Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Gyokeres yuko tayari kujiunga na Man Utd

Chanzo cha picha, BBC Sport
Mshambuliaji wa Sporting na timu ya taifa ya Uswidi Viktor Gyokeres, 27, yuko tayari kuungana tena na kocha wake wa zamani Ruben Amorim katika klabu ya Manchester United. (Sportsport)
Arsenal imewaongeza winga wa Aston Villa Muingereza Morgan Rogers, 22, na mshambuliaji wa Brazil Igor Paixao, 24, anayechezea Feyenoord, kwenye orodha ya wachezaji wanaopania kuwasajili msimu huu. (Times- usajili unahitajika)
Brentford imekataa dau la kwanza lililowasilishwa na Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo. Tetesi zinasema Klabu hiyo ya Old Trafford ilitoa pauni milioni 45 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 10 lakini The Bees wanataka zaidi ya pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Independent)
Klabu ya Tottenham italazimika kumlipa kocha mkuu Ange Postecoglou fidia ya pauni milioni 4 iwapo wataamua kumfukuza raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 59. (Telegraph - usajili unahitajika)
Winga wa Israel Manor Solomon, 25, anatarajiwa kupata nafasi nyingine Spurs baada ya kufanya vyema kwa mkopo Leeds msimu uliopita. (Sun)
Chelsea ina nia ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 20 Muingereza Jamie Gittens msimu huu wa kiangazi. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Bayer Leverkusen Erik ten Hag anafuatilia hali inayomzunguka winga wa Manchester United Antony, 25, ambaye alimleta Old Trafford baada ya kuwa na Mchezaji huyo wa Brazil huko Ajax. (Sky Germany)
Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imewasilisha ofa ya dau la £55m pamoja na £4m kama nyongeza kwa klabu ya Napoli ili kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen. (Fabrizio Romano)
Manchester City inakaribia kufikia makubaliano na klabu ya Wolves kumsaini beki wa wa Algeria Rayan Ait-Nouri, 23. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha ametatizika katika kikosi cha kwanza cha Bayern Munich ingawa anataka kusalia katika klabu hiyo ya Ujerumani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 huenda akaondoka ikiwa hali yake haitakuwa sawa. (Sky Sports Ujerumani)
Arsenal ina nia ya kumsajili winga wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 24 Rodrygo. (Sky Sports)
Beki wa Inter Milan na Italia Francesco Acerbi, 37, huenda akaungana na kocha wa zamani wa Inter Milan Simone Inzaghi katika klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal. (Florian Plettenberg)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












