Si Trump peke yake yuko hatarini katika uchaguzi ujao hata wapinzani wake pia wako mkondo mmoja

Chama cha upinzani Marekani,Democrats kimesema kuwa utawala wa Trump umefikia ukingoni

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Chama cha upinzani Marekani,Democrats kimesema kuwa utawala wa Trump umefikia ukingoni

Ukiachilia mbali maisha ya filamu kama za Netflix. Katika uhalisia , sio jambo la kawaida kumuona rais wa Marekani akiwa katika hatari ya kuondolewa madarakani na wapinzani wake.

Hivyo kama siasa ni suala ambalo unalifuatilia kwa karibu, utakuwa umesikia kuhusu vituko vingi vya kisiasa kuhusu madai ya kashfa dhidi ya rais Donald Trump kuanzia tarehe 3 mwezi Novemba.

Kaa mkao wa kula kusikiliza vimbwanga hivi

Kumekuwa na mfululizo wa simulizi nyingi kama tamthilia.

Lakini makala haya yanaweza kujibu baadhi ya maswali ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiulizwa na wasomaji wetu.

Unaweza kusoma pia kuhusu madai ya Trump:

Lakini madai haya ni yapi?

Kashfa ambayo inaweza kusababisha kumuondoa rais wa Marekani madarakani na wapinzani wake.

Baadhi ya watu wanadhani kuwa madai haya ndio yanaweza kumuondoa rais moja kwa moja madarakani lakini kiuhalisia huu ni mwanzo tu wa hatua nyingine mbili ambazo baraza la sheria linaweza kuangazia.

Bado haijajulikana kama uamuzi utatolewa na kamati maalum.

Chanzo cha picha, Empics

Maelezo ya picha, Bado haijajulikana kama uamuzi utatolewa na kamati maalum.

Uamuzi wa awali wa wawakilishi wa baraza hilo uliangalia ushahidi kama wataweza kutoa hukumu dhidi ya rais au hapana.

Ingawa kamati kuu ambayo inangoja uchunguzi huo ilisema kuwa kama rais atakuwa na hatia basi ataondolewa madarakani na nafasi yake itachukuliwa na makamu wa rais.

Marais wangapi waliwahi kukutana na kashfa za kuweza kuwaondoa madarakani?

Ni wawili tu: Andrew Johnson mwaka 1868 na Bill Clinton mwaka 1998.

Wote wawili walitakiwa kuondolewa madarakani lakini baadae seneti iliweza kuwaokoa wasalie madarakani.

Mwaka 1974, Rais Richard Nixon alipatikana akichunguza wapinzani wake kwa kashfa inayofahamika kama 'Watergate' - alijiuzulu kwa sababu alijua kuwa madai yale lazima yangemtoa madarakani na Ikulu au kuondolewa na wabunge wa seneti.

Vipi kuhusu Trump - Kwa nini anakabiliana na madai haya?

Donald Trump anashutumiwa kwa makosa ya kutumia vibaya nafasi yake ya uongozi kwa ajili ya manufaa yake binafsi ili aweze kuchaguliwa tena mwakani.

Volodymyr Zelensky na Donald Trump walikutana katika mkutano wa Umoja wa mataifa nchini Marekani, Septemba 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Volodymyr Zelensky na Donald Trump walikutana katika mkutano wa Umoja wa mataifa nchini Marekani, Septemba 2019

Trump anashutumiwa kwa kumshinikiza rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, kumchunguza Joe Biden, ambaye kwa sasa ndiye mgombea aliye mstari wa mbele kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais mwaka ujao, na mtoto wake wa kiume Hunter Biden, ambaye awali alifanyia kazi kampuni ya nishati ya Ukraine.

Je, Trump alivunja sheria?

Sio kila mtu anakubali kuwa inabidi uondolewe kwa sababu umemtaka kiongozi wa nchi nyingine kukufanyia vitu vibaya kwa mpinzani wako.

Trump anasema kuwa hakuna kosa alilolifanya mpaka ifikie hatua hiyo ya kumuondoa madarakani na kuona hafai tena kuongoza. Huku White House imesema kuwa haitashiriki katika maamuzi hayo.

Lakini madai ambayo yamechochea uamuzi huu ni kuhusu taarifa iliyotolewa kuwa Trump alimpigia simu ya siri Zelensky tarehe 25 Julai.

Trump alisitisha msaada wa mabilioni ya fedha pamoja na msaada kwa taifa la Ukraine na maafisa wanne waliweka wazi kuwa hatatoa fedha hizo mpaka Ukraine itakapoanza uchunguzi dhidi ya wapinzani wake, jambo ambalo ikulu ya Marekani inakanusha.

Spika wa bunge Nancy Pelosi alitaka uchunguzi ufanywe dhidi ya madai hayo

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Spika wa bunge Nancy Pelosi alitaka uchunguzi ufanywe dhidi ya madai hayo

Ni nini ambacho kinaweza kutokea?

Uchunguzi ulifanywa na baraza la sheria katika makundi madogo madogo yanayoitwa kamati.

Kila kundi lilikuwa linachunguza jambo lake kwa mfano masuala ya mambo ya nje ,matumizi ya fedha na sheria. Kamati hizi zitawasilisha mashahidi kutoa ushuhuda kwa Umma.

Wakili wa rais pia ataruhusiwa kuwa sehemu ya kamati hizo.

Maelezo ya video, Je inawezekana kumvua madaraka rais wa Marekani?

Kama kamati zitaamua kuwa rais inabidi ahukumiwe basi wawakilishi wote wa rais wanapaswa kupiga kura.

Je kuna namna yoyote ambayo rais atapatwa na hatia?

Ni viongozi wachache wa Marekani ndio walifikia katika hatua ya namna hii. Kwa kuwa chama cha upinzani cha Democratic kuwa na wengi bungeni, kuna uwezekano kuwa Trump ataondolewa.

Democrats wanataka kura hiyo ipigwe kabla ya mwisho wa mwaka.

Andrew Johnson, Richard Nixon na Bill Clinton

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Andrew Johnson (kushoto) na Bill Clinton (kulia) walikutwa haatiani lakini walikombolewa na bunge la Senate, huku Nixon alijiuzulu mwenyewe

Sasa uwezekano wa Trump kuondolewa madarakani upo?

Hajaanza kufungasha mizigo yake. Chama chake cha Republican kina viti 53 kati ya viti 100 vya wanachama wa Seneti na kura zinahitajika kufika robo tatu ili kiongozi huyo aweze kuondolewa kabisa katika madaraka yake.

Hivyo kama idadi ya watu 20 kutoka chama chake wakimpinga. Lakini kama sivyo Trump ataendelea kubaki kwenye nafasi yake, Na wanachama wa Republican bado wanamuunga mkono.

Sasa kuna umuhimu gani wa kesi hii kuendelea kuvuma au ndio mikogo ya kisiasa tu?

Wanaomuunga mkono Trump wanaamini kuwa upinzani unajaribu kushusha nguvu ya rais katika uchaguzi wa urais. Mlolongo huu ambao Trump anapitia umeweza kuharibu nafasi yake kama rais.

Matokeo ya uchaguzi huu yameingiza dosari kwa Trump kwa uchaguzi wa rais wa mwaka 2020

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Matokeo ya uchaguzi huu yameingiza dosari kwa Trump kwa uchaguzi wa rais wa mwaka 2020

Bilionea huyu aliyeamua kuwa mwanasiasa amekuwa na maamuzi yenye utata , ikiwemo la kuingilia uchunguzi wa madai ya Urusi kuingilia uchaguzi mwaka 2016, kukataa kutoa nakala za malipo ambayo alidaiwa kuwalipa wanawake wawili ambao walidai kuwa na mahusiano naye.

Uhusiano wake na Ukraine.

Lakini ikumbukwe kuwa madai yanayomkabili Trump yanawaweka hatarini wapinzani pia katika uchaguzi wa mwaka 2020.