Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 19.11.2024

Muda wa kusoma: Dakika 4

Chelsea inapanga kuwasilisha ombi la kumunua Caoimhin Kelleher, Christian Pulisic anavivutia vilabu vya Ligi ya Premia, Ruben Amorim kufanya kazi na bajeti ndogo zaidi Manchester United.

Manchester United wanavutiwa na winga wa AC Milan na Marekani Christian Pulisic, 26, pamoja na Liverpool na West Ham . (Kalciomercato)

Chelsea wanapanga kumnunua kipa wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher mwenye umri wa miaka 25 msimu ujao wa kiangazi(Sun)

Ruben Amorim anatazamiwa kufanya kazi kwa bajeti ndogo zaidi kuliko ya mkufunzi wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag na atakuwa na jukumu la kuongeza uwezo ambao haujatumiwa katika kikosi huku klabu hiyo ikilenga kumaliza mzunguko mbaya na wa gharama kubwa wa marekebisho makubwa. (Telegraph - usajili unahitajika)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Denmark Christian Eriksen anapanga kuondoka kilabu hiyo msimu huu na hakuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu mkataba mpya. ( Fabrizio Romano)

Lakini Manchester United pia wanatafuta makubaliano ya kubadilishana ambayo yatamfanya mshambuliaji wao wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 23, ajiunge na Napoli , huku mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, akielekea Old Trafford. (Kalcio Napoli)

West Ham na Fulham wote wanavutiwa na kiungo wa kati wa Manchester City na England walio chini ya umri wa miaka 21 James McAtee mwezi Januari, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akiwa amebakiza dakika moja pekee ya Ligi Kuu ya Uingereza kufikia sasa msimu huu(Guardian)

Arsenal wanavutiwa na mshambuliaji wa Brazil Raphinha na wanaripotiwa kuandaa ofa inayokaribia pauni milioni 75. Hata hivyo, Barcelona hawako tayari kuachana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa chini ya pauni milioni 83. (Fichajes - kwa Kihispania)

Liverpool na Arsenal hawataweza kumsajili winga wa Ghana Mohammed Kudus kwa chini ya kifungu chake cha pauni milioni 85 msimu ujao, huku West Ham wakipania kusalia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Football Insider)

Nottingham Forest itapuuza ofa zozote za kumtaka mlinzi wa Brazil Murillo, 22, mwezi Januari, huku Real Madrid wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka. (Football Insider)

Winga wa Liverpool Federico Chiesa, 27, anaweza kurejea nchini kwao Italia mwezi Januari huku Inter Milan wakitarajia kuhamia kwa mkopo.(Mirror)

Chelsea , Manchester Cit y na Tottenham wanatazamiwa kumenyana kuipata sahihi ya mlinzi wa Bournemouth na Ukraine Illia Zabarnyi mwenye umri wa miaka 22. (Teamtalk)

Tottenham wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Valencia na Uhispania Javi Guerra, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akipatikana kwa kiasi kikubwa chini ya kifungu chake cha pauni milioni 84.(GiveMeSport)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 31, amedhamiria kuendeleza soka yake katika mojawapo ya ligi kuu tano za Ulaya baada ya kukatisha mkataba wake na Juventus wiki iliyopita. (ESPN)

Meneja wa Everton Sean Dyche atakuwa chini ya uangalizi wakati wa msururu mgumu wa Ratiba ya Toffees katika kipindi cha Krismasi. (Football Insider)

Arsenal wamewasiliana na mshauri wa soka wa Paris St-Germain Luis Campos kuhusu kuchukua mikoba ya mkurugenzi wa zamani wa michezo Edu.(Football Transfers)

Beki wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah, 28, ataanza kuzungumza na vilabu mwezi Januari huku akinuia kuwaacha mabingwa hao wa Bundesliga mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. Barcelona , Real Madrid na Bayern Munich ni miongoni mwa klabu zinaomtaka. (Mundo Deportivo)

Mshambulizi wa zamani wa Brazil Ronaldo anatayarisha kampeni ya kuwa rais mpya wa Shirikisho la Soka la Brazil mwezi Machi 2026 - na anataka kumteua mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola kama meneja ajaye wa timu hiyo. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah