‘Niletee kichwa chake’-Jasusi aliyetumwa kumleta Bin Laden

TH

Chanzo cha picha, CENTRAL INTELLIGENCE AGENCY TWITTER

Mnamo tarehe 19 Septemba, 2001 - huku magofu ya majengo ya World Trade Center na Pentagon yakiendelea kufuka kutokana na mashambulizi ya 9/11 - afisa wa CIA Gary Schroen aliingia katika ofisi ya bosi wake na kupokea amri kadhaa: "Mkamate Bin Laden, umuue na urudishe kichwa chake kwenye sanduku kwenye barafu kavu."

Kuhusu naibu wa Osama Bin Laden, Ayman Al Zawahiri, na washiriki wengine wa ndani wa Al-Qaeda, maagizo yalikuwa sawa sawa: "Vichwa vyao juu ya miiba".

Ndani ya siku chache, Schroen na kikundi cha maafisa wa kijeshi walikuwa Wamarekani wa kwanza nchini Afghanistan, wakiwa tu na simu za satelaiti - lakini pia mamilioni ya dola taslimu ili kupata njia ya kuwawekea chamboni washirika watarajiwa. Wiki kadhaa baadaye, tarehe 7 Oktoba, Marekani ilianza mashambulizi yake dhidi ya Afghanistan inayotawaliwa na Taliban, na kusababisha vita vya karibu miaka 20 vilivyomalizika Agosti 2021.

Bin Laden aliuawa mwaka 2011, lakini ilichukua muongo mwingine kumuua Zawahiri.

Na tarehe 1 Agosti - siku moja tu baada ya ndege isiyo na rubani ya Marekani kumuua huko Kabul - Gary Schroen alikufa akiwa na umri wa miaka 80, akiripotiwa kuwa na kiharusi.

Baada ya kifo chake, mkurugenzi wa CIA William Burns alimsifu Schroen kama "Gwiji na mtu aliyeleta msukumo" kwa kila afisa anayefanya kazi ndani ya shirika la kijasusi la Marekani.

"Nchini Afghanistan zaidi ya miongo miwili iliyopita na katika kila jukumu lingine alilohudumu katika CIA, Gary aliwakilisha shirika letu na ubora wake," Bw Burns alisema. "Hatutasahau kamwe kujitolea kwake, uaminifu na uvumilivu."

Wachache ikiwa maafisa wowote waliokuwa wakihudumu katika CIA wakati huo walifaa zaidi kuongoza operesheni ya awali. Katika kipindi cha kazi iliyochukua miongo kadhaa, Schroen aliwahi kuwa "mkuu wa kituo" cha CIA kwa Afghanistan na Pakistan katika miaka ya 1980 na 1990.

Wakati huo, "hakukuwa na maslahi na serikali ya Marekani" nchini Afghanistan, baadaye alikumbuka katika mahojiano na PBS,

"Wataliban walikuwepo. Kila mtu alijua kwamba walikuwa wakitenda ukiukaji wa haki za binadamu na walikuwa ni serikali duni, inayowatendea watu wao vibaya," alisema. "Lakini kwa kweli, hakuna mtu huko Washington aliyejali sana."

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kufikia 1996, hata hivyo, Schroen alisema kwamba "hali ilikuwa imebadilika" baada ya ujasusi wa Marekani kuanza kuangazia shughuli za Osama Bin Laden, mwanajihadi ambaye wakati huo alikuwa hajulikani sana na mkongwe wa vita vya msituni dhidi ya Wasovieti katika miaka ya 1980.

Schroen aliunda sehemu ya kikundi kidogo ndani ya Kituo cha Kupambana na Ugaidi cha CIA ambacho kilionya juu ya tishio kutoka kwa raia huyo wa Saudi. Hivi karibuni Schroen alianza kuanzisha tena mawasiliano na makamanda wa Afghanistan ambao alikuwa anawafahamu tangu wakati wake katika eneo hilo.

Kwa miaka mitatu iliyofuata, kwa maelekezo ya Schroen, CIA ilijaribu mara kwa mara kumuua au kumkamata Bin Laden, kwa mipango kuanzia kuvizia kwenye msafara wake na uvamizi katika shamba lake kusini mwa Afghanistan ili kusafirisha makombora na mashambulizi ya mabomu.

Hatimaye, Bin Laden aliendelea na mipango ya milipuko ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998, na alinusurika shambulio kubwa la kombora la cruise kwenye vituo vya Al-Qaeda katika Jimbo la Khost nchini Afghanistan mwezi Agosti mwaka huo.

Miaka mitatu baadaye, watekaji nyara 19 wa Al-Qaeda walianzisha mashambulizi ya 9/11.

Ujumbe wa 2001 nchini Afghanistan - unaojulikana rasmi kama Operesheni Jawbreaker – ulimfanya Schroen na Wamarekani wengine saba kuungana na Muungano wa Kaskazini,(Northern Alliance)muungano wa vikundi vinavyopigana na serikali ya Taliban ambayo ilikuwa imetawala Afghanistan tangu 1996. Alipopata maagizo yake, Schroen, basi 59, ilikuwa tayari siku 11 katika mpango wa mpito wa CIA kwa wafanyikazi wanaostaafu.

"Sikutarajia kamwe kupata simu ya kuingia katoka oparesheni hii," alisema miaka kadhaa baadaye. "Nadhani lilikuwa chaguo sahihi, kutokana na uhusiano wangu wa muda mrefu na watu hao katika Muungano wa Kaskazini."

Tathmini ya Schroen iliungwa mkono na Michael "Mick" Mulroy, afisa wa zamani wa CIA, mkongwe wa vita wa Afghanistan na Naibu Katibu Msaidizi wa zamani wa Ulinzi.

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dhamira ya Gary Schroen ya 2001 ilikuwa kuungana na wapiganaji wa Northern Alliance kama hawa.

"Uzoefu wake nchini Afghanistan kabla ya Septemba 11, 2001 ulikuwa muhimu sana kwa mafanikio yetu huko katika uvamizi wa awali, uvamizi ambao aliongoza," Bw Mulroy aliiambia BBC. "Akiwa kwenye timu ya kwanza nchini Afghanistan, Gary aliweka mfano na kutoa mfano wa dhana ya kuongoza kutoka mbele."

Kama operesheni ya kijeshi, uvamizi wa Afghanistan ulikuwa wa mafanikio makubwa na kuwaondoa Taliban kutoka madarakani kufikia Desemba 2001. Lakini mlengwa mkuu wa Schroen - Bin Laden - na watu wengine wakuu wa Al-Qaeda kama vile Al-Zawahiri walitoroka, wakati Taliban walijikusanya na kupigana vita vya muda mrefu vya msituni ambavyo viliishia kwa machafuko ya Marekani kujiondoa Kabul mwaka jana.

Katika mahojiano ya baadaye katika maisha yake, Schroen alisema kushindwa kwa Marekani kuilinda Afghanistan na kuwakamata maadui wake wakuu kulitokana, kwa kiasi kikubwa, na kudhoofika kwa rasilimali za CIA na kijeshi kulikosababishwa na uvamizi wa Iraq wa 2003.

Licha ya madai ya awali kutoka kwa utawala wa Marekani wa George W Bush kwamba serikali ya Iraq kwa namna fulani ilihusishwa na mashambulizi ya 9/11, Schroen alisema kamwe haamini katika uhusiano wowote.

"Idadi ya watu, wafanyakazi wa CIA, katika kambi hizi ndogo za mbali na vituo vilipunguzwa kwa kiasi kikubwa ... kwa sababu ya mahitaji ya wafanyakazi kuongeza juhudi za Iraq," aliiambia NPR mwaka 2005. "Kwa kweli ilitugharimu, nadhani. , kasi kubwa. Kupoteza kasi ambayo bado iko leo." 

Hatimaye Schroen aliweza kustaafu katika miaka ya baada ya uvamizi wa Afghanistan, na mwaka wa 2005 alichapisha kitabu kilichoitwa "First In" kuhusu operesheni hiyo.

Hata miaka baada ya kustaafu, washirika wa bin Laden waliendelea kuona Schroen kama lengo walilofaa kuangamiza . Mnamo mwaka wa 2013, kundi la wanamgambo wa Kisomali la Al-Shabaab lilidai kwenye Twitter kuwa limemuua, na kusababisha maafisa wa Marekani ambao hawakutajwa majina kuwaambia NBC kwamba madai kama hayo yanapaswa kuchukuliwa "kwa chembe ya chumvi".

"Gary Schroen yuko hai na yuko sawa," ripoti ya NBC wakati huo ilitangaza.

Misheni ya Schroen inaendelea katika makao makuu ya CIA huko Virginia: Helikopta iliyotumika katika misheni ya 2001 inabaki kwenye uwanja wa CIA kama ukumbusho.