Chelsea yaibuka na ushindi mwembamba 1-0 dhidi ya PAOK, Samatta ang'ara Genk ikiibuka na ushindi wa 2-0, Arsenal 4-2 Vorskla

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Mtanzania Mbwana Aly Samatta aliwafungia KRC Genk na kuwawezesha kuandikisha ushindi wa 2-0 dhidi ya klabu ya Malmö FF katika mechi ya Europa League zilizochezwa Alhamisi usiku.
Samatta alitumia mguu wake wa kushoto kutoa kiki kali kutoka katikati mwa eneo la hatari na mpira wake ukatua wavuni kwenye kona ya kulia kunako dakika ya 71.
Samatta alipumzishwa dakika ya 86 na badala yake akaingia Marcus Ingvartsen.
Bao la kwanza la Genk lilifungwa na Leandro Trossard kunako dakika ya 37.
Katika mechi nyingine usiku huo, Goli pekee la Willian dhidi ya PAOK Salonika katika ligi ya Europa lilitosha na kuendeleza mwanzo mzuri wa Chelsea kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali msimu huu Ulaya.
Pierre-Emerick Aubameyang naye alifunga mawili (32' na 56'), na Danny Welbeck (48') na Mesut Özil (74') wakajazia kikapu cha Arsenal na kuwawezesha kupata ushindi wa 4-2 dhidi ya Vorskla Poltava.
Willian raia wa Brazil ameichezea Chelsea kwenye Ligi ya Europa tangu Chelsea alipocheza mara ya mwisho mwaka 2013.
Alvaro Morata na Pedro walikosa nafasi za wazi za kuifanya Chelsea kushinda goli nyingi baada ya kuutawala mchezo kwa kiasi kikubwa.
Chelsea tangu ilipopoteza mchezo dhidi ya Manchester city kwenye Kombe la Ligi, ushindi wa jana unakuwa ni ushindi wa sita mfululizo msimu huu ,ushindi huo umeifanya kushika nafasi ya pili baada ya BATE Borisov Belarus ambayo inaongoza kundi L ikiifunga timu ya Vidi goli 2-0.

Kocha wa Chelsea Sarri alifanya mabadiliko ya wachezaji watano kutoka kwenye kikosi kilichoibuka na ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Cardiff, huku kikosi hicho bado kimeonyesha uhai mkubwa kikitegemewa kuleta changamoto kwenye mashindano inayoshiriki msimu wa 2018/2019.
Sarri alimpumzisha staa wake Eden Hazard baada ya kulalamika mwezi uliopita kuwa staa huyo anachoka, sambamba na Hazard, Sarri alimpumzisha David Luiz na Mateo Kovacic.
Willian alifunga goli katika dakika ya saba baada ya kupokea mgongeo murua kutoka kwa Barkley, Willian ambaye pia alianikiza ushindi wa Chelsea siku ya Jumamosi dhidi ya Cardiff ushindi wa goli nne kwa bila Hazard alifunga goli tatu (hat trick)
Ilikuwa ni mpira mzuri kutokakwa kiungo wa zamani wa Everton aliyeanzisha mashambulizi kutoka eneo la katika ya uwanja kabla haja mgongea Barkley ambaye akampasia Willian aliyekuwa upande wa kulia na kupiga shuti upande wa kulia mwa golikipa Alexandros Paschalakis.

Pamoja na kwamba wachezaji wengi wa Chelsea wanaonekana wameuelewa mfumo wa kocha bado Morata anahaha baada kutokea bechi mechi dhidi ya Cardiff akimpisha Giroud aliyeanza mechi hiyo.
Giroud alielewana vizuri kiuchezaji na Hazard siku ya Jumamosi na kufanya sababu ieleweka ya kwanini Sarri alichagua kumwazisha kama chaguo la kwanza mbele ya Morata.
Giroud alikuwa hana namba ya kudumu tangu Arsenal ingawa mwanzo mbaya wa Morata ambaye amefunga goli moja tu kwenye michezo mitano aliyoanza kunampa Giroud nafasi ya kucheza.
Chelsea ilikosa nafasi nyingi za wazi huku Morata akiwa amekosa nyingi Zaidi akionekana mzito baada ya kushindwa kumalizia mpira kutoka kwa Pedro na Antonio Rudiger.

Pedro alikuwa na nafasi ya kuongeza goli la pili katika dakika ya 38 baada Chelsea kufanya shambulio la kushitukiza huku mgongeo wa Marcos Alonso uliguswa ukampoteza Morata kuweza kufunga goli baada ya kupiga mpira kichwa ukapaa.
Willian alikaribia kufunga goli la pili kipindi cha pili, ingawa shuti lake lilikingwa na kupotea mabawa.
Ubora wa mlinda mlango Paschalakis ulizuia Pedro kujipatia goli, baadae Morata alitolewa katika dakika ya 81 kumpisha Giroud.
Mshambuliaji aliyetokea bechi wa PAOK Diego Biseswar alimanusuru aipatie goli la kusawazisha baada ya shuti kali lililolenga lango kuokolewa na kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga.
Takwimu za Mchezo
Makocha 10 Chelsea wa mpaka sasa wameshinda mechi zao za kwanza za mashindano ya ulaya, isipokuwa Claudio Ranieri alishindwa kufanya hivyo septemba 2000 (0-2 v FC St Gallen).
Chelsea wameshinda michezo yote ya minne ya mwisho ya Ligi ya Europe ikijumuisha na michezo mitatu ya fainali mwaka 2012-2013..
Kocha Maurizio Sarri ameshinda michezo yote saba ya hatua ya makundi, michezo mitano akiwa hajaruhusu wavu wa timu yake kutikiswa . Ross Barkley amesaidia goli lililofungwa na Willian kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe na Chelsea, huku mara ya mwisho alisaidia goli April 2017.
PAOK wameshindwa kufunga hata goli moja katika michezo sita ya nyumbani katika mashindano ya Ligi ya Europe.
Matokeo ya michezo mingine
Arsenal 4-2 Vorskla
Akhisarspor 0-1 FK Krasnodar
Sevilla 5-1 Standard Liege
Dynamo Kiev 2- 2 FC Astana
Rennes 2-1 FK Jablonec
MOL Vidi 0-2 BATE Borisov
PAOK Salonika 0-1 Chelsea
Rapid Vienna 2-0 Spartak Moscow
Villarreal 2-2 Rangers
Lazio 2-1 Apollon Limassol
Marseille 1-2 Frankfurt
Besiktas 3-1 Sarpsborg 08
KRC Genk 2-0 Malmö FF













