Wachezaji 10 bora wa kombe la Dunia

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zidane alifunga mabao mawili katika fainali ya Kombe la Dunia 1998 wakati Ufaransa ilipoilaza Brazil 3-0

Kombe la Dunia limekuwa likionyesha wanasoka bora zaidi duniani kwenye hatua kubwa zaidi kwa kipindi bora zaidi cha karne.

Lakini ni nani mchezaji bora zaidi katika historia ya Kombe la Dunia?

Gary Lineker, Alan Shearer na Micah Richards walijadili mada hiyo kwa kina .

Gary Lineker (Richards: wa 10, Shearer: wa 9)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lineker akishangilia kwa kufunga penalti dhidi ya CameroonLineker alifunga mabao 10 katika mechi 12 za Kombe la Dunia akiwa na England

Mfungaji bora wa muda wote wa England katika Kombe la Dunia, Lineker alizifumania nyavu mara 10 katika mechi 12 katika mashindano ya 1986 na 1990. Lineker alifunga mabao sita na kushinda Kiatu cha Dhahabu mwaka 1986 na akafunga mengine manne mwaka 1990 na kusaidia vijana wa Bobby Robson kutinga nusu fainali, na kupoteza kwa mikwaju dhidi ya Ujerumani Magharibi.

Richards: Mabao kumi katika mechi 12 ni mazuri.

Shearer: Alicheza mechi 12 za Kombe la Dunia na kufunga mabao 10. Alishinda Kiatu cha Dhahabu na kutinga robo fainali na nusu fainali.

Lineker: Sijui ninachofanya kwenye orodha hii...

Johan Cruyff (Richards: wa 6, Shearer: wa 10)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cruyff akicheza dhidi ya Argentina kwenye Kombe la Dunia la 1974Cruyff aliisaidia Uholanzi kuzishinda Argentina na Brazil katika Kombe la Dunia 1974 kabla ya kushindwa na Ujerumani Magharibi katika fainali.

Cruyff aliisaidia Uholanzi kuzishinda Argentina na Brazil katika Kombe la Dunia 1974 kabla ya kushindwa na Ujerumani Magharibi katika fainali.

Bila shaka alikuwa mchezaji bora zaidi ambaye hakuwahi kushinda Kombe la Dunia, mshindi huyo mara tatu wa Ballon d'Or alifunga mabao matatu na kuisaidia Uholanzi kufika fainali ya 1974, kabla ya kushindwa na Ujerumani Magharibi. Cruyff alistaafu mwaka 1977, mwaka mmoja kabla ya Waholanzi kushindwa katika fainali na wenyeji Argentina mwaka 1978.

Richards: Alikuwa mtu maalum.

Shearer: Alicheza Kombe moja la Dunia pekee na hii inatokana na uchezaji wao wa Kombe la Dunia. Kwa vyovyote vile sisemi Lineker ni mchezaji bora kuliko Cruyff, ni rekodi yake ya Kombe la Dunia ndio inamweka nafasi ya tisa.

Bobby Moore (Richards: 9, Shearer: 6th)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Moore akishangilia na kombe na wachezaji wenzake wa timu ya UingerezaMoore aliinuliwa juu na wachezaji wenzake wa timu ya Uingereza baada ya fainali ya Kombe la Dunia ya 1966

Moore akiwa nahodha katika historia ya Kombe la Dunia la Uingereza, aliwahi kuwa nahodha wa Three Lions katika michuano hiyo ya mwaka 1966 katika ardhi ya nyumbani. Baada ya kifo chake mnamo 1993, Pele alisema gwiji huyo wa West Ham ndiye beki mgumu zaidi kuwahi kukumbana naye wakati wa uchezaji wake.

Richards: Unaona video na kusikia jinsi wachezaji hawa walivyokuwa bora.

Shearer: Alikuwa nahodha wa England akiwa na umri wa miaka 22. Nimeona picha zake, lakini kufanywa nahodha baada ya mechi yake ya 12 akiwa na umri wa miaka 22, inaonyesha jinsi alivyokuwa mzuri Pia alishinda Kombe la Dunia, ajabu.

Gerd Muller (Richards: wa 7, Shearer: wa 7

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gerd Muller akinyanyua kombe la duniaMuller alifunga bao la ushindi katika fainali ya 1974

Mmoja wa wafungaji bora zaidi kuwahi kutokea kwenye Kombe la Dunia, Muller alifunga mara 10 na kuisaidia Ujerumani Magharibi kumaliza katika nafasi ya tatu mwaka 1970 na kufunga mabao manne katika kampeni ya ushindi wa 1974, ikiwa ni pamoja na mshindi katika fainali. Muller alifunga mabao 14 katika mechi 13 za Kombe la Dunia.

Shearer: Mabao kumi na manne katika mechi 13 za Kombe la Dunia, 10 katika Kombe moja la Dunia. Lo!

Lineker: Alikuwa kama [Sergio] Aguero, mchezaji wa eneo la penalti, mwepesi wa ajabu na jangili halisi. Bao lililoshinda Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi ya Cruyff - lilimdhihirisha Muller. Jinsi alivyokuwa akicheza na kugeuka, alikuwa mchezaji wa ajabu. Nambari zake ziko hapo juu. Mashujaa wangu walikuwa Frank Worthington, Peter Shilton na Muller alikuwa shujaa wangu wa kimataifa.

Franz Beckenbauer (Richards: wa 8, Shearer: wa 5)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Beckenbauer alinyanyua taji la Kombe la Dunia mnamo 1974Beckenbauer aliwahi kuwa nahodha wa Ujerumani Magharibi na kutwaa tuzo kubwa zaidi ya soka mwaka 1974 kabla ya kushinda kama meneja mwaka 1990.

Beckenbauer alinyanyua taji la Kombe la Dunia mnamo 1974

Beckenbauer aliwahi kuwa nahodha wa Ujerumani Magharibi na kutwaa tuzo kubwa zaidi ya soka mwaka 1974 kabla ya kushinda kama meneja mwaka 1990.

Akiwa nahodha, 'Der Kaiser' aliwahi kuwa nahodha wa Ujerumani Magharibi hadi kutwaa taji la Kombe la Dunia katika ardhi ya nyumbani mwaka 1974, na kuwashinda Uholanzi katika fainali. Beckenbauer pia ni mmoja wa wanaume watatu (pamoja na Mbrazil Mario Zagallo na Didier Deschamps wa Ufaransa) walioshinda Kombe la Dunia kama mchezaji na meneja.

Lineker: Alikuwa beki wa kati mara kwa mara alitoka nje ya ulinzi akiwa na mpira.

Zinedine Zidane (Richards: wa 5, Shearer: wa 8)

Maisha ya Zizou katika Kombe la Dunia yalianza vyema, akifunga mara mbili kwenye fainali na kuisaidia Ufaransa kushinda katika ardhi ya nyumbani. Jeraha lilimfanya acheze mara mechi moja huku timu yake ikiwa na na safu mbaya zaidi ya mwaka 2002, lakini akarejea katika kiwango bora nchini Ujerumani miaka minne baadaye, na kukiwezesha kikosi cha Raymond Domenech kutinga fainali, ambapo Zidane alifunga na kukumbukwa kwa kadi nyekundu kwa kumpiga kichwa Marco Materazzi wa Italia kifuani huku Ufaransa ikipoteza kwa mikwaju ya penalti.

Richards: Kitaalam, alikuwa mmoja wa wachezaji bora milele.

Shearer: Mchezaji bora niliyewahi kucheza dhidi yake alikuwa mchezaji wa ajabu.

Lothar Matthaus (Richards: wa 4, Shearer wa 4)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matthaus asherehekea kufunga bao katika robo fainali ya Kombe la Dunia 1986Matthaus ni mmoja kati ya wachezaji watatu pekee waliowahi kucheza Kombe la Dunia mara tano pamoja na Antonio Carbajal wa Mexico na Rafael Marquez.

Mchezaji wa Ujerumani aliyecheza mara nyingi zaidi wakati wote, Matthaus aliongoza Ujerumani Magharibi kwa mafanikio Italia '90, akiwashinda Argentina inayoongozwa na Maradona katika fainali. Matthaus ni mmoja wa wachezaji watatu pekee waliocheza katika michuano mitano ya Kombe la Dunia na anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi akiwa na 25.

Richards: Kushiriki makombe matano ya Dunia ni jambo la kushangaza, na alishinda moja.

Shearer: Alicheza katika makombe matano ya Dunia na kucheza mechi 25. Nilicheza dhidi yake kwenye Euro 2000 na ulikuwa mchezo wake wa mwisho tulipowafunga 1-0.

Ronaldo (Richards: wa 3, Shearer: wa 2)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ronaldo asherehekea ushindi wa Brazil wa 2002Ronaldo ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia akiwa na mabao 15 hadi Miroslav Klose wa Ujerumani alipozipita alama zake mwaka 2014.

Akiwa mchezaji mwingine wa Brazil, Ronaldo alinyanyua taji hilo maarufu mara mbili: mwaka 1994 na 2002. Ingawa hakushiriki katika ushindi wa Brazil 1994, alifunga mara nne na kuisaidia kufika fainali ya 1998, ambapo aliachwa nje ya kikosi cha kwanza kabla ya kurejeshwa na kuanza. Ufaransa ilishinda mwaka huo lakini Ronaldo aliacha alama yake miaka minne baadaye, akifunga mara nane - ikiwa ni pamoja na mawili katika fainali dhidi ya Ujerumani - huku Brazil ikitwaa tena hadhi yao ya kuwa mabingwa wa dunia.

Shearer: Alishangaza wengi, tumezungumza kuhusu Ronaldo mara nyingi sana. Ubrazili. Sababu nyingine iliyonifanya awe wa pili ni mechi 19, mabao 15 na asisti tano.

Diego Maradona (Richards: wa 2, Shearer: wa 3)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maradona akiwa na kombe la duniaMaradona alikuwa nahodha wa Argentina katika Kombe lao la pili la Dunia huko Mexico '86

Maradona hakuweza kuzuilika nchini Mexico mwaka huo, akifunga mabao matano, yakiwemo mawili dhidi ya Uingereza katika robo fainali: 'Goli la mkono wa Mungu ‘na juhudi bora zaidi za mchezaji binafsi ambazo zinaorodheshwa kati ya mashambulio makubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye mashindano.

Akiwa amepoteza fainali ya 1990 dhidi ya Ujerumani Magharibi, Maradona alicheza fainali ya Kombe la Dunia kwa fedheha mwaka 1994 aliporudishwa nyumbani kwa kushindwa vipimo vya dawa za kulevya.

Lineker: Kabla ya Messi kuja siku zote kulikuwa na mjadala ule kati ya Brazil na Argentina, nani alikuwa bora - Pele au Maradona?

Pele (Richards: 1, Shearer: 1st)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pele anasherehekea ushindi wa Brazil wa 1970Pele alifunga mabao manne katika ushindi wa Brazil wa Kombe la Dunia 1970, likiwemo la kwanza katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Italia kwenye fainali.

Akionekana na wengi kama mchezaji bora wa Kombe la Dunia, Pele alikuwa na umri wa miaka 17 pekee alipoisaidia Brazil kushinda mashindano ya 1958 nchini Uswidi. Mshambulizi huyo mashuhuri aliendelea na kushinda Kombe la Dunia la 1962 na 1970 pia, akishinda Mpira wa Dhahabu kwa mchezaji bora wakati huo. Pele alifunga mabao 12 katika mechi 14 za Kombe la Dunia katika michuano minne ya Brazil.

Richards: Pele lazima awe mshindi.

Shearer: Huwezi kufikiria aliichezea Brazil katika umri huo, chini ya shinikizo hilo. Walitarajiwa kushinda, kila mechi watakayocheza, aliwa na nyota ya juu kila mahali. Mchezaji wa kushangaza.