Uchaguzi wa Uingereza: Namna ya kupiga kura bila kitambulisho na je kuna njia zinazopelekea mtu kuwa maarufu duniani

Bunge la Uingereza na kijisanduku cha kupigia kura bungeni
    • Author, Peter Ball
    • Nafasi, BBC World Service

Bunge la Uingereza siyo tu moja ya mabunge ambayo yanafahamika kwa demokrasia pia mfumo wake ni wa kustaajabisha.

Mfumo wake wa kupiga kura umekuwa ukibadilika kwa miaka kadhaa kadiri maiaka inavyokwenda umekuwa na mambo mengi ya kustaajabisha ambayo yatajitokeza wakati wayu wanakwenda kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Alhamisi 12, Desemba.

Zifuatazo ni miongoni mwa mbinu za kustaajabisha kuhusu vile raia wa Uingereza wanavyopiga kura kumcagua waziri mkuu, ambaye atachukua uongozi wanchi hii ambayo uchumi wake ni watano kwa ukubwa duniani, inayotengeneza silaha za nyuklia na pia inashiriki katika Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.

Huna haja yakuthibitisha wewe ni nani kabla ya kupiga kura

Mtu akiweka kura yake katika sanduku la kupigia kura

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Huitaji aina yoyote ya kitambulisho kupiga kura nchini Uingereza

Siku ya kupiga kura, shughuli ya kupiga kura inafanyika kwa njia rahisi kabisa .Unachohitajika kufanya ni kujitokeza katika kituo cha kupiga kura, na kawaida huwa ni sehemu iliyokribu na nyumba yako, utampa afisa husika jina lako na anwani ya nyumba yako kisha utapewa karatasi ya kupiga kura.

Andika "x" ndani ya alama ya kisanduku karibu na mgombea unayetaka kumpigia kura, weka karatasi yako kwenye kijisanduku na utakuwa umemaliza kupiga kura.

Raia wa Iraqi akionesha kidole chake kilichotiwa wino baada ya kupiga kura

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika baadhi ya nchi watu kuwekwa alama ya wino vidoleni kuashiria kuwa tayari umeshapiga kura

Sababu kubwa ya kufanya hivi ni kwamba Uingereza hakuna mfumo wa kuwa na kitambulisho cha taifa na karibia watu milioni 3.5 hawana stakabadhi zengine kam vile leseni ya gari au paspoti

Lakini kumekuwa na mapendekezo ya kufanya iwe lazima kuonyesha fomu mfano wa kitambulisho ili kupiga kura ikiwemo kuanzisha kadi maalum ya kupiga kura, ambayo ni lazima kwa raia wa Uingereza wanaoishi Kaskazini mwa Ireland.

Wanaotaka kubadilishwa kwa mfumo wa sasa wamedai kwamba, mwaka 2017, ambako kisa kimoja cha uudanganyifu kilibainika kati ya kura milioni 44.4 zilizopigwa.

Hata hivyo kilichojitokeza wakati wa zoezi la upigaji kura ni kwamba, watu idadi kubwa haikuweza kupiga kura kwasababu ya ukosefu wa kitambulisho.

Aliyekufa anaweza kuamua nani wa kuibuka na ushindi

Kura iliyopigwa ikiweka katika sanduku la posta
Maelezo ya picha, Wakati ambao kura zilizopigwa kwa njia ya posta zitakuwa zinahesabiwa, huenda hata waliopiga wakawa wamekufa

Nchini Uingereza huna haja ya kupiga kura mwenyewe, unaweza kutuma maombi ya kupiga kura kwa njia ya posta ambapo fomu ya kupiga kura inatumwa nyumbani kwako na baaada ya kuijaza utairejesha kwa njia ya posta.

Unaweza kufanya hivi wiki kadhaa kabla ya uchaguzi, na kuzingitia kwamba idadi kubwa ya wazee kupendelea kupiga kura kwa njia hii, huenda ikawa wamekufa wakati kura zao zinahesabiwa.

Upigaji kura nchini Uingereza unaweza kuwa na ushindani mkubwa, katika uchaguzi uliopita mbunge mmoja alishinda kwa kura mbili pekee, na bila shaka kura zilizopigwa na watu ambao huenda wakafa muda mfupi baadaye, zinajukumu kubwa katika kuamua mshindi.

Na uchaguzi mkuu ambao unakaribia, huenda hilo likawa na nafasi kubwa katika kuamua yule atakayekuwa waziri mkuu.

Wabunge wengi Uingereza hawachaguliwi na wapiga kura

Bbunge la juu la Uingereza wakati kikao kinafungulia mara ya kwanza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bunge la juu la Uingereza linaofahamika kama ''House of Lords'', halijachuguliwi na wapiga kura

Kama nchi zengine nyingi, Uingereza lina mabunge mawili, Bunge la Wawakilishi likiwa na takriban wabunge 650 huku bunge la Malodi likiwa na wabunge 800.

Wabunge wote watachaguliwa katika uchaguzi huu ujao lakini raia wa kawaida hawaruhusiwi kuchagua wabunge wa Bunge la Malodi.

Mara nyingi kuwa uanachama wa Bunge la Malodi huwa ni wa kudumu na mara nyingi watu huingia katika bunge hilo kwasababu kuna watu wafimilia zao waliowahi kuwa wabunge ama kwa kuteuliwa.

Takriban asilimia 10 ya wabunge katika Bunge la Malodi, ni kutokana na watu wa familia waliokuwepo.

Wabunge hao ni pamoja na Malcolm Sinclair, ambaye ni wa 20 katika familia ya Earl of Caithness na kwasababu walipata kibali cha kukaa katika bunge hilo, yeye moja kwa moja alikuwa mrithi ikiwa ni zaidi ya miaka elfu moja iliyopita mwaka 1455.

Karibia kila mmoja ameteuliwa katika Bunge la Malodi milele kwasababu wamefanikiwa katika nyanja walizobobea ama wameteuliwa na chama cha kisiasa kuwawakilisha.

Wafanyakazi na bunge la Malodi kabla ya kikao rasmi cha ufunguzi wa bunge

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Bunge la Malodi wakiwa wamevalia majoho yao wakati wa kikao rasmi cha ufunguzi wa bunge

Hakuna sheria iliyoundwa kuhusiana na hili lakini kawaida ni kwamba chama kilichounda serikali kinateua idadi kubwa ya wabunge huku vyama vya upinzani ikiachiwa fursa ya kuchagua wabunge kidogo.

Hakuna sheria inayoangazia ni nani anayestahili kuwa Waziri Mkuu

Boris Johnson stood outside No 10 Downing Street

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, There aren't any qualifications to be the prime minister in the UK

Ikiwa unataka kuwa Rais wa Marekani,kulingana na kartiba ya nchi hiyo lazima uwe raia wa nchi hiyo kwa kuzaliwa, siyo chini ya miaka 35 na umekuwa mkaazi wa Marekani kwa angalau miaka 14.

Ili kuwa Waziri Mkuu wa Ungereza? Hakuna masharti yoyote ya lazima.

Kitu kilichopo ni mwongozo kutoka kwa Baraza la Mawaziri laUingereza ambao unasema waziri mkuu atakuwa kiongozi wa chama cha kisiasa chenye idadi kubwa ya wabunge katika bunge la Wawakilishi.

Lakini mwaka 1963, Sir Alec Douglas-Home alikuwa waziri mkuu alipokuwa mbunge wa Bunge la Malodi , akijivua ubunge na kuwa raia wa kawaida kwa wiki mbili hadi aliposhinda uchaguzi mdogo na kuwa mbunge katika Bunge la Wawakilishi

Pia ni muhimu fahamu kwamba mwongo katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri siyo nyaraka inayotambulika kihalali bali ni mwongozo uliandikwa na wafanyakazi waandamizi wa Uingereza katika sekta ya Umma.