Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 23.09.2018: Grealish. Sane, Ibrahimovic, De Jong, Cornet

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati Jack Grealish, 22, anatarajiwa kukataa ofa ya Tottenham na kusaini mkataba zaidi na Aston Villa. (Express)
Mwenyekiti wa Juventus Andrea Agnelli anataka mabingwa hao wa Italia kumsaini wing'a wa Manchester City mjerumani Leroy Sane, 22. (Calciomercato)
Mshambuliaji wa zamani wa LA Galaxy raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 36, amepewa ofa ya kurudi klabu yake ya utotoni ya Malmo. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanatajiunga na Manchester United katika mbio za kumasaini kiungo wa kati mholanzi Frenkie de Jong, 21. (Mirror)
City pia wataka kumsani tena kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, ambaye alikuwa na muda mfupi huko Etihad kama kijana na ambaye anatarajiwa klabua hiyi ya Ufaransa msimu ujao. (Star)
Mshambuliaji wa Ajax raia wa Brazil David Neres, 21, amehusishwa na Tottenham na Roma. (De Telegraaf, via Calciomercato)

Chanzo cha picha, Getty Images
Fulham wanatarajiwa kutoa ofa ya pauni milioni 18 kwa mshambuliaji wa Lyon raia wa Ivory Coast Maxwel Cornet, 21. (Sun on Sunday)
Arsenal walikataa fursa ya kumsaini mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk, 27, akiwa huko Cletic kwa sababu mholanzi huyo alikuwa mtulivu sana. (Bein Sports, via Metro)
Mlinzi wa Manchester City Kyle Walker, 28, anasema anataka kurudi nafasi yake ya beki na England baada ya kucheza kama kiungo cha kati na nyuma wakati wa kombe la dunia. (Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wolves wana mpango wa kuongeza bajeti ya chuo chao wakati wanaangalia bajeti za washindani wao Manchester City na Chelsea. (Sunday Mirror)
Stephen Caulker huenda yuko njiani kuelekea Wigan. Beki huyo wa zamani wa Cardiff na QPR 26, aliondoka Dundee msimu huu. (Mail on Sunday)
Kipa wa Manchester United mwenye miaka, 27, David de Gea ndiye bora zaidi duniani, kwa mujibu wa mwenzake wa Everton na England Jordan Pickford, 24. (Sunday Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Chelsea na Croatia Mateo Kovacic, 24, anasema anatazama video za YouTube za Paul Scholes wa Manchester United ili aweze kuboresha mchezo wake. (Sun on Sunday)
Wing'a wa zamani wa Arsenal na Sweden Freddie Ljungberg anasema anapenda kazi yake ya umeneja wa kikosi cha chini ya miaka 23 huko Gunners. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa zamani wa Newcastle Kevin Keegan alidanganya ili apate kuingia uga wa St James' Park baada ya kukosana na mmiliki wa klabu Mike Ashley. (Sunday Times - subscription required)
Bora Kutoka Jumamosi
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 25, alichunguzwa na maskauti wa Barcelona wakati wa mechi ya vilabu bingwa ya ushindi dhidi ya Young Boys. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
United inaongoza vilabu vya ligi ya Uingereza kurudisha tarehe ya mwisho ya uhamisho kuwa mwisho wa mwezi wa Agosti. (Mail)
Nyota wa Spurs Christian Eriksen, Toby Alderweireld na Danny Rose wanataka malipo yao kuongezwa ili kuwa sawa na yale ya Harry Kane ambaye analipwa kitita cha £200,000 kwa wiki. (Sun)
Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud analengwa na klabu ya Besiktas. Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 hana kandarasi katika klabu ya Chelsea msimu ujao . (Goal - in Turkish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa klabu ya Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot, 23, yuko tayari kujiunga na Manchester City kwa uhamisho usiokuwa na malipo wakati kandarasi yake itakapokwisha mwisho wa msimu huu. (Metro)
Mkufunzi wa zamani wa Swansea Carlos Carvalhal anataka kupewa fursa nyengine katika kufunza katika ligi ya Uingereza.. (Times - subscription required)
Barcelona inajiandaa kuwasilisha ombi la kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 29.












