Wageni wa mazishi ya Malkia: Ni nani amealikwa na nani hakualikwa?

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Mazishi ya Malkia yanayotatajiwa kufanyika Jumatatu yamepangwa kuwa kusanyiko kubwa la wafalme na wanasiasa kuwahi kukongamana nchini Uingereza kwa miongo.

Mialiko ilitolewa mwishoni mwa juma, huku wakuu wa nchi 500- na waheshimiwa wa kigeni wakitarajiwa kuhudhuria.

Wengi wa viongozi wameombwa kuwasili katika ndege za kibiashara na kuambiwa kuwa watachukuliwa kwa mabasi, kutoka katika eneo la magharibi mwa London.

Hafla itafanyika katika Westminster Abbey, eneo ambalo lina uwezo wa kuwapokea watu wapatao 2,200.

Haya ndiyo yanayofahamika hadi sasa kuhusu ni nani atakayehudhuria na ambaye hatahudhuria.

Familia za kifalme za Ulaya

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mfalme Willem-Alexander na Malkia Maximawa uholanzi atakuwa miongoni mwa wafalme wa Ulaya katika mazishi

Familia za Wafalme wa Ulaya. Mfalme Willem-Alexander na Malkia Queen Maxima wa Uholanzi watakuwa ni miongoni mwa Wafalme wa Ulaya katika mazishi.

Wajumbe wa familia za kifalme kutoka kote Ulaya, ambao wengi wao walikuwa undugu wa damu wa Malkia, wanatarajiwa.

Mfalme wa Ubelgiji Philippe na Malkia Mathilde wamethibitisha kuwa watakuwa pale, huku Mfalme Willem-Alexander na mke wake, Malkia Maxima, pamoja na mama yake, Mwanamfalme malkia wa Uholanzi Beatrix.

Mfalme Felipe na Malkia Letizia wa Uhispania pia wamekubali mwaliko, sawa na familia za ufalme za Norway, Sweden, na Demark.

Marais wa Marekani

G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais Joe Biden, akionekana akisaini kitabu cha rambirambi dkwa Malkia, atahudhuria pamoja na Mke wake Jill Biden

Ikulu ya White House imethibitisha kuwa Rais Joe Biden atahudhuria pamoja na Mke wa Rais Jill Biden, ingawa inafahamika kuwa hawatasafiri kwa basi.

Mjadala mwingi umeangazia kuhusu iwapo Rais Biden atamualika mtangulizi wake, Donald Trump, kuwa sehemu ya ujumbe wa Marekani, lakini ukomo wa ukubwa wa ujumbe unamaanisha kuwa haitakuwa lazima marais wote wa zamani weweze kuhudhuria.

Kumekuwa na tetesi kwamba rais wa zamani na wake wa marais – hususan Obama na mke wake – wanaweza kupokea mialiko ya kibinafsi.

Jimmy Carter, ambaye alihudumu kama rais kuanzia mwaka 1977 hadi 1981, hajapokea mwaliko, ofisi yake imeliambia gazeti la Politico.

Viongozi wa Jumuiya ya Madola

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa India Narendra Modi hajathibitisha iwapo atahudhuria

Viongozi kutoka kote katika Jumuiya ya Madola, ambako Malkia alihudumu kama mkuu wake katika kipindi chote cha utawala wake, wanatarajiwa kuhudhuria.

 Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese amekubali mwaliko, sawa na Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern na Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau.

 Majenerali-magavana kadhaa ambao wamehudumu kama wawakilishi wa ufalme katika Jumuiya ya Madola wanatarajiwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa nchi zao.

 Waziri mkuu wa Bangladesh aliyehudumu kwa muda mrefu Sheikh Hasina na Rais wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe pia wameripotiwa kukubali mialiko. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi bado hajathibitisha iwapo atahudhuria.

Viongozi wengine wa dunia

CHRISTOF STACHE

Chanzo cha picha, CHRISTOF STACHE

Maelezo ya picha, Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na Rais wa Italia Sergio Mattarell watahudhuria mazishi

Viongozi kutoka kote katika Jumuiya ya Madola, ambako Malkia alihudumu kama mkuu wake katika kipindi chote cha utawala wake, wanatarajiwa kuhudhuria.

Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese amekubali mwaliko, sawa na Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern na Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Majenerali-magavana kadhaa ambao wamehudumu kama wawakilishi wa ufalme katika Jumuiya ya Madola wanatarajiwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa nchi zao.

Waziri mkuu wa Bangladesh aliyehudumu kwa muda mrefu Sheikh Hasina na Rais wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe pia wameripotiwa kukubali mialiko. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi bado hajathibitisha iwapo atahudhuria

Viongozi wengine wa dunia

G

Chanzo cha picha, CHRISTOF STACHE

Maelezo ya picha, Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na Rais wa Italia Sergio Mattarell watahudhuria mazishi
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Viongozi wengine wa dunia ambao wamesemekana kukubali mialiko ni pamoja na rais wa Irish Taoiseach Micheal Martin, rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, na rais wa Italia Sergio Mattarella pamoja na Rais wa tume ya Muungano wa Ulaya Ursula von der Leyen.

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-Yeol na rais wa Brazil Jair Bolsonaro pia wamethibitisha kuhudhuria kwao.

Pia anayetarajiwa kusafiri kuelekea London kwa ajili ya mazishi ya Malkia ni Mfalme wa Japan Naruhito, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Haijafahamika iwapo rais wa Uchina Xi Jinping, ambaye ziara yake katika Kazakhstan na Uzbekistan wiki hii itakuwa ni ya kwanza kwake kuondoka Uchina tangu mwanzoni mwa janga la Covid-19, atapokea mwaliko au ataukubali.

Jamuhuri ya kiislamu ya Iran, ambayo imekumbwa na vikwazo vya muda mrefu vya kimataifa kutokana na mpango wake wa nyuklia, itawasilishwa tu na balozi wake, vyanzo vya Whitehall vilisema.

Ambao hawakualikwa

Getty

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Urusi Vladimir Putin ni miongoni mwa viongozi wa dunia ambao hawajaalikwa

Hakuna mwakilishi kutoka Urusi, Belarus, au Myanmar ambaye amealikwa , anasema mwandishi wa BBC James Landale.

Uhusiano wa kidiplomasia baina ya Uingereza na Urusi ulivunjika, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, na msemaji wa rais wa Urusi Vladimir Putin alisema wiki iliyopita kwamba "hakuwa anafikiria uwezekano " wa kuhudhuria mazishi.

Uvamizi ulianzishwa kwa sehemu kutoka eneo la Beralus, ambayo rais wake, Aleksandr Lukashenko, ana ushirika wa karibu na Rais Putin.

 Uingereza imeondoa kwa kiwango kikubwa uwepo wake wa kidiplomasia katika Myanmar tangu yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi katika nchi hiyo mwezi Februari 2021.