Saudia Arabia imejipanga vipi kuandaa Kombe la dunia 2034?

Uwanja wa Kimataifa wa King Salman uliopendekezwa mjini Riyadh unatarajiwa kuandaa mechi ya ufunguzi na fainali ya Kombe la Dunia la 2034.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uwanja wa Kimataifa wa King Salman uliopendekezwa mjini Riyadh unatarajiwa kuandaa mechi ya ufunguzi na fainali ya Kombe la Dunia la 2034.
    • Author, David Watkinson
    • Nafasi, Mwandishi wa BBC Sport
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Kombe la dunia la soka la wanaume litafanyika nchini Saudi Arabia likiahidi viwanja vya ''kipekee'' na waandalizi kusisitiza kila mmoja anakaribishwa.

Hata hivyo, uamuzi wa kombe la dunia kufanyika Saudia, utakaohusisha viwanja 11 ambavyo bado havijajengwa - kimoja katika mji mpya ambao hujajengwa - ni jambo lenye utata.

Ombi la Saudi Arabia lilipokelewa bila upinzani, na Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) lililiunga mkono kuwa Saudia awe mwenyeji wa Kombe la Dunia la 2034 katika mkutano wa FIFA wa Jumatano.

Hii ni mara ya pili mashindano haya kufanyika Mashariki ya Kati baada ya Kombe la Dunia la Qatar la 2022.

Saudi Arabia imewekeza takriban pauni bilioni tano katika michezo tangu mwaka 2021,ambapo Mwana Mfalme Mohammed bin Salma alipoifanya kuwa sehemu muhimu ya mikakati yake ya kuimarisha uchumi, kwa kuleta mashindano makubwa ya michezo nchini humo, ikiwa ni pamoja na masumbwi maarufu na Formula 1.

Ligi ya soka ya ndani ya nchi hiyo sasa inajumuisha nyota wa dunia kama vile Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Neymar Jr., na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia unamiliki Newcastle United na kuzindua mfululizo wa mashindano ya gofu ya LIV.

Hata hivyo, nchi hiyo imekosolewa kwa kutumia soka ili kuboresha sifa za ufalme wa mafuta juu ya rekodi yake ya haki za binadamu na athari za kimazingira.

Je, Kombe la Dunia nchini Saudi Arabia litakuwa vipi?

Uwanja wa Aramco,Al Khobar

Chanzo cha picha, SAUDI 2034

Maelezo ya picha, Uwanja wa Aramco,Al Khobar

Mnara,mfumo wa kukaa wa muonekano wa wimbi la bahari -viwanja 11

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ripoti ya FIFA kuhusu ombi la Kombe la Dunia la Saudi Arabia inashabikia miradi ya viwanja vya "kipekee" vilivyopendekezwa.

"Vina uwezo mkubwa na bila shaka vitabadilisha namna miundo ya viwanja itakavyoundwa na jinsi ya kuzingatiwa kwa muundo wa viwanja vya baadaye," inasema ripoti hiyo.

Kwa jumla, waandalizi wanasema Kombe la Dunia la Saudi Arabia litachezwa katika viwanja 15 katika miji mitano: Riyadh, Jeddah, Abha, Al-Khobar na Neom, mji mpya ambao bado haujajengwa kaskazini-magharibi mwa nchi.

Mipango ya ujenzi wa uwanja wa Neom inaonyesha kuwa utakuwa mrefu na mita 350 kutoka ardhini na utafikia uwanja huo kwa haraka kupitia kambarau za kasi na magari yasiyo na madereva.

Hii ni sehemu ya mradi wa "The Line" wa nchi hiyo, ambao umependekezwa kama mji usio na magari, upana wa mita 200 (656ft) tu na urefu wa kilomita 170 (maili 106 ). "The Line" utakuwa mrefu zaidi kuliko Jumba la Empire State la New York na kama urefu wa umbali kati ya Bristol na London.

Uwanja wa Qiddiya Coast utakuwa na muundo wa mawimbi ya maji ili kuonyesha muonekano wa wimbi la Mexico, huku Uwanja wa Prince Mohammed bin Salman huko Riyadh ukiwa juu ya kilele cha milima.

Viwanja nane katika ya 11 vya mashindano vitakuwa katika mji mkuu Riyadh - ikiwa ni pamoja na uwanja wa Kimataifa wa King Salman wa 92,760, ambao utakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi na fainali.

Kati ya viwanja 15, vinne vimeshajengwa, nane vimepangwa na vitatu viko chini ya ujenzi na vitakuwa mwenyeji wa Kombe la Asia la AFC mwaka 2027.

Mwenyeji wa kombe la dunia 2034 ana utata?

Saudi Arabia wamekosolewa kwa ukiukaji wa haki za binadamu,dhuluma dhidi ya wanawake, uhalifu wa ushoga, ukandamizaji wa uhuru wa kusema na vita huko Yemen.

Mashirika yasiyo ya kiserikali hivi karibuni yalidai kuwa mamlaka zilitia saini kwa kuuawa kwa watu wasiopungua 200 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2024, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kwa miongo mitatu.

Hadhi ya kimataifa ya ufalme huo ilidhurika sana na mauaji ya Jamal Khashoggi mwaka 2018, mwandishi wa habari wa Saudi aliyekuwa akifanya kazi Marekani na ambaye alikuwa mkosoaji maarufu wa serikali.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa serikali ya Saudi Arabia inajificha nyuma ya kuandaa kombe la duni ilhali ni visa vigi vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Hata hivyo,Serikali ya Saudi Arabia inasema kuwa uwekezaji katika michezo unachangia kuinua uchumi, kuvutia utalii na kuwahamasisha watu kuwa na shughuli za kimwili zaidi.

Kwa mujibu wa miongozo ya FIFA, nchi zinazowania kuwa wenyeji wa dimba hili lazima zijitolee kuheshimu haki za binadamu.

Mnamo Novemba, FIFA ilitoa ripoti yake ya tathmini kwa ombi la Saudi Arabia, ikipatia alama "ya wastani ya 4.2 kutoka 5" - ambayo ni alama ya juu zaidi kuwahi kutolewa.

FIFA ilidai kuwa "kuna uwezekano mzuri kwamba mashindano haya yanaweza kuwa kichocheo cha baadhi ya mabadiliko na mageuzi yanayoendelea na ya baadaye, na kuchangia matokeo mazuri ya haki za binadamu kwa watu wa Saudi Arabia na eneo hilo, ambayo yatakuwa na manufaa zaidi ya ile ya mashindano yenyewe".

Mwezi uliopita, hata hivyo, kundi la kampeni la Amnesty International lilisema kuwa mchakato wa kuchagua Saudi Arabia kama mwenyeji wa Kombe la Dunia la 2034 lazima uahirishwe hadi mageuzi makubwa ya haki za binadamu yatangazwe. Lilidai kuwa kufanyika kwa mashindano huko kunaweza kusababisha ukiukaji mkubwa na mpana wa haki za kibinadamu.

'Kila mmoja anakaribishwa'

Pombe imeharamishwa Saudi Arabia na huenda hilo halitabadilika kabla ya kombe la dunia.

Adhabu ya kunywa pombe ni pamoja na faini, vifungo vya gerezani na kufukuzwa nchini.

"Tumeshapokea zaidi ya matukio mia moja ya michezo, tukikaribisha mashabiki milioni tatu wa michezo bila pombe," Hammad Albalawi kutoka Wizara ya Michezo ya Saudi Arabia aliiambia Sky mapema mwaka huu. "Wamefurahi kwa wakati wao na kugundua kile Saudi Arabia inachotoa - burudani, sanaa, muziki, tamaduni na urithi."

Uhusiano wa jinsi moja pia ni haramu nchini Saudi Arabia na ukiwa Huntha hautambuliwi kwa jinsia yako.

Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza inawashauri wasafiri kwenda nchini Saudi Arabia kuheshimu mila za wenyeji, desturi, sheria na dini "ili msije mkafanya makosa". Inasema kuwa wasafiri wanaweza kukutana na "adhabu kali kwa kufanya jambo ambalo haliwezi kuwa kinyume cha sheria nchini Uingereza" na wanapaswa kuepuka kuonyesha mapenzi hadharani.

Kutokubeba vitambulisho vya kibinafsi kunaweza kusababisha faini au kifungo cha gerezani.

Akizungumza na mhariri wa michezo wa BBC Dan Roan mwaka jana, waziri wa michezo wa Saudi Arabia Prince Abdulaziz bin Turki Al Faisal alisema kwamba utata kuhusu matibabu ya wafanyakazi wahamiaji nchini Qatar kabla ya Kombe la Dunia la 2022 "hautarudiwa".

Alisisitiza pia kwamba "kila mtu atakaribishwa" katika kombe la dunia 2034.

Miji itakayoandaa dimba hilo iko umbali wa mamia ya maili
Maelezo ya picha, Miji itakayoandaa dimba hilo iko umbali wa mamia ya maili

Kufurahia kwa mashabiki

Ombi linahusisha mipango ya kupanua viwanja vya ndege, kuanzisha huduma za reli za kasi na kuboresha usafiri wa umma.

Hata hivyo, umbali mrefu kati ya viwanja unamaanisha kuwa mashabiki wanaotaka kusafiri kati ya miji zitakazoandaa mechi hizo huenda wakahitaji kutegemea usafiri wa ndege.

Saudi Arabia ni nchi kubwa zaidi Mashariki ya Kati na karibu mara tisa kubwa kuliko Uingereza.

Kombe la Dunia linapanuliwa na litajumuisha timu 48 kuanzia mwaka 2026. Hii ni ongezeko kutoka timu 32 zilizoshiriki Qatar.

FIFA ilisema "kuboresha miundombinu ya usafiri wa umma kunatarajiwa" katika miji, ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa mfumo mpya wa metro huko Riyadh.

Bustani kumi za mashabiki, mbili kila jiji, zinapangwa.

Kuhusu malazi kwa timu, maafisa, vyombo vya habari na mashabiki, ripoti ya ombi la FIFA inasema kuna "mchango mpana wa makazi mazuri yatakayotosheleza wadau wa mashindano watakaohudhuria".

Je, inaweza kuwa mashindano wakati wa msimu wa baridi?

Mashindano ya 2034 yanaweza kufanyika katika msimu wa baridi ili kuepuka mechi zichezwe wakati kuna msimu wa joto kama vile ilifanyika katika kombe la dunia la 2022 nchini Qatar.

Akizungumza na BBC,waziri wa michezo mwana mfalme Abdulaziz amesema kuwa waandalizi wanapima iwapo kombe hilo litafanyika msimu wa joto.

''Kwanini tusiangalie uwezekano wakuandaa mechi majira ya joto?iwapo itakuwa msimu wa baridi au joto hilo halitutatizi ,tutahakikisha tutawapa wachezaji na mashabiki mazingira mazuri ambayo watayafurahia,''anasema waziri wa michezo.

Nyuzi za joto nchini Saudia huwa ziko katika viwango vya wastani kuanzia mwezi Oktoba hadi Aprili.

Wakati wa miezi kama hii,nyuzi za joto za kila siku katika miji ambayo itaandaa dimba hilo ni kuanzia nyuzi za 15 seliasi hadi 30 seliasi.

Kuanzia mwezi Mei na Septemba,nyuzi za joto ni kuanzia seliasi 27 na seliasi 43 katika mikoa ya bara,na seliasi 27 hadi seliasi 38 katika maeneo ya pwani.

Mada zinazofanana:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid