Harriet Tubman: Mwanamke mweusi ambaye Biden anataka kumuweka kwenye $20

Harriet Tubman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanaharakati wa Marekani Harriet Tubman mwaka 1885.

Utawala wa Joe Biden unasema utaona namna wataavyoweza kuharakisha kupitisha muswada wa kutaka dola 20 ya Marekani kuwa na sura ya Harriet Tubman baada ya utawala wa Trump kuchelewesha zoezi hilo baada ya utawala wa Barack Obama kuanzisha mswada huo.

"Idara ya fedha watachukua hatua ya kuanza tena jitihada za kumuweka bi. Harriet Tubman katika noti ya dola $20 ,"Jen Psaki amesema kutoka idara ya habari ya Ikulu ya Marekani.

"Wanataka kusema fedha zetu, zinaashiria historia yetu na utofauti wetu , na picha ya Harriet Tubman ikiwekwa kwenye noti mpya ya dola 20 itaweza kuleta taswira ya namna hiyo."

Utawala wa Obama ilitangaza mwaka 2016 kuwa wataenda kumuweka Bi.Harriet Tubman katika fedha hiyo ya $20 na kumuondoa Andrew Jackson.

Lakini utawala wa Trump ulisema mwaka 2019 kuwa mabadiliko hayo yatachelewa na yanaweza kufanyika labda mwaka 2028 kwasababu za changamoto za kiteknolojia.

Na sasa Jen Psaki anasema wataongez kasi ili zoezi hilo lifanyike haraka iwezekanavyo.

Harriet Tubman on the $20
Maelezo ya picha, Namna ambavyo noti ya $20 inaweza kuonekana

Taarifa ya CNN inasema msemaji mmoja wa idara ya fedha anasema wanasubiri tu kupata uthibitisho wa kufanya hivyo.

Kama mabadiliko haya yakifanyika , Harriet Tubman atakuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa katika fedha ya Marekani.

Harriet Tubman ni nani?

Harriet Tubman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harriet Tubman mnamo mwaka 1885.

Harriet Tubman alikuwa anafanya kazi kama mtumwa, mpelelezi na mwishoni alihusika kukomesha biashara ya utumwa.

Alikuwa mwanamke jasiri , alipokutana na changamoto nyingi.

  • Harriet Tubman, alizaliwa katika mazingira utumwa mwaka 1822 huko Mashariki mwa Maryland. Ni mtoto wa nne kati ya watoto tisa na wazazi wake walimuita Araminta au Ross
  • Harriet Tubman alifanya mahojiano ya kwanza ya kuanza kazi akiwa na miaka mitano tu.
  • Harriet Tubman alitoroka shambani ambako alikuwa mtumwa na kukimbilia Pennsylvania mwaka 1849 lakini alirudi kuiokoa familia yake pamoja na watumwa wengine 300 .
  • Baada ya mabadiloko ya katiba ya utumwa ya mwaka 1850 ambayo iliruhusu watumwa kuwa huru nchini humo, Harriet Tubman aliwaongoza watumwa kutoroka ilikuwa huru Canada kwa kutumia reli ya chini.
  • Harriet Tubman alijulikana kwa jina la Bi. "Moses" wa reli ya barabara ya chini, ripoti zinasema hakupoteza abiria wake hata mmoja.
  • Harriet Tubman ni miongoni mwa watumwa waliopambana kutokomeza utumwa.
  • Kwa mujibu wa muandishi mmoja, Fergus Bordewich, ameandika Harriet Tubman alikuwa na nguvu sana kwa Wamarekani na aliwapa motisha ya kukabiliana katika vita ya wenyewe kupinga utumwa.
  • Wakati wa vita, Harriet Tubman alitengeneza umoja wa jeshi katika wapishi , manesi na baadae wapepelezi.
  • Harriet Tubman alifariki kutokana na nomonia akiwa na umri wa miaka 91 huko Auburn, New York mwaka 1913 baada ya kutoa maisha yake yote katika harakati za kupinga utumwa.