Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 23.08.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raheem Sterling
Muda wa kusoma: Dakika 3

Winga wa Chelsea Raheem Sterling, 29, amepewa ofa kwa Aston Villa lakini Unai Emery hana uhakika kama mshambuliaji huyo wa Uingereza atafaa katika mipango yake. (Mirror)

Sterling hakuambiwa kwamba asingeichezea klabu ya Chelsea lakini ameondoa uwezekano wa kuhamia katika ligi ya Suadia . (Mail)

Leicester City wanakaribia kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace wa miaka 32 Jordan Ayew. (Sky Sports)

Wachezaji wengine wawili wa kiungo cha kati pia wako kwenye orodha ya kocha wa Leicester Steve Cooper kabla ya dirisha kufungwa. (Telegraph – subscription Required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ayew

Norwich City wamejitokeza kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Brazil Reinier, 22, kutoka Real Madrid. (O Globo – in Portugal)

Tottenham wanatazamiwa kumruhusu beki wa kati mwenye umri wa miaka 19 Ashley Phillips kujiunga na Stoke kwa mkopo. (Athletic – Subscription Required)

Girona wamekubali dili la awali la pauni milioni 21.2 pamoja na nyongeza na Watford kwa ajili ya kumnunua kiungo wa Colombia Yaser Asprilla, 20. (Sky Sports).

Brighton, Real Sociedad na Real Mallorca wanapigania kumsajili beki wa Ujerumani Mats Hummels mwenye umri wa miaka 35 kwa uhamisho wa bila malipo. (Florian Plettenberg).

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mats Hummels

Barcelona wamekubali makubaliano ya kibinafsi na winga wa Italia Federico Chiesa, 26, ambaye anatarajiwa kununuliwa kwa pauni milioni 11 kutoka Juventus. (Sport – In Spanish)

Everton, AC Milan, Bayern Munich na vilabu kadhaa nchini Uturuki vina nia ya kumsajili beki wa Newcastle Muingereza Kieran Trippier, 33. (Talksport).

Brentford wako tayari kukamilisha dili la £10m kwa winga wa Brazil Gustavo Nunes mwenye umri wa miaka 18 kutoka Gremio. (Fabrizio Romano)

Beki wa Jamhuri ya Ireland John Egan, 31, anafanya mazoezi na Burnley baada ya kuondoka Sheffield United. (Football Insider)

Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla