Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 15.10.2021: Lewandowski, Sterling, Mazraoui, Fekir, Sanches, Lingard, Sessegnon

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard yuko tayari kuondoka klabu hiyo mwezi Januari ili kuimarisha nafasi yake ya kuteuliwa katika kikosi cha England cha Kombe la Dunia mwaka ujao. Barcelona na AC Milan wamehusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo wa miaka 28. (Mirror)
Ajenti wa Roberto Lewandowsky Pini anaona klabu ya Manchester City kama klabu ambayo mshambuliaji huyo wa bayern na Poland mwenye umri wa miaka 33 anaweza kuhamia msimu ujao. (Bild - in German)
Real Madrid, Newcastle United, Arsenal na kurejea Liverpool ni miongoni mwa klabu ambazo mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, anaweza kujiunga nazo baada ya kutangaza kuwa yuko tayari kuondoka Manchester City. (Express)
Leeds United wanamfuatilia mlinzi wa Morocco na Ajax wa miaka 23 Noussair Mazraoui, ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa Arsenal na Roma. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Lille Olivier Letang amefichua kuwa kiungo wa kati wa Portugal Renato Sanches, 24, ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo ikiwa klabu kubwa itawasilisha ofa ya kumnunua Januari mwakani. (Express)
West Ham na Tottenham wamehusishwa na kipa Saint-Etienne Muingereza Etienne Green, 21. (TeamTalk)
Newcastle United wamewasiliana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Real Betis na Ufaransa Nabil Fekir, 28. (Footmercato - in French)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa Uhispania Cesar Azpilicueta, 32, na mchezaji mwenzake wa Chelsea Denmark beki Andreas Christensen, 25, ni miongoni mwa wachezaji ambao wananyatiwa na Barcelona kwa usajili msimu ujao. (Fichajes - in Spanish)
Liverpool wameonesha ishara ya kutaka kumsajili winga wa Leeds United na Brazil Raphinha, 24, wakati wa uhamisho wa msimu wa joto, wakala wa mchezaji huyo amedokeza. (Globo Esporte - in Portuguese)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana orodha ya walinzi wa Uingereza anaopania kuwasajili ambayo inawajumuisha Tariq Lamptey,21, wa Brighton, James Justin, 23 wa Leicester City, na Max Aarons, 21, wa Norwich. (Fichajes - in Spanish)
Fenerbahce wanatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham na England Ryan Sessegnon, 21, ifikapo Januari (Sun)
Arsenal hawana mpango wa kumuachilia mshambuliaji wa Brazil wa miaka 20 Gabriel Martinelli kuondoka kwa mkopo wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari. (90min)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham ni klabu ya hivi punde ya Ligi ys Primia kuonesha nia ya kumtaka mlinzi wa Stoke City Harry Souttar, huku Aston Villa wakiwa tayari wanamnyatia kiungo huyo wa Aausralia wa miaka 22. (Football Insider)













