Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 11.07.2021: Di Lorenzo, Haaland, Kane, Camavinga, Emerson, Zidane, Giroud, Benzema
Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel anataka wakuu wa kilabu wachukue hatua ya "haraka" kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland kutoka Borussia Dortmund, lakini klabu hiyo ya Ujerumani inapanga bado kuwa naye Westfalenstadion msimu ujao kwani wanadai euro 175m (pauni milioni 150) kwa kijana huyo wa miaka 20 msimu huu wa joto. (Picha - kwa Kijerumani)
Manchester United inalenga kufanikisha uhamisho wa pauni milioni 17 kumsajili beki wa kulia wa Napoli na Italia Giovanni di Lorenzo baada ya mchezo wa mwisho wa Jumapili wa Uropa dhidi ya England. (Il Napolista, via Sun on Sunday)
Manchester United haifanyi juhudi za kuafikia makubaliano ya kubadilishana wachezaji kumleta mshambuliaji wa England Harry Kane, 27, Old Trafford kutoka Tottenham. (Sunday Express)
Chelsea imewasiliana na Rennes kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Ufaransa 18 Eduardo Camavinga, ambaye pia anasakwa na Manchester United, Arsenal na Real Madrid lakini inasemekana anapendelea kukaa Ufaransa na uwezekano wa kuhamia Paris St-Germain. (Le Parisien - via Sun on Sunday)
Meneja wa Everton Rafael Benitez ana nia ya kusajili beki wa kulia, na The Toffees inamuangalia nyota wa kimataifa wa chini ya miaka 21 wa Norwich City na England Max Aarons, 21, na Mholanzi Denzel Dumfries, 25, kutoka PSV Eindhoven. (90mins)
Napoli watafanya kila wawezalo kumsajili beki wa Italia mwenye umri wa miaka 26 wa Italia Emerson Palmieri kutoka Chelsea, ambaye Luciano Spalletti amemtambua kama lengo kuu msimu huu wa joto. (Corriere dello Sport - in Italian)
West Ham wapo mstari wa mbele kitafuta sahihi ya mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 23, na Aston Villa hapo awali walipenda kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa England wakati Wolves na Borussia Dortmund wote pia wanahusishwa naye. (Football Insider)
Burnley wanajishughulisha na dau la pauni milioni 13 kumsajili beki wa Lyon mwenye umri wa miaka 24, Maxwel Cornet, ambaye pia anasakwa na Hertha Berlin. (Sun on Sunday)
Tottenham inaweza kufanya iwe vigumu kwa Real Madrid kumsajili beki wa Ufaransa Jules Kounde kutoka Sevilla, Spurs ikiwa tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 51 kwa mchezaji huyo wa miaka 22 ambayo itakuwa zaidi ya kile klabu ya Uhispania inaweza kutumia. (Sport)
Chelsea pia imetangaza kupendezwa na Kounde na inaweza kujaribu kuteka nyara juhudi za Spurs kumsajili katika msimu wa joto. (Eldesmarque, via Sun on Sunday)
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane, 49, atakataa kurudi kwenye usimamizi wa kilabu na badala yake atasalia na matumaini ya siku moja uwezekano wa kufanikiwa kumrithi Didier Deschamps mwenye umri wa miaka 52 kama meneja wa Ufaransa (L'Equipe - via ESPN)
Kukamilika kwa uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud kutoka Chelsea kwenda AC Milan unatamatika , na mchezaji huyo wa miaka 34 akikubaliana mkataba wa miaka miwili na kilabu hiyo ya Italia. (Le Parisien - in French)
Kocha wa Everton Rafael Benitez amewauliza wakuu wa kilabu kuisaka saini ya beki wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 Clement Lenglet(Fichajes - in Spanish)
Karim Benzema, 33, atasalia Real Madrid hata kama kilabu hiyo ya Uhispania itafanikiwa kumsaini mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka Paris St-Germain msimu huu wa joto.(Marca)
Mabingwa wa Italia Inter Milan wameshinda harakati za kumsaini mchezaji wa chini ya miaka 16 wa Shamrock Rovers wa Jamhuri ya Ireland Kevin Zefi, 16, ambaye pia alikuwa akitafutwa na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu, na pia timu za Ujerumani na Uholanzi. (Sun on Sunday)
Barcelona wamekubali mpango wa kumuuza kiungo wa Uhispania Carles Alena mwenye umri wa miaka 23 kwenda Getafe wakati kilabu hiyo ya Catalan ikiendelea na juhudi zake za kupunguza gharama kujaribu kuhakikisha wanaweza kumpata fowadi wa Argentina Lionel Messi, 34, kujitolea kwa mkataba mpya. (Goal)
Juhudi za Arsenal kujaribu kumsajili mlinda mlango wa Ajax Andre Onana, 25, zimepata pigo wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroun akisema anapendelea kuhamia Lyon ya Ufaransa badala ya Ligi ya Premia.(Football London)
Tottenham wana imani kuwa wanaweza kumshusha beki wa miaka 23, Cameron Carter-Vickers, licha ya kuzidisha bei yao ya kumuuza hadi £ 5m. Wote Newcastle United na Celtic wanapendezwa na nyota huyo wa kimataifa wa USA (Football Insider)