Virusi vya corona: Je ipo haja ya kutumia vidonge vya vitamin D?

Chanzo cha picha, Getty Images
Sekta ya afya nchini Uingereza inapendekeza watu wanywe vidonge vya vya virutubisho vya vitamini D kila siku katika msimu huu wa joto wakati ambao marufuku ya ya kutotoka nje kutokana na virusi vya corona ikiwa inaendelea.
Kwa kawaida wengi wetu huwa tunapata vitamini hiyo ya kutosha tukiwa nje wakati ambapo jua linapotupiga.
Vitamini D inaweza kusaidia mwili kuwa imara, na kuzuia kupata maambukizi hivyo ni muhimu wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa corona.
Ushauri huo unapendekeza nini?
Raia wa Uingereza wanashauriwa kuzingatia kuchukua nyongeza ya vijiko 10 kwa siku wakati wa miezi ya msimu wa baridi (kutoka Oktoba hadi Machi) na kama katika mwaka mzima hawatutatumia wakati mwingi nje.
Sekta ya afya nchini Uingereza ina wasiwasi kuwa watu wanaweza kukosa vitamini wakati wa janga la virusi vya corona wakati tunashauriwa kukaa nyumbani zaidi.
Tunachukua mionzi mingi kutoka katika jua ambapo mwili hutengeneza vitamini D.
Hali ikoje Afrika
Mtaalamu wa afya kutoka Tanzania anasema, mapendekezo hayo kwa Afrika pia ni muhimu, vitamin D inafahamika sana katika kusidia kuimarisha mifupa na kusaidia mwili dhidi ya magonjwa.
Tafiti mbalimbali barani Afrika zimeonyesha uhusiano katika ya upungufu wa Vitamin D na afya ya akili, mifupa na kadhalika.
Kwa sababu ya umuhimu huu, Kuna nchi Kama Marekani ambapo kipimo Cha Vitamin D kimekuwa na umuhimu pia.
Huku Afrika hakijakuwa maarufu sana lakini kuna hospitali za binafsi zinaweza unaweza kuomba upime kipimo hicho.
Kwa nini tunahitaji vitamini D?
Vitamini D ni muhimu kwa mifupa, meno na misuli yenye afya. Kukosekana kwake kunaweza kusababisha ugonjwa wa mifupa kitaalamu unaitwa rickets kwa watoto na hali kama hiyo ya udhaifu wa mfupa inayoitwa 'osteomalacia' kwa watu wazima.
Tafiti zingine zinaonyesha husaidia kupambana na homa ya kawaida pamoja na mafua, ingawa hakuna ushahidi kwamba vitamini D huongeza kinga.
Je! Ninapaswa kuitumia zaidi?
Hapana. Ingawa virutubisho vya vitamini D ni salama sana, kutumia zaidi ya kiwango kilichopendekezwa kila siku kinaweza kuwa mahdhara makubwa huko mbeleni.
Ukichagua kutumia virutubisho vya vitamini D:
- Watoto wenye umri wa miaka 1-10 hawapaswi kutumia zaidi ya kilo 50 kwa siku.
- Watoto wachanga (chini ya miezi 12) hawapaswi kutumia zaidi ya vijiko 25 kwa siku
- Watu wazima hawapaswi kutumia zaidi ya kilo 100 kwa siku, na ikiwa watatumia virutubisho hivyo kiasi kilichopendekezwa ni vijiko 10 kwa siku.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kipimo cha juu kabisa wakati mwingine kinaweza kupendekezwa na daktari kwa wagonjwa walio na upungufu wa vitamini D.
Walio na matibabu maalumu, kama vile figo, hawaruhusiwi kutumia vitamini D.
Inaweza kuzuia coronavirus?
Hapana. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba unapunguza hatari ya kuambukizwa au kuugua ugonjwa wa homa kali ya mapafu.
Lakini wataalam wanatazamia kuwa inaweza kuwa na faida wakati wa janga.
Virutubisho vya Vitamini D vitaboresha afya ya watu wasio na upungufu.
Watafiti wengine wamependekeza kwamba upungufu wa vitamini D unaweza kuhusishwa na matokeo ya kutokuwa makini ikiwa mtu atapata homa kali ya mapafu.
Lakini sababu zingine za hatari, kama ugonjwa wa moyo, ni kawaida kwa wagonjwa hawa pia, na inafanya kuwa vigumu kupata hitimisho.
Watafiti wa Uhispania na Ufaransa wanafanya majaribio ya kliniki kuona kama vitamini D itaweza kusaidia wagonjwa wa homa kali ya mapafu.
Prof Jon Rhodes, mtaalamu wa dawa nchini Uingereza, anasema vitamini D ina athari za kuzuia uchochezi na kuna utafiti ambao unaonyesha inaweza kupunguza kinga ya mwili kwa virusi.
Hii inaweza kuwa muhimu kwa wagonjwa wa homa kali ya mapafu, wagonjwa wanaosumbuliwa sana na mapafu wanaweza kutoka kwa dhoruba ya "cytokine" ya kujibu virusi, ingawa utafiti zaidi unahitajika ili kuchunguza hii, anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wapi naweza kununua?
Vitamini D zinapatikana kwenye maduka makubwa na madogo yaliokidhi vigezo.
Unaweza kuipata vitamini D pekee au sehemu yenye vitamin zote.
Usinunue zaidi ya unahitaji ili usaidie wengine nao pia wapate virutubisho hivyo, wataalam wanasema.
Kiunga kilichoorodheshwa kwenye lebo ya virutubisho vingi vya Vitamini D ni D3.
Vitamini D2 hutengenezwa na mimea, na Vitamini D3 ndio inayotengenezwa na ngozi yako.
Matone ya vitamini yanapatikana kwa watoto.












