Ayman al-Zawahiri : Kiongozi wa Al Qaeda aliuawa vipi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la ujasusi la Marekani CIA limemuua kiongozi wa mtandao wa ugaidi wa Al-Qaeda, Ayman Al-Zawahiri, katia operesheni ya kupambana na ugaidi .
Mauaji haya, ambayo yamefanyika katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, yalifanywa usiku wa Jumamosi kuamuia Jumapili.
Al-Zawahiri, ambaye amekuwa akisakwa kwa muda mrefu, awali alikuwa naibu wa muasisi wa Al-Qaeda, Osama bin Laden, ambapo alichukua uongozi wa kundi hilo wakati Bin laden alipouawa tarehe 2 Mei, 2011.

Chanzo cha picha, Reuters
Al-Zawahiri aliuawa vipi?
Maafisa wa Marekani wamesema Zawahiri alikuwa amesimama kwenye veranda ya nyumba yake ya mafichoni. Ghafla, ndege isiyokuwa na rubani- inayofahamika kama drone- ikadondosha makombora mawili.
Taarifa inasema kuwa kombora lilimpiga Zawahiri ambaye alikuwa amesimama nyumbani kwake.
Ndugu wengine wa familia ya Ayman Al-Zawahiri walikuwepo pamoja naye katika eneo hilo, lakini hakuna mtu mwingine aliyeuawa wala kujeruhiwa katika shambulio hilo, na kiongozi wa Al-Qaeda akafa mara moja pale peke yake, maafisa walisema.
Agizo la Joe Biden.
Rais wa Marekani , Joe Biden, amethibitisha kwamba shambulio la ndege lililofanywa na Marekani limemuua kiongozi wa al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri.
Alisema kwamba aliidhinisha operesheni hiyo ifanyike Jumamosi katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul.
Biden amesema kuwa Ayman al-Zawahiri alihusika kikamilifu katika mashambulio yaliyofanyika nchini Marekani Septemba 11, 2001, ambayo yaliwauwa takriban watu 3,000.
Rais huyo wa Marekani aliongeza kuwa mauji ya al-Zawahiri ni habari njema kwa familia za wale waliouawa katika mashambulio.
Biden, ambaye mwaka jana aliyaondoa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, alisisitza kuwa nchi hiyo haitakuw amahala salama kwa makundi ya ugaidi tena.
Taliban imesemaje?
Kwa upande mwingine, msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid, amesema kuwa Marekani imefanya mashambulio ya droni katika kitongoji cha Sherpur cha mji mkuu Kabul, ambako wanaishi raia.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye ukurasa wake wa Twitter, Zabihullah alisema kuwa mwanzoni jinsi shambulio lilivyofanywa na lengo lake havikujulikana, baada ya vikosi vya usalama na ujasusi kufanya uchunguzi, iligundulikana kwamba shambulio lilifanywa na ndege isiyokuwa na rubani.
Msemaji wa Taliban amelaani shambulio na alilielezea kama ukiukaji wa sheria ya kimataifa na Makubaliano kuhusu Bonde.
Marekani yenyewe imesema kuwa Taliban ilifanya kosa kubwa kwa kumpatia hifadhi kiongozi wa Al-Qaeda mjini Kabul, jambo ambalo ni kinyume na makubalino baina ya pande mbili.
Muandalizi wa fikra nyuma ya Al-Qaeda
Uchambuzi na Gordon Corera, Mwandishi wa masuala ya usalama
Ayman al-Zawahiri ameelezewa kama mtu aliyeleta wazo la kuanzisha kwa mtandao wa Al-Qaeda network.
Alikuwa daktari kutoka Misri, na baadaye akawa mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu wa kikundi cha Al-Qaeda , ambacho kinajumuisha mashirika mengi ya Kiislamu.
Alifungwa jela katika miaka ya 1980 baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika kikundi cha wanamgambo wa Kiislamu.
Aliondoka nchini mwaka wakati alipoachiliwa na muda mfupi baada yah apo alijiunga na makundi ya jihadi ya kimataifa.
Hatimaye, alianzisha ngome nchini Afghanistan na kujiunga na jeshi lililoanzishwa na mwanaume Tajiri mzaliwa wa Saudia Osama bin Laden, ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza wa Al-Qaeda.

Chanzo cha picha, Reuters
Pamoja walitangaza vita dhidi ya marekani na kupanga mashambulio ambayo yalifanyika Septemba 11, 2001.
Ilichukua miaka 10 kufanikiwa kumpata na kumuua Osama bin Laden, ambaye hatimaye aliuawa na Marekani Septemba 2011.
Tangu wakati huo, Al-Zawahiri alikuwa alikuwa kiongozi wa Al-Qaeda, lakini ilikuwa ni nadra sana kuonekana binafsi au picha yake. Mar kadhaa alikuwa anatuma jumbe kuhusu masuala maalumu.
Wamarekani wanaona kifo chake kama ushindi wao mkubwa , baada ya vikosi vyao kuondoka kutoka Afghanistan mwaka jana.
Bila shaka kiongozi mpya atajitokeza kuliongoza kundi al-Qaeda, lakii huenda asiwe na ushawishi sawa na mtangulizi wake.












