Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 16.07.2021: Pellegrini, Abraham, Salah, Varane, Lingard, Vlahovic, Ajer, Emerson
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anawataka viongozi wa klabu kumsajili mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah,29, anayekipiga Liverpool ikiwa mchakato wa kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe utakwama msimu huu wa joto. (Fichajes - in Spanish)
Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 23 ambaye the blues pia wameashiria kuwa tayari kumuuza kwa Tottenham na Inter milan.Chelsea wanawalenga mshambuliaji wa Spurs na England Harry Kane mwenye umri wa miaka 27 na Romelu Lukaku wa Inter na Ubelgiji (Telegraph)
Tottenham wanamtaka mshambuliaji Danny Ings lakini wanakabiliwa na ugumu kwasababu Southampton wanasita kufanya biashara na klabu hiyo ya kaskazini mwa London. (Standard)
Tottenham wanaweza kumsajili kiungo wa kati wa Roma Lorenzo Pellegrini,25, lakini watatakiwa kutoa kititia cha pauni milioni 26 kumnasa Muitaliano huyo. (Athletic )
Mabingwa wa Uhispania Atletico Madrid wamekuwa wakihusishwa na taarifa za kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard, ambaye pia anatolewa macho na West Ham ambao walipendezwa naye alipokuwa kwa mkopo msimu uliopita. (90min)
Fiorentina wanalenga kuzuia kupokonywa nyota Dusan Vlahovic ambaye anamezewa mate na Liverpool na Tottenham kwa kuhakikisha wanampa mshambuliaji huyo wa Serbia mkataba mpya(Calciomercato - in Italian)
Real Madrid wameridhia kuwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Raphael Varane hatasaini mkataba mpya na wanasubiri ofa ya Manchester United. (Goal)
Brentford wanajiandaa kuweka mezani ofa ya ya pauni milioni 13.5 kwa ajili ya mlinzi wa Celtic Kristoffer Ajer,23. (Sun)
Mlinzi wa Chelsea Emerson Palmieri,26, anatakiwa na Inter Milan na Roma, huku akiwa chaguo pendwa kwa Napoli wakati pia wakimtolea macho Mathias Olivera, 23, anayekipiga Getafe. (Calciomercato)
Kumsajili mchezaji wa Arsenal Joe Willock,21, kwa mkataba wa kudumu bado imekuwa kipaumbele cha Newcastle United msimu huu baada ya kiungo huyo wa kati, 21, kuwepo St James' Park kwa mkopo msimu uliopita. (Chronicle)
AC Milan wamekataa zabuni ya pauni milioni 34 kutoka Paris St-Germain kwa ajili ya kiungo wa kati wa Ufaransa Theo Hernandez mwenye miaka 23. (Tuttosport - in Italian)
Inter Milan imeisitiza kuwa kiungo wa kati Nicolo Barella ''hataguswa'' baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 24 ataelekea Liverpool na Manchester United. (Fabrizio Romano on Twitter)