Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Man City kumnunua beki wa Crystal Palace Marc Guehi

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanavutiwa na beki wa Crystal Palace na Uingereza Marc Guehi, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akionekana kama mchezaji ambaye anaweza kuwa sehemu ya marekebisho ya safu ya nyuma ya timu hiyo. (Football Insider),
Atletico Madrid wanaweza kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester United Mwingereza Marcus Rashford, 27, ambaye hachezeshwi katika kikosi cha kwanza Old Trafford. (TBR Football)
Vilabu nchini Saudi Arabia pia vinavutiwa na Rashford na vinaamini kuwa yeye ndiye mchezaji sahihi wa kuongeza hadhi ya ligi hiyo duniani. (Telegraph)
Arsenal wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 26, mwezi Januari. (Caught Offside)
Crystal Palace, Leicester na Wolves wote wana nia ya kumsajili fowadi wa Newcastle na Paraguay Miguel Almiron, 30, kwa mkopo mwezi Januari. {Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, ambaye amekuwa akiwachwa nje ya kikosi cha kwanza na Amex, baada ya bao moja pekee msimu huu. (GiveMeSport kupitia Caught Offside), nje
Fulham pia wanavutiwa na Ferguson na wanataka kumsajili kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Independence)
Liverpool wamempa beki wa kulia wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, ofa ya kandarasi iliyoboreshwa, lakini Real Madrid watazidisha juhudi zao za kumsaini kwa mkataba wa bila malipo msimu ujao wa joto na kukutana naye Januari. (Caught Offside), nje
Liverpool hawana uwezekano wa kumnunua mlinzi wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 24, ikiwa Alexander-Arnold ataondoka kwa sababu meneja Arne Slot angependelea beki wa kulia wa jadi, ambaye ni bora katika safu ya nyuma, na haamini hiyo inamfaa Frimpong. (Florian Plettenberg/Sky Germany)
Beki wa kushoto wa Scotland Kieran Tierney, 27, ataondoka Arsenal msimu wa joto baada ya klabu hiyo kuchagua kutomuongezea mkataba{ Athletic, external}

Chanzo cha picha, Getty Images
Marseille wanafikiria kumnunua Mfaransa Paul Pogba, 31, ambaye anatafuta klabu mpya baada ya marufuku yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli kupunguzwa. (Goal)
Manchester United inamtaka beki wa kushoto wa Ureno mwenye umri wa miaka 22 Nuno Mendes, ambaye mkataba wake wa sasa na Paris St-Germain unataka kurefushwa zaidi ya 2026. (Florian Plettenberg/Sky Germany).
Mlinzi wa Inter Milan na Italia Federico Dimarco, 27, atakataa mbinu yoyote kutoka kwa Manchester United ili kusalia na mabingwa hao wa Serie A. (Tuttosport via Goal)
Vilabu vya Premier League vinafikiria kumnunua fowadi wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, huku Paris St-Germain wakimpa nafasi ya kuhama. (Times),
Tottenham wana uwezekano wa kumnunua beki wa Paris St-Germain na Slovakia Milan Skriniar, 29, mwezi Januari. (Gazzetta - In Italy)

Chanzo cha picha, BBSport
Liverpool, Manchester City na Tottenham wanavutiwa na winga wa Real Valladolid na Uhispania Raul Moro, 22, ambaye anaweza kupatikana kwa kati ya euro 4-10m. (Sport - In Spanish)
Leeds watavutiwa na mlinda lango wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher iwapo watapandishwa daraja hadi Ligi ya Premia, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anaweza kutafuta timu nyengine. (TeamTalks),
Mshambulizi wa Leeds Patrick Bamford, 31, anavutia klabu ya Serie A Genoa na timu ya League One Wrexham, lakini Mwingereza huyo hana uwezekano wa kuondoka Januari huku meneja Daniel Farke akitaka washambuliaji wapandishwe daraja. (Teamtalks)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












