Je kombe la Dunia katika mataifa sita litakuwaje?

dfcx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mechi tatu za ufunguzi zimependekezwa kuchezwa Amerika ya Kusini kwa ajili ya kumbukumbua ya miaka mia ya kombe la dunia

Mpango uliopendekezwa wa mashindano ya kombe la duni ya 2030 - yatakayofanyika Amerika Kusini, Afrika na Ulaya - ni mgumu unapoufikiria.

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kuchezwa katika bara zaidi ya moja. 2002 lilikuwa tukio la awali kombe la dunia kuwa na wenyeji zaidi ya mmoja, Korea Kusini na Japan.

Hayo yatabadilika wakati Marekani, Mexico na Canada watakapoandaa 2026 - lakini haitalingana na Kombe la Dunia la 2030.

Uhispania, Ureno na Morocco zimetajwa kuwa wenyeji, lakini mechi tatu za ufunguzi zitafanyika Uruguay, Argentina na Paraguay kuadhimisha miaka 100 ya Kombe la Dunia.

Mambo mapya

Mji mkuu wa Uruguay ndio utakaoandaa mechi ya ufunguzi mwaka 2030, na mechi nchini Argentina na Paraguay zitafuata kabla ya michuano iliyosalia ya timu 48 kufanyika Afrika kaskazini na Ulaya.

Mara tu mechi hizo za mapema zitakapokamilika, michuano itagawanywa kati ya mataifa matatu - kama ilivyopangwa kwa Kombe la Dunia la 2026.

Kombe la Dunia litapanuliwa kwa ajili ya timu 48 na kwa mara ya kwanza litachezwa katika miji 16 mwenyeji nchini Marekani, Mexico na Canada.

Pamoja na uamuzi wa Fifa wa kuhifadhi muundo wa makundi ya timu nne, itamaanisha idadi ya mechi kuongezeka kutoka 80 hadi 104, sambamba na kuanzishwa kwa hatua mpya ya 32 bora.

Misimu miwili?

Mabadiliko ya hali ya hewa katika vizio vya dunia yanamaanisha kuwa baadhi ya timu zinaweza kujikuta zinacheza katika misimu miwili tofauti kwenye Kombe la Dunia moja.

Wale ambao watashiriki katika mechi tatu za ufunguzi huko Amerika Kusini kabla ya kuanza tena mechi zao barani Ulaya au Afrika Kaskazini watatoka katika msimu wa baridi hadi msimu wa joto.

Juni, Uruguay hupata baridi ya wastani ya kati ya 8C na 15C, na wakati huo huo halijoto nchini Morocco inaweza kuwa zaidi ya 30C. Nchi ya Argentina ina hali ya hewa sawa na Uruguay. Paraguay ina wastani wa zaidi ya nyuzijoto 23C.

Lakini hali hiyo bado ni baridi ukilinganisha na joto la kiangazi linalotarajiwa katika sehemu za Uhispania na Ureno ambazo, kama Morocco, zina wastani wa takriban nyuzijoto 35C wakati wa Julai.

Vipi kuhusu usafiri?

DSXC
Maelezo ya picha, Kizio cha Kusini cha dunia kwenye mataifa ya Argentina, Paraguay na Uruguay ni msimu wa baridi katika miezi ya Juni na Julai wakati ni msimu wa kiangazi Morocco, Portugal na Spain
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Maelezo zaidi yataelezwa siku zijazo, lakini ni wazi kutakuwa na safari ndefu - ikiwa ni pamoja na mashabiki wanaotarajia kuzifuata timu zao.

Ratiba pia inaweza kuleta changamoto kwa wale wanaotazama kutokea mbali, kuna tofauti ya saa tano kati ya Paraguay na Uhispania. Na safari ya ndege ni takriban saa 13 kati ya Argentina na Uhispania.

Kwa makadirio Fifa wenyewe, Kombe la Dunia la 2026 - ambalo limetabiriwa kuleta ongezeko la faida la pauni milioni 521 - litakawa shindano litakalo zalisha hewa ukaa zaidi kuwahi kufanywa.

Rais wa Fifa Gianni Infantino alisema uamuzi wa kupanua Kombe la Dunia uliongozwa na hitaji la mashindano hayo "kujumuika zaidi" na "sio kuhusu kupata pesa au madaraka".

Fifa iliiambia BBC Sport "inafahamu kikamilifu mabadiliko ya tabia nchi ni mojawapo ya changamoto kubwa zaidi ya wakati wetu na inaamini kila mmoja wetu anapaswa kuchukua hatua za haraka na endelevu".

Iliongeza: "Fifa pia inafahamu kikamilifu athari ambazo matukio makubwa yanaathiri uchumi, mazingira asilia na kwa watu na jamii, na imekuwa ikifanya juhudi kubwa kukabiliana na athari hizo."

Bodi hiyo ilisema "itatekeleza mkakati thabiti katika tukio hilo. Fifa itafanya kila linalowezekana ili kuongeza uzoefu wa timu, mashabiki na viongozi huku ikipunguza athari kwa mazingira."

Itakuwaje kwa mashabiki?

Kombe la Dunia linahusu uandaaji wa tukio, fursa kwa timu na mashabiki kujihusisha na utamaduni wa nchi mwenyeji.

Iwapo pendekezo hilo litaidhinishwa katika kongamano la Fifa mwaka ujao, Morocco itakuwa taifa la pili la Afrika kuwa mwenyeji baada ya Afrika Kusini mwaka 2010. Ureno itakuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza, huku Uhispania haijaandaa michuano hiyo tangu 1982.

Lakini je, furaha ya wale wanaotarajia kusafiri inaweza kuathiriwa na kiwango cha gharama zinazohusiana na mashindano yajayo?

"Kwa shabiki itakuwa changamoto," shabiki wa soka wa Uingereza Garford Beck, ambaye husafiri kutazama timu kwenye mashindano makubwa, aliiambia BBC Radio 5 Live.

"Ilikuwa tabu nchini Urusi, kutoka Moscow hadi Samara kwa robo fainali - ni safari ya masaa 18 kwenye treni kwenda na kurudi.

"Nadhani kile ambacho hawakielewi - mashabiki hawapendi mashindano yawe katika nchi mbili, achilia mbali sita au tatu."