Hizi ni sababu tano za kwanini ujianike juani

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Kwa miaka mingi, tumeambiwa ni hatari kwenda nje kwenye jua bila mafuta ya jua. Kwa hakika, miili yetu inaihitaji mwanga wa jua hasa kwa watu wanaoishi katika Kizio cha Kaskazini mwa dunia, ili kuboresha afya, kupunguza shinikizo la damu, kuimarisha mifupa, misuli, na hata mfumo wa kinga.

Kujiweka juani kuna manufaa kwa afya yako ya mwili na akili. Hiyo ni kwa sababu, bila ya jua la moja kwa moja, mwili wako hauwezi kuzalisha vitamini D, kemikali muhimu kwa mifupa, misuli, na mfumo wa kinga.

Nchini Uingereza, miale ya jua ina nguvu ya kutosha ya kuzalisha vitamini D kuanzia Aprili hadi Septemba, hivyo unahitaji kuongeza viwango vya vitamini D katika miezi hii ya kiangazi.

Binadamu tunahifadhi vitamini D tuliyoikusanya wakati wa kiangazi katika hifadhi yetu ya mafuta ili kuitumia wakati wa baridi!

Wengi wetu tuna viwango vya chini vya vitamini D wakati wa majira ya baridi, ukosefu huo hupelekea magonjwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na shida ya kupoteza kumbukumbu, kukosa kinga mwilini, na kisukari.

Pia unaweza kusoma

Kujisikia vizuri

jua

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwanga wa jua huongeza utoaji wa homoni ziitwazo serotonin katika ubongo wako, homoni ambazo hukufanya ujisikie utulivu na umakini.

Utafiti mmoja uligundua kuwa watu huwa na viwango vya juu vya serotonini katika damu zao wakati wa siku angavu ikilinganishwa na siku ya mawingu.

Pia waligundua kuwa kiwango cha uzalishaji wa serotonini kwenye ubongo kina uhusiano wa moja kwa moja na muda ambao kuna mwangaza wa jua.

Kuna baadhi ya tafiti zinaeleza, mwanga wa moja kwa moja wa jua, unaweza kusababisha seli za ngozi yako kuzalisha homoni za endorphins, ambazo pia hukufanya ujisikie vizuri!

Kupunguza shinikizo la damu

Mwangaza wa jua pia hupunguza shinikizo la damu moja kwa moja. Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh walifanya utafiti. Ikiwa utaweka mkono wako kwa dakika 20 tu juani, zinatosha kuongeza uzalishaji wa gesi ya Nitric oxide (NO) kwenye ngozi yako.

Gesi hii husababisha mishipa yako ya damu kupanuka, na kupunguza shinikizo la damu. Kwa hivyo kuna sababu nyingi za kuhakikisha unapata vitamini D.

Kuongeza nguvu

sun

Chanzo cha picha, Getty Images

Vitamini D ni muhimu kwa afya ya mifupa, haijalishi umri wako, na hukufanya uwe na nguvu zaidi. Utafiti wa hivi karibuni uligundua kuwa kula vitamini D kunaboresha nguvu ya misuli ya wanariadha, kwa kuchochea ukuaji wa seli za misuli.

Pia kuna ushahidi kwamba Vitamin D vinasaidia kukukinga na maambukizi ya njia ya upumuaji na kuongeza uimara wa mfumo wako wa kinga ya mwili.

Mwanga wa jua na vitamini D

SUN

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni kweli kwamba unaweza kupata baadhi ya vitamini D kutoka katika chakula, lakini ni vigumu sana kupata vitamini D vya kutosha kutokana na chakula pekee.

Vyanzo bora vya vitamini D ni samaki wa mafuta. Lakini kula vya kutosha ili kupata vitamini D unavyohitaji itakuwa ngumu. Kwa bahati nzuri, ni rahisi kuvipata kupitia jua. Mara tu mwanga wa jua unapopiga ngozi yako, mwili wako unaweza kunyonya mionzi na kuibadilisha kuwa kirutubisho hiki chenye nguvu.

Kiasi gani kinatosha?

NJI

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kiasi cha jua unachohitaji ili kupata kiwango bora cha vitamini D kinategemea aina ya ngozi yako na mahali unapoishi. Jambo muhimu zaidi ni kutounguza ngozi yako.

Ngozi nyeusi zina rangi inayoitwa melanin ambayo huwa ni kama kinga ya asili ya jua, hunyonya mionzi ya jua na kuilinda ngozi dhidi ya uharibifu.

Unaweza kufikiria kuwa kupigwa na jua kwenye uso wako inatosha lakini ili kufaidika zaidi, unapaswa kuweka wazi mikono na miguu yako pia. Unatakiwa utoke nje hata ikiwa kuna mawingu, kwani bado unaweza kupata mionzi hii hata kama kuna wingu jepesi.

Huenda umewahi kusikia kuwa haitakiwi kwenda nje katikati ya mchana, wakati jua ni kali zaidi, lakini kutembea wakati wa mchana ni njia bora ya kupata dozi yako ya vitamini D ya kila siku.

"Kwenda nje wakati wa mchana, ndipo unapotengeneza vitamini D nyingi zaidi," anasema Prof Ann Webb kutoka Chuo Kikuu cha Manchester. Ushauri huu ni kwa watu wanaosihi Uingereza tu na sio katika nchi ambazo jua ni kali sana.

Ikiwa utatoka nje kwa muda mrefu sana, kuna hatari ya ngozi yako kuungua, hivyo ni muhimu kuilinda ngozi yako. Hakikisha umeuifunika au kujipaka mafuta ya kuzuia jua.

Pengine unatamani ukae juani kwa muda mrefu, lakini vitamini D nyingi hutengenezwa dakika za mwanzo tangu miale ya jua ianze kukupiga. Na kupunguza muda wa kukaa juani, ni njia bora ya kuzuia ngozi kutoungua.

Wakati wa miezi ya baridi, unaweza kula vitamini D. Mikrogramu 10 ni kiwango mwafaka kufurahia manufaa mbalimbali ya vitamini hivi.