Kuagwa kwa Malkia Elizabeth: Je, foleni ni ndefu kiasi gani?

People queuing to see the Queen near Westminster

Chanzo cha picha, PA Media

Foleni ndefu zinashuhudiwa kando ya Mto Thames, watu wakisubiri kutoa heshima zao kwa Malkia.

Ataendelea kuagwa kwa saa 24 kwa siku hadi 06:30 BST Jumatatu 19 Septemba - siku ya mazishi.

Haya ndiyo unayohitaji kujua kabla ya kujiunga na foleni hiyo.

Nitapanga foleni kwa muda gani?

Serikali ya Uingereza imechapisha programu inayofuatilia moja kwa moja foleni ya watu wanaosubiri kuaga mwili wa Malkia kwenye YouTube.

Kwa sasa foleni ina urefu wa maili tatu na nusu.

Alama ya karibu zaidi nyuma ya foleni hiyo ni Tower Bridge.

Mwanamume mmoja, kuelekea mbele ya foleni karibu na Ukumbi wa Westminster, aliambia BBC Alhamisi asubuhi alikuwa amepanga foleni kwa saa nane.

Watu walio kwenye foleni wanaonywa kwamba watahitajika kusimama kwa saa nyingi bila fursa ya kuketi, kwa kuwa foleni inasonga kila mara.

Urefu mkubwa zaidi wa foleni ni maili 10 - na maili 6.9 kutoka Westminster hadi Southwark, na foleni ya kupinda pinda ya maili tatu ikionekana huko Southwark Park.

Map showing the queue indicating distance in miles

Chanzo cha picha, BBC News

Je, najiunga na foleni kuanzia wapi?

Angalia kifuatiliaji ili kuona sehemu ya nyuma ya foleni ilipo.

Watu wanapaswa kupokea bangili za rangi wakati wanajiunga, ili waweze kuondoka kwenda kunywa, au kwenda chooni, na kisha kurudi.

Wale walio kwenye foleni wanaombwa wasijaribu kuhifadhi nafasi kwa ajili ya mtu mwingine, au kuacha vitu vya kibinafsi bila kuwa na mtu wa kuvitunza, au kuweka hema.

Kadiri foleni inavyozidi kuwa ndefu, inaendelea kusonga hadi Ukingo wa Kusini, ambapo itafuata kingo za Mto Thames, kupita ukumbi wa michezo wa Kitaifa, Tate Modern na HMS Belfast, hadi Southwark Park.

Mara tu watu wanapofika mbele ya foleni, watapitia Tuta la Albert na kisha kuelekezwa kuvuka Daraja la Lambeth, hadi kwenye bustani ya Victoria Tower, kuelekea Bunge.

Watalazimika kupitia usalama wa mtindo wa uwanja wa ndege kabla ya kuingia ukumbi wa Westminster, ndani ya kasri la Westminster.

Je, ninaweza kwenda chooni wapi wakati nikipanga foleni?

Kuna zaidi ya vyoo 500 vinavyobebeka katika sehemu mbalimbali kando ya njia hiyo.

Majumba ya ndani na majumba ya makumbusho - ikijumuisha Kituo cha Southbank, Ukumbi wa Michezo wa Kitaifa, BFI Southbank na Globe ya Shakespeare - yatakaa wazi kwa saa nyingi na katika hali zingine kwa saa 24, kwa watu kutumia vifaa vyao.

Kahawa na biashara zingine za ndani pia zinatarajiwa kufunguliwa kwa muda mrefu.

Maelezo ya video, Watu wamepanga foleni usiku kucha ili kupata nafasi ya kutoa heshima zao kwa Malkia

Je, mwisho wa kupanga foleni hiyo ni lini?

Kipindi cha kuaga mwili kinaisha saa 06.30 BST siku ya Jumatatu, 19 Septemba, na kujiunga na foleni kutafungwa mapema ili kuhakikisha kuwa watu wengi iwezekanavyo wanaweza kuingia kuaga mwili. Uamuzi wowote wa mwisho wa kujiunga na foleni utachapishwa kwenye akaunti za serikali za mitandao ya kijamii.

Je wasiojiweza wanaweza kufika vipi eneo hilo?

Watafika eneo hilo bila kufuata utaratibu huo kupitia njia tofauti kwa wale wenye ulemavu kuanzia Tate Britain.

Nafasi za kuingia zilizoratibiwa zitatolewa ili kujiunga na foleni kando ya Millbank.

Ufikiaji wa eneo hilo bila kufuata mchakato uliowekwa unawezekana huko Westminster Hall kwa wale wenye uhitaji, mbwa wa kuwaongoza na mbwa wengine wa usaidizi wataruhusiwa.

Wakalimani wa lugha ya ishara ya Uingereza pia watapatikana.

Wasaidizi wa wageni katika Bunge wataongoza watumiaji wa viti vya magurudumu na watu wowote wenye matatizo ya kutoka sehemu moja hadi jingine (na walezi wao) kwenye njia ya kufikia Westminster Hall.

Je huduma za ziada za treni zitakuwepo?

Wakubwa wa usafiri wamethibitisha huduma za ziada za treni zitaendelea.

Usafiri wa London unasema eneo la Westminster la London ''litakuwa na shughuli nyingi'. Watu wanaombwa kuepuka kuendesha gari kuingia London ikiwa inawezekana. Baadhi ya barabara zitafungwa, haswa karibu na Westminster yenyewe, ambako kutatatiza huduma za mabasi.

Watoa huduma za usafiri wanasema njia bora ya kuingia katikati mwa London itakuwa kwa kutumia hudumza za treni za chini ya ardhi kuingia London, ingawa kunaweza kuwa na kituo cha muda ndani ya muda mfupi, pamoja na mipangilio maalum ya kupanga foleni.

Wageni wanashauriwa kupanga mapema, kuangalia maelezo ya safari ya wakati halisi, na kufikiria kutembea badala yake inapowezekana.

Watu pia wanaombwa kuepuka kituo cha Green Park Tube isipokuwa wahitaji huduma za dharura.

Je, ninahitaji tikiti?

Huhitaji tikiti.

Pia kuna idadi ya sheria kuhusu kile unachoweza kuchukua katika Ukumbi wa Westminster, na jinsi wageni wanapaswa kuwa - kuna maelezo zaidi kwenye tovuti ya Bunge.

Je, ninahitaji kuleta kitambulisho?

Watu hawatahitaji kuonyesha vitambulisho rasmi ili kuingia ukumbini, lakini ukaguzi wa usalama wa mtindo wa uwanja wa ndege utafanyika.

People queuing to see the Queen near Westminster Bridge

Chanzo cha picha, PA Media

Nilete nini?

Watu wanashauriwa kuangalia hali ya hewa mapema, na kuvaa ipasavyo.

Pia wanashauriwa kuleta:

  • vyakula na vinywaji - ingawa vitahitajika kuliwa au kutupwa kabla ya kufika kwenye ukaguzi wa usalama
  • dawa au vifaa vyovyote muhimu
  • chaja ya simu inayobebeka.

Siwezi kubeba nini?

Kuna mwongozo wa kina juu ya kile ambacho hakiwezi kuletwa ndani ya ukumbi, ambayo ni pamoja na:

  • chupa za chai au chupa zisizo wazi - chupa za maji angavu pekee ndizo zinazoruhusiwa
  • maua au vitu vingine vya kutoa heshima - maua yanaweza kupelekwa kwenye eneo lililotengwa katika wakfu wa Bustani ya Green Park
  • vitu vyovyote vyenye ncha kali ikiwa ni pamoja na visu,
  • Vipoeza, mifuko ya kulalia na vifaa vingine vya kwenye kambi
  • viti vya kusukuma visivyoweza kukunjwa
  • mabango, bendera, matangazo au ujumbe wa uuzaji

Bidhaa zozote zilizopigwa marufuku zitachukuliwa na hazitarejeshwa.

Polisi wanaweza pia kufanya ukaguzi wa usalama kwenye sehemu za kupanga foleni.

Kila mtu anaruhusiwa tu kubeba mfuko mmoja mdogo wenye funguo moja au zipu

Kutakuwa na kituo cha kudondoshea vitu, lakini kitakuwa na uwezo mdogo, na ukitaka kuutumia, huenda ukachukua muda wa ziada kusubiri hadi uweze kupatikana ukiwa sawa kutumika.

Ni sheria gani za kufuata ukiwa ndani?

Watu wanaombwa kuheshimu hadhi ya tukio, na wanapaswa kukaa kimya wakiwa ndani ya kasri la Westminster na kuvaa ipasavyo, Mtu yeyote aliyevaa nguo zenye ''kauli mbiu za kisiasa au za kuudhi'' hataruhusiwa kuingia.

Simu za rununu na vifaa vingine vya umeme vinapaswa kuzimwa au kuwekwa katika hali ya kuwa havitoi sauti.

Ukiwa ndani ya Ukumbi wa Westminster, foleni itagawanywa kupita kila upande, ambayo ni jukwaa lililoinuliwa ambapo jeneza lililofungwa liko.

Wageni wanaombwa kuendelea kusonga mbele wakati wote wakiwa kwenye foleni, hadi watakapotoka kwenye Viwanja vya Bunge.

Je, ninaweza kupiga picha?

Sio ndani.

Upigaji picha na matumizi ya simu za mkononi au vifaa vingine havitaruhusiwa katika eneo la utafutaji wa usalama au punde utakapoingia ndani ya kasri la Westminster.

A woman places flowers in St. James' Park near Buckingham Palace (10 September 2022)

Chanzo cha picha, Reuters

Je, nikihitaji usaidizi wa kimatibabu?

Kuna vituo nane vya huduma ya kwanza vinavyoendeshwa na St John Ambulance kando ya foleni.

Wako Bustani ya Southwark, Potters Fields Park, Tate Modern, Southbank Centre, Belvedere Road, Bustani ya Archbishop, Kasri la Lambeth na Bustani ya Victoria Tower.

Na zaidi ya watu 1,000 wa kujitolea, wasimamizi na maafisa wa polisi watakuwepo kusaidia yeyote anayehitaji.

Wanaojitolea wanatoka Skauti, Wasamaria, Msalaba Mwekundu wa Uingereza, Uuguzi wa Huduma ya Kwanza Yeomanry na Salvation Army yaani Jeshi la Wokovu.

Ninaweza kupata wapi kinywaji?

Kuna vituo vya maji na vinjwaji kando ya njia, kwenye maeneo maalum na makumbusho.

Ukimya wa kitaifa ni lini?

Kimya cha dakika moja kitafanyika kote Uingereza saa 20:00 BST Jumapili 18 Septemba, usiku kabla ya mazishi ya Malkia.

Vipi kuhusu zawadi za maua?

Idadi kubwa ya zawadi za maua tayari zimewekwa na umma katika makazi ya kifalme karibu na Uingereza. Kaya ya Kifalme imetoa mwongozo juu ya wapi wanaweza kuachwa:

Katika kasri la Buckingham, tovuti maalum zimeanzishwa katika eneo la Green Park na Hyde Park.

Katika kasri la Windsor, wanaweza kuachwa kwenye Lango la Cambridge na katika Familia ya Kifalme kwenye mtaa wa Sandringham Estate huko Norfolk, maua yanaweza kuachwa kwenye Lango la Norwich.

Katika kasri la Balmoral, ambapo Malkia alikufa siku ya Alhamisi, maua yanaweza kuachwa kwenye Lango Kuu.

Baraza la Aberdeenshire limewataka watu kutumia huduma za bustani na wapanda farasi kutoka kwa makazi ya karibu ya Braemar na Ballater kwani hakuna ufikiaji wa eneo hilo kupitia barabara kwa sasa.

Huko Edinburgh, washiriki wa umma wanaweza kuweka maua kwenye Bustani ya Fizikia, karibu na Lango la Abbey Strand kwenye Jumba la Holyroodhouse.

Katika kasri la Hillsborough Castle maua yanaweza kuachwa Forecourt mbele ya lango kuu.

Shirika la Kifalme lilisema bidhaa zisizo weza kuvunjika, kama vile mwanasesere, zinapaswa kuepukwa inapowezekana.

Ninaweza kusaini wapi kitabu cha maombolezo?

Mamlaka nyingi za mitaa zimeanzisha vitabu vya rambirambi katika maktaba, kumbi za miji na majengo mengine ya kiraia.

Unaweza kutumia linki kupata mamlaka ya eneo lako, kisha utembelee tovuti yake ili kujua kinachoweza kupatikana karibu nawe.

Ninawezaje kutoa heshima zangu mtandaoni?

Kuna kitabu cha mtandaoni cha maombolezo kwenye tovuti ya Familia ya Kifalme ambacho kinaweza kupatikana kwa kubofya hapa.

BBC News pia inakusanya hadithi na kumbukumbu zako za Malkia kwa ukurasa wetu wa mtandaoni wa heshima - unaweza kushiriki matukio yako maalum nasi kupitia fomu hii ya mtandaoni.

HM Queen Elizabeth II 640x55
HM Queen Elizabeth II black line