi la Israeli; Benny Gantz na Gadi Eisenkot.

Lakini baraza hili lilipasuka kuhusu mustakabali wa kisiasa wa Gaza baada ya vita. Netanyahu bado hana jibu kuhusu Gaza itakuwaje baada ya vita.

Lakini Rais wa Marekani, Joe Biden anaamini suluhu ni "kulifanya eneo la Gaza na eneo la Ukingo wa Magharibi kuwa eneo moja la Palestina' linalotawaliwa na 'Mamlaka ya Palestina' chini ya usimamizi wa pamoja wa jeshi la Israel na Magharibi kwa kupitia usimamizi wa kijeshi wa Egypt.

Mwandishi anagusia juu ya kile anachokiona kama hila za kisiasa zinazofanywa na Netanyahu, ambazo zinalenga kusaka manufaa kwa dola ya Kiyahudi na kudumisha umoja ndani yake.

Lakini atalifanya hilo kwa njia ambayo inakinzana na sera za Marekani ambazo White House inataka kuziweka katika kanda hiyo, ili kusaidia Netanyahu kupata uungwaji mkono zaidi.

Kurudi kwa Boris Johnson

SD

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Boris Johnson

Makala iliyochapishwa katika gazeti la Uingereza, the Independent na Andrew Grace, inaelezea juu ya safari ya kisiasa ya Boris Johnson.

Boris Johnson, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, anaweza kuwa njiani kurejea Chama tawala cha Conservative, lakini safari hii anarudi katika sura ya mwokozi wa chama.

Lakini sio dhidi ya Theresa May au Chama cha Labour, bali dhidi ya Nigel Farage. Nia ya Johnson ni kuanzisha kampeni ili kudhibiti ushawishi wa wahafidhina baada ya kushindwa vibaya katika chaguzi zilizopita.

"Si ajabu kurejea Johnson kwenye jukwaa la kisiasa, wafuasi wa Chama cha Conservative cha Uingereza wanatarajia kupokea barua pepe kutoka kwa Johnson inayowataka kumzuia Farage, hasa kwa kuwa chama chake cha mageuzi (UK Reform), anachokiongoza, kinazidi kupata wafuasi kukikaribia chama cha Conservative.

Kuna baadhi ya viongozi wa Chama cha Conservative, kama vile, Suella Braverman, na Robert Jenrick, wanaotaka Nigel ajiunge na Conservatives, na kumpa nafasi katika chama ikiwa atachaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Commons.

Kampeni za Boris Johnson na Nigel Farage wakati wa Brexit 2016, kila mmoja alikuwa mkuu wa kampeni zake –ili kuitoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, lakini kampeni zao zilitoka pande mbili tofauti.

Ingawa wanachama wengi wa Chama cha Conservative walitamani Johnson angepoteza uchaguzi uliopita, Waziri Mkuu huyo wa zamani hakumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama cha Conservative, Rishi Sunak.

Makala za Sunak katika gazeti la Daily Mail, hazikuwa na shambulio lolote dhidi ya Johnson, akimshambulia tu Keir Strmer, kiongozi wa Chama cha Labour cha Uingereza.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Seif Abdalla