Uchaguzi mkuu 2019: Kwa nini uchaguzi huu wa Uingereza ni muhimu sana

Jeremy Corbyn na Boris Johnson

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Tabia za Corbyn na Johsnon zimetawala kampeni hizo

Huku wapiga kura wa Uingereza wakijiandaa kushiriki katika uchaguzi muhimu- ukiwa ni wa tatu mwaka huu - wanakabiliwa na chaguo gumu, linalohusisha viongozi wawili wasiopendwa.

Nick Boles mbunge wa zamani wa chama cha uhafidhina anasema kwamba wanakabiliwa na 'chaguo la kutisha' kati ya mtu 'asiyeaminika na dikteta'.

Ni kama uchaguzi wa urais 2016 ambapo wagombea wote walionekana kuwa na 'dosari na wasioaminik'a na swala hilo linaonekana tena miaka mitatu baadaye katika upande wa pili wa Atlantic.

'Watu wana wasiwasi na kusema kwamba wamechoka'', Mary Roberts mgombea wa chama cha Leba katika eneo bunge la Kaskazini mwa Wales la Ynys Mon, aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara siku ya Jumapili.

Hilo linafanya mambo kuwa magumu.

Je Johnson anaaminika?

Hii ni fursa ya kwanza ya Johnson kusimama mbele ya wapiga kura wa Uingereza kama waziri mkuu wa Uingereza.

Ni uchaguzi alioutaka licha ya kwamba kampeni zenyewe hazijakosa pandashuka.

Wakosoaji wamezua hofu kuhusu uaminifu wake swala muhimu wakati ambapo Johnson anajaribu kuwahakikishia wapiga kura kwamba anaweza kuiongoza Uingreza nje ya Muungano wa Ulaya ifikiapo mwisho wa Januari na baadaye afuatilie hilo na mazungumzo mazuri ya uhusiano wa kibiashara.

Wengi wamedai kumekuwa na msururu wa ahadi ambazo hazikutekelezwa, ikiwemo matamshi ya kupotosha , kuhusu bima ya afya, na mipango yake ya kujiondoa kwa Ireland kaskaizni.

Pia amekosolewa kwa kukataa kuzungumzia kuhusu idadi ya watoto alionao, swala ambalo pia liliangaziwa na vyombo vya habari vya Marekani.

Swala linalojiri mara kwa mara katika maswali yetu ni uaminifu, mwandishi wa BBC Andrew Neil alisema katika mahojiano aliojiandaa kumfanyia Johnson .

Na kwa nini mara nyingi katika kipindi chake cha siasa amekuwa na wakosoaji na mara nyengine hata wale walio karibu naye wanamuona kutokauwa muaminifu.

Johnson alikataa mahojiano wakati wa uchaguzi katika kipindi cha Neil- akiwa ndiye mgombea wa pekee kufanya hivyo katika uchaguzi wa hivi karibuni.

Pia alikataa kuhudhuria mjadala kuhusu hali ya hewa na badala yake akawakilishwa na donge la barafu lililokuwa likibubujika.

Boris Johnson akiwa Manchester

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mara nyngine Johnson amekwepa ukosoaji uliomlenga

Pia Nigel Farage, kiongozi wa chama cha Brexit hakumsaza katika ukosoji.

''Nimemjua Boris kwa zaidi ya miaka 25 ni mtu anayependwa , anapenda kufurahisha watu . lakini je unamuamini? Hapana''.

Mitandaoni

Pengine kitu ambacho kimemuharibia sifa Johnson katika siku za mwisho za kampeni yake ni chapisho la siku ya Jumatatu kuhusu picha ya mtoto mdogo mwenye miaka minne, aliyelazwa katika hospitali moja mjini Leeds akiwa amelala katika sakafu kwa kuwa hakukuwepo vitanda zaidi katika hospitali hiyo.

Picha hiyo iliosambaa mitandaoni na hususan katika mitandao ya kijamii, imekitia wasiwasi chama cha Uhafidhina, huku kikiomba msamaha kuhusu kile kilichomtokea mtoto huyo mbali na kujitetea dhidi ya madai kwamba kisa hicho kinatokana na ufadhili wa chini katika mfumo wa afya nchini humo.

Johnson alijibu katika mahojiano na ripota mmoja wa ITV.

Alikataa kutazama picha ya kijana huyo katika simu ya ripota huyo baada ya kuichukua simu hiyo na kuingiza katika mfuko wake akisema kwamba ataifuatilia baadaye.

Tabia yake ilionyesha wazi kwamba huenda waziri huyo mkuu hajajihami vya kutosha kukabiliana na ukosoaji dhidi yake huku akishindwa kuonyesha huruma.

Corbyn aliingilia akisema chama cha Wahafidhina kimekuwa uongozini kwa miaka tisa na sasa kinasema kwamba kinafadhili mfumo wa afya , ni uongo, hawajaanza hata kurekebisha mapungufu waliokuwa nayo katika kipindi cha miaka tisa iliopita.

Uaminifu na mafikira ya Corbyn

Kiongozi wa chama cha Leba hayuko huru kutokana na ukosoaji wake mwenyewe , hatahivyo .

Ujumbe wake unaokanganya kuhusu Brexit -akikataa kukifanya leba kuwa chama kinachojitangaza - kumekandamiza uaminifu wake.

Kutokana na hali ngumu ya chama hicho kinachojaribu kuwakilisha maeneo bunge yaliokipigia kura na kuwacha mengine ni maswala yaliopingwa, huku kiongozi huyo akijaribu kuwa katikati ya pande hizo mbili anaonekana kuwakasirisha wote kutoka pande zote mbili.

Akiwa kaskazini mwa Wales wiki hii , hakuzungumzia swala hilo akipendelea kuzungumia kuhusu ahadi zake za kuwekeza katika huduma ya afya badala yake.

Corbyn akiwa mjini Manchester

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Corbyn ni maarufu sana mashinani lakini hajakuwa aakishirikiana nao kuhusu Brexit

Uchaguzi wa Brexit

Vitabu vya historia vitaukumbuka uchaguzi huu kama uchaguzi wa Brexit.

Johnson mwenyewe aliyechukuwa uongozi wa taifa hilo mapema mwaka huu baada ya mtangaluzi wake Theresa May , alishindwa kupitisha muswada wa kujiondoa.

Kutokana na hilo chama cha Wahafidhina kinafanya kampeni ya kuhakikisha Brexit inatekelezwa - juhudi za kuvutia maeneo ya muda mrefu ya leba ambayo yalipigia kura kuondoka kwa Uingereza katika muungano wa Ulaya.

Zaidi ya hilo hatahivyo ni kwamba kampeni ya Johnson inalenga kupata uwakilishi mkubwa bungeni kwa mara ya kwanza tangu 2017.

Kila kitu anasema kinategemea hilo- Brexit , biashara mpya na Muungano wa Ulaya pamoja na Marekani , kupunguza kodi ,na kuongeza matumizi katika huduma ya kiafya pamoja na elimu.

Rais wa Marekani Donald Trump hana umaarufu mkubwa Uingereza.

Mgogoro wake na Meya wa London Sadiq Khan ulichochea jumbe za Twitter kuhusu siasa za Uingereza na jinsi Marekani ilivyomfanyia balozi wa Uingereza Marekani zimemfanya achukiwe na raia wengi wa Uingereza.

Vyama vingine vya kutazama

Kulikuwa na maoni kwamba harakati za vyama hivyo viwili vikubwa na viongozi wake vitatoa fursa kwa baadhi ya vyama vingine vidogo - kama vile liberal Democrats na chama cha Brexit party na vyama vya kitaifa vya SNP nchini Uskochi na kile cha Plaid Cymru huko wales kupata umaarufu.

Huku chama cha SNP kikipigiwa upatu kufanya vyema tena katika kinyang'anyiro hicho, vingine vinakumbwa na wakati mgumu licha ya kujaribu kuwashawishi wapiga kura katika maeneo ya uwakilishi mdogo.

Kiongozi wa SNP Nicola Sturgeon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongozi wa chama cha SNP Nicola Sturgeon amefanya kampeni Uskochi

Badala yake katika maeneo mengi ya taifa hilo, kutakuwa na ushindani mkali kati ya vyama hivyo viwili -Leba na conserevative mbali na viongozi wake wawili.

Johnson ambaye mara nyingi hachani nywele na asiyependelea kusoma hotuba zake amewashinikiza wafuasi wake kufuata mfumo wa kihafidhina akiunga mkono Brexit kwa hali na mali .

Ukimfananisha na Trump nchini Marekani hawafanani ,lakini ukimchunguza kwa ukaribu, Johnson kama mwenzake wa Marekani ni msumbufu ambaye amejionyesha kwamba yuko tayari kufutilia mbali tamaduni ili kuafikia malengo ya sera zake.

Kwa upande mwengine Corbyn ,ambaye amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama chake 2015, anawakilisha upande mwengine ulio tofauti na chama cha leba katika miongo ya hivi karibuni.

Iwapo utamfananisha na mwanasiasa yeyote nchini Marekani , basi umaarufu wake ni sawa na ule kama wa Bernier Sanders anayekidhibiti chama cha Democrats.

Leba ni chama tofauti sana kwa sasa ukilinganisha na mara ya mwisho kilipokuwa katika uongozi wakati wa miaka ya utawala wa Tony Blair na Gordon Brown katika miaka ya 2000.

Wapiga kura wengi wa Uingereza bila kujali vyama vyao , huenda wakatazama matukio ya muongo uliopita na kushangaa iwapo hii ni Uingereza tofauti.

Siku ya Alhamisi Uingereza itajulikana ni taifa la aina gani.