Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 15.07.2021: Nicolo Barella, Trippier, Koulibaly, Barella, Areola, Griezmann, Bellerin
Liverpool wanaripotiwa kutenga pauni milioni 60 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Inter Milan Nicolo Barella, 24. (La Repubblica)
Everton imewasilisha du la mwanzo kumsajili mchezaji wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 30 ambaye anaripotiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na maneja Rafa Benitez(Calciomercato)
Barcelona wanakaribia kukamilisha mpango wa kumpeleka mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 30, kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid ili iweze kumnasa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 26. (Mail)
Mlinzi wa pembeni wa England na Atletico Madrid Kieran Trippier kurejea ligi ya Primia wakati mchezaji huyo, 30, akisubiri uhamisho kuelekea Manchester United. (Telegraph - subscription needed)
Chelsea inataka kumtoa ofa mshambuliaji Tammy Abraham,23, kwenda Borussia Dortmund kama sehemu ya makubaliano ya kumchukua mshambuliaji wa miaka 20 Erling Braut Haaland. (Mirror)
West Ham wako mbioni kuridhia makubaliano ya mkopo,kwa kumnunua mlinda mlango wa Ufaransa wa Paris St-Germain Alphonse Areola, 28. (Evening Standard)
Mlinzi wa Arsenal Hector Bellerin bado hajakubaliana na Inter Milan lakini klabu hiyo ya Italia ina mpango wa kumnasa Mhispania huyo mwenye miaka 26. (Football.london)
Wakati huohuo kiungo wa kati wa washika bunduki hao Joe Willock,21, ameripotiwa kuiambia klabu kuwa atajiunga tena na Newcastle kwa mkopo kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya Primia. (Daily Express)
Leicester City wametoa ofa kwa mchezaji wa Ubelgiji Youri Tielemans, 24, ya mkataba wa muda mrefu na wanaamini kiungo huyo wa kati atasalia katika klabu hiyo, ingawa Liverpool wanamuhitaji.(Telegraph)
Tottenham ni moja kati ya klabu nne za ligi ya Primia zenye nia ya kumnasa mshambuliaji wa Schalke Matthew Hoppe,20, aliyefunga mabao sita na klabu ya Bundesliga msimu uliopita. (The Boot Room)
Mlinzi Brandon Williams, 20, anaweza kushuhudia uhamisho wake kwa mkopo ukiwa hatarini kuhamia Southampton kutokana na mahitaji ya kifedha ya Manchester United. (talkSPORT)
Kocha wa Roma, Jose Mourinho anaweza kuigeukia Old Trafford kuongezea nguvu kikosi chake msimu huu wa joto, huku kocha huyo wa zamani wa United akimtolea macho beki wa kushoto wa Brazil Alex Telles, 28, kama mbadala wa Leonardo Spinazzola aliye majeruhi. (Daily Star)
Arsenal inajiandaa kumkosa mshambuliaji wa PSV Eindhoven Mholanzi Donyell Malen, 22, baada ya kufikia makubaliano ya kujiunga na Borussia Dortmund kama mbadala wa Jadon Sancho (Just Arsenal via Sports Bild)