Je Boris Johnson anaweza kweli kurejea tena mamlakani?

Chanzo cha picha, Reuters
Boris Johnson, mwanaume aliyeng’olewa mamlakani kama waziri mkuu wa Uingereza na serikali yake mwenyewe miezi mitatu tu iliyopita, amejitokeza kama mgombea aliye mstari wa mbele kuwa Waziri mkuu ajaye.
Aliyechukua wadhifa wake Liz Truss alijiuzulu baada ya siku 45 mamlakani, baada ya kulazimika kuachana na sehemu kubwa ya mpango wake wa sera baada ya kuporomoka ghafla kwa masoko ya fedha.
Bw Johnson alishinda katika ucgauzi mkuu wa mwaka 2019 -na chini ya katiba ya Uingereza chama kilichopo madarakani kinaweza kumbadilisha kiongozi bila uchaguzi.
Bw Truss alichaguliwa na wajumbe wa chama cha Conservative, ambao wanaweza kuwa na usemi wa mwisho katika mchuano wa sasa, iwapo wagombea wawili watasabakia baada ya wabunge kupiga kura.
Uwaziri mkuu wa Johnson utakuwa ni mageuzi yasiyo ya kawaida hata kwa mwanasiasa ambaye ameweza kurejea kwa miujiza uongozini kabla.
Mara ya mwisho mtu yeyote aliyerejea katika mamlaka ya Waziri mkuu baada ya kupoteza uongozi ilikuwa ni miaka 140 iliyopita wakati William Gladstone aliporejea uongozini kuongoza chama cha Liberal.
Na haiwezekani kwa njia yoyote ile kwamba Bw Johnson atagombea – bado hajaamua, tunaambiwa.
Ingawa kulingana na baba yake Stanley Waziri mkuu huyo wa zamani huenda yuko ndani ya ndege safarini akirejea Uingereza kutoka kwenye mapumziko yake katika Jamuhuri ya Dominica.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Will Walden, afisa wa zamani wa habari wa Bw Johnson, aliimbia Sky News kwamba Bw Johnson ana "sikiliza kwa makini sauti " kuhusu azma ya uongozi.
Katika mahojiano yake ya mwisho akiwa Waziri mkuu Bw Johnson alimalizia kwa wimbo "hasta la vista, baby".
Huenda alikua anatoa ishara kuu kwamba bado hajamalizwa kama angetumia usemi mwingine wa kuvutia kutoka kwa filamu za Terminator films: "Nitarejea."
Mmoja wa wafuasi wake sugu, Waziri wa biashara Jacob Rees-Mogga ameanzisha kampeni ya mtandao wa kijamii ya kumrejesha Bw johnson katika Downing Street, na makumi ya wabunge wa chama cha Conservative wamemuunga mkono wazi.
Waziri wa ulinzi Ben Wallace, anaoyeonekana kama nguvu ya ushawishi katika chama cha Conservative ameiambia BBC kuwa "anaegamia upande " wa kumuunga mkono Bw Johnson.
Sheria ya chama kuhusu uchaguzi wa uongozi inamaanisha kuwa wanaogombea wadhifa huo wanahitaji uungaji mkono wa walau wambunge wa Conservative 100 kufikia Jumatatu asubuhi ili kuendelea kubakia katika kinyang’anyiro.
Inavyoonekana, hii sio kazi ndogo kwa mtu ambaye wenzake 148 walipiga kura dhidi yake katika kura ya Imani iliyopigwa mwezi Juni - iliyofuatiwa na kujiuzulu kwa karibu watu 60 katika wizara mwezi mmoja baadaye .
Miezi ya mwisho kipindi cha Bw Johnson katika ofisi kilitawaliwa na shutuma kwamba alivunja sheria za wizara kwa kutosema ukweli kuhusu sheria ya Covid ya kuka nyumbani kwa kuendesha sherehe katika Downing Street.
Bado yuko chini ya uchunguzi wa kamati ya viwango ya bunge, ambao inaweza, kinadharia, kupelekea kuondolewa kwake bungeni, au hata kuondolewa kwenye kiti cha ubunge.
Msururu wa kashfa na maswali ya maadili ya kibinafsi vilimuangusha Bw Johnson. Je wabunge waliomuona kama mtu asiyeweza kuungwa mkono wiki sita zilizopita wanaweza kumkubali sasa?
Mbunge wa Conservative Sir Roger Gale amesema kuwa atajiuzulu kama mwanachama iwapo Bw Johnson atachaguliwa tena kama Waziri mkuu.
Sir Roger, mkosoaji wa mara kwa mara wa Bw Johnson, aliiambia Times Radio: "Ninadhani kwamba kutakuwa na watu, kama mimi ambao tutajipata katika nafasi mbaya ya kulazimika kujiuzulu katika mfumo wa usimamizi wa Conservative ."
Mwenzake katika Conservative Crispin Blunt pia amekwishasema wazi akidai kuwa Bw johnson sio mtu wa kurejesha sifa ya chama cha Conservative.
"Sitadhi kwamba tunataka kurejea nyuma ambako tulikuwa wiki sita zilizopita , tunahitaji kuangalia mbele," alisema Blunt.
Vyama vya upinzani pia vimeharakisha kulaani kauli kwamba Bw Johnson anaweza kurejea tena mamlakani.
Kiongozi wa Labour Sir Keir Starmer alisema kuwa Waziri mkuu "hafai kuongoza ofisi ". Waziri Mkuu wa Scotland Minister Nicola Sturgeon aliita kurejea kwa Johnson "pendekezo la kejeli".


Boris Johnson alikataa kuelezea kuwa hatarejea tena kabla ya kujiuzulu kwake.
Bw Johnson amekuwa kimmya kisiasa tangu alioondoka mamlakani. Alizungumza mara chache bungeni na ametumia wiki chache zilizopiota kfanya ziara ya mazungumzo ya marekani kabla ya kuelekea katika mapumziko.
Lakini kama mwandishi wa wasifu wake Andrew Gimson anavyoelezea yeye sio aina ya mtu’’wa kuishi maisha ya kutojulikana".
Kama tu mgombea mmoja atajitokeza shindano litakua limekwisha siku ya Jumatatu – kama haitakuwa hivyo kiongozi mpya atachaguliwa kwa kura kutoka kwa wajumbe wa chama kudikia Ijumaa tarehe 28 Oktoba.
Kura zilizochukuliwa katika siku za mwisho za uwaziri mkuu wa Liz Truss zimekuwa zikiendelea kuonyesha Bw Johnson kama mtu maarufu anayeweza kumrithi.
Patrick English, Mkurugenzi mwenza wa kampuni inayohusika na masuala ya kura YouGov, alisema chama cha Conservative wanamtafuta "mtu anayeweza kuleta umoja na kukiunganisha chama na kushindana tena(kiongozi wa Labour) Keir Starmer.
"Iwapo utawauliza wajumbe ni nani anayeweza kufanya hivo – Ni Boris Johnson," Bw English alisema.
"Kama Bw johnson ataenda katika wagombea wawili wa mwisho, amefika mwisho."
Kugombea kwa Boris Johnson kunaweza pia kuwasaidia wagombea wengine, kulingana na Bw English.
Rishi Sunak na Penny Mordaunt, ambao waligombea bila mafanikio katika kinyang’anyiro cha kumpata mrithi wa wa Bw Johnson pia wanaangaliwa kama watu wanaoweza kugombea tena.
"Ninadhani kama tunazungumzia kuhusu wagombea wanaoweza kuleta umoja na wanaoweza kuchukua maamuzi, Bw Sunak na Bw Johnson ni mfano halisi wa mgawanyiko mkubwa zaidi katika chama ," Bw Johnson alisema.
"Wanatambulika sana na makundi yao kwamba ninafikiri Bi Mordaunt ataweza kuja katikati na kusema kitu fulani kinaweza kufanyika ni mgombea wa umoja."
















