Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wana nia ya kumsajili fowadi wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, kutoka PSG na huenda likawa chaguo la mkopo ambalo lina kifungu cha kumnunua kabisa mwezi Januari. (L'Equipe, kupitia Pata Habari za Soka za Ufaransa), za nje
Kolo Muani ni miongoni mwa mpango wa meneja Luis Enrique na na vilevile anaivutia RB . (Sky Sports Germany)
Newcastle United wanalenga kumnunua mlinzi wa Barcelona Andreas Christensen, 28, na kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark kunaweza kuruhusu klabu hiyo ya La Liga kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Dani Olmo, 26. (Fichajes - in Spanish),
Newcastle wanapanga kumuuza beki wa kushoto wa Uingereza Kieran Trippier, 34, na kiungo mshambuliaji wa Paraguay Miguel Almiron, 30, ili kusaidia msimamo wao linapokuja suala la sheria za faida na uendelevu. (Football Insider),

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wako tayari kuwaruhusu wachezaji wa kati wa Uingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 26, na Carney Chukwuemeka, 21, kuondoka kwa mkopo katika klabu hiyo mwezi Januari. (Mirror)
Leicester City wanapanga kumrejesha klabuni Dewsbury-Hall, baada ya kumuuza kwa Chelsea katika majira ya joto. (Football Insider)
Meneja wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter alikataa nia ya Wolves mwezi uliopita huku klabu hiyo ya Midlands ikitafuta chaguo kuchukua nafasi ya Gary O'Neil, ambaye kwa sasa ametimuliwa. (Guardian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Senegal Nicolas Jackson nusura ajiunge na Aston Villa na Bournemouth kutoka Villarreal Januari 2023 kabla ya kwenda Chelsea. ( 90min)
Klabu ya AC Milan ya Italia inakaribia kumpata mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic mwenye umri wa miaka 26 kwa mkataba mpya. (Fabrizio Romano)
AC Milan pia wanatazamia kuongeza mkataba wa kiungo wa kati wa Uholanzi Tijjani Reijnders na kipa wa Ufaransa Mike Maignan kwa masharti mapya na yaliyoboreshwa. (Calciomercato - In Itali)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












