Barani Afrika kuna maoni tofauti kuhusu urithi wa Malkia

A newspaper vendor seen reading a local daily reporting on the death of Queen Elizabeth II in the city of Nairobi. Queen Elizabeth II

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Na Nomsa Maseko
    • Nafasi, BBC News, Johannesburg

Kifo cha Malkia Elizabeth II kimesababisha kumiminiwa kwa jumbe za huzuni na heshima kutoka kwa viongozi wa ulimwengu na watu wa kawaida kwa njia sawa

Wengi katika makoloni ya zamani ya Uingereza wameheshimu kumbukumbu ya Malkia waziwazi, wakati wengine wameshiriki picha zake akitembelea nchi zao.

Lakini pongezi si kwa kauli moja. Kwa baadhi,kifo chake kimeamsha kumbukumbu za historia ya umwagaji damu wakati fulani wa utawala wa kikoloni - ukatili dhidi ya watu wa kiasili, wizi wa vinyago na vitu vya sanaa kutoka mataifa ya Afrika Magharibi, dhahabu na almasi kutoka Kusini mwa Afrika na India, utumwa na ukandamizaji.

Wakati Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akimtaja Malkia kama mtu wa ajabu wa umma ambaye atakumbukwa sana na watu wengi duniani, chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF), kilisema hakitakuwa miongoni mwa wanaoomboleza.

"Wakati wa utawala wake wa miaka 70 kama Malkia, hakuwahi kukiri uhalifu ambao Uingereza na familia yake ilitekeleza kote ulimwenguni na kwa kweli alikuwa mbeba bendera wa kujivunia wa ukatili," chama cha tatu kwa ukubwa nchini kilisema katika taarifa.

"Kwetu kifo chake ni ukumbusho wa kipindi cha kutisha sana katika nchi hii na historia ya Afrika."

Kwenye mitandao ya kijamii, wakosoaji wameenda mbali hata zaidi.

Queen Elizabeth dancing with Ghanaian president Kwame Nkrumah in 1961, four years after the country gained independence

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malkia Elizabeth akicheza na rais wa Ghana huru, Kwame Nkrumah, mwaka 1961 - picha hiyo iliwashtua baadhi ya watu katika utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Jumbe za Twitter zilizotumwa na profesa wa Marekani mzaliwa wa Nigeria Uju Anya, saa chache kabla ya kifo cha Malkia, zilizua mjadala mkali. Mmoja aliondolewa na Twitter kwa kukiuka sheria zake.

Katika ujumbe wa pili wa twitter , aliandika: "Ikiwa mtu yeyote anatarajia nionyeshe chochote isipokuwa dharau kwa mtawala wa kifalme ambaye alisimamia serikali iliyofadhili mauaji ya halaiki ambayo yaliua na kuhamisha nusu ya familia yangu na matokeo ambayo kati ya walio hai leo bado wanajaribu kushinda, unaweza kuendelea kutamani nyota."

Ujumbe wake wake unaonekana kurejelea vita vya Biafra mwishoni mwa miaka ya 1960, ambapo serikali ya Uingereza iliunga mkono na kuipatia silaha serikali ya Nigeria ambayo hatimaye iliwakandamiza waliotaka kujitenga na kuunda Jamhuri iliyojitangaza ya Biafra.

Mtumiaji mmoja wa Twitter, @ParrenEssential, alijibu kuwa hivi sivyo jinsi Wanigeria wanavyofanya, akiongeza: "Unawakilisha vibaya utamaduni wetu na nchi yetu."

Wengine wamesema kuwa kumshtumu mtu wakati wa kifo chake sio jambo la "kiafrika".

Machapisho ya kutaka kurejeshwa kwa almasi ya Star of Africa, ambayo ilichimbwa nchini Afrika Kusini mwaka wa 1905 na sasa inaangaziwa katika Vito vya Crown ya Uingereza, pia yalionekana siku ya kifo cha Malkia.

Wengi huitaja kama "iliyoibiwa". Ingawa ilinunuliwa na serikali ya Transvaal na kupewa Familia ya Kifalme ya Uingereza kama ishara ya uaminifu, maoni yaliyopo kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba wamiliki wake wa kweli ni watu wa Afrika Kusini.

Mtumiaji wa Twitter @Qban_Linx alisema almasi ya $400m - kipande kikubwa zaidi ambacho kimewekwa kwenye fimbo ya kifalme, iliyobebwa na wafalme wakati wa kutawazwa kwao - inaweza kugharamia elimu ya juu kwa wanafunzi 75,000 wa Afrika Kusini.

Queen Elizabeth at her coronation, carrying the sceptre topped with the Star of Africa in her right hand

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malkia Elizabeth katika kutawazwa kwake, akiwa amebeba fimbo, juu ya Nyota ya Afrika, katika mkono wake wa kulia

Kumekuwa na kilio kama hicho nchini India, ambapo hashtag "Kohinoor" ilianza kuvuma haraka baada ya kifo cha Malkia Elizabeth - kurejelea almasi kubwa katika taji la kifalme ambalo linaripotiwa litavaliwa na mwenzi wa mfalme mpya ,Camilla .

Wakosoaji wengine wanasema kwamba Malkia alipaswa kutumia uwezo na ushawishi wake kuhakikisha kwamba mabaki ya watu waliopigana dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza yanarudishwa.

Wakenya na Waafrika Kusini wanadai vichwa vya mashujaa kama Koitalel Samoei, ambaye aliongoza upinzani wa Nandi katika Kenya ya leo mwishoni mwa Karne ya 19, na Mfalme Hinstsa kaKhawula wa ufalme wa Xhosa wa Afrika Kusini, ambaye aliuawa mwaka wa 1835. Miili yao ilikatwakatwa na vichwa vyao vilipelekwa Uingereza kama nyara.

Mauaji ya kikatili ya Wakenya wakati wa uasi wa Mau Mau pia yamekumbukwa. Gitu Wa Kahengeri, ambaye alijiunga na uasi akiwa na umri wa miaka 17 miaka 81 iliyopita, alikariri kuzuiliwa katika kambi na vikosi vya Uingereza, kupigwa na kunyimwa chakula.

Gitu wa Kahengeri, photographed on 9 September

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vetarani wa uasi wa Mau Mau Gitu wa Kahengeri analaani vitendo vya Uingereza, lakini anasema bado anamuomboleza Malkia.

"Walichukua ardhi yangu, haki yangu ya kuzaliwa," aliambia shirika la habari la Reuters. "Lakini tunaomboleza Malkia kwa sababu yeye ni mtu, binadamu," alisema. "Tunasikitika kwa watu kufa."

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, aliyemtaja Malkia kama "kinara wa kujitolea k", amekashifiwa na baadhi ya Wakenya kwa kutangaza siku nne za maombolezo ya kitaifa.

Rais wa zamani wa Botswana, Ian Khama, alikuwa mwingine ambaye alitetea urithi wa Malkia, akimtaja kama usioweza kubadilishwa.

"Ukoloni si kitu tunachotaka kukumbuka, kilikuwa ni kipindi cha giza," alisema. "Malkia alirithi urithi huo, hakuwa mwanzilishi ... lakini alipotoka ilikuwa kama kurekebisha uharibifu uliosababishwa na ukoloni, alionyesha kuwa hatuko juu yako, tunataka kushiriki katika maendeleo yako. na kukusaidia kukua kama mataifa."

Bara linapaswa kumtazama kama mtu ambaye "alileta enzi mpya kutoka kwa ya zamani mbaya" alisema .

Wengi wamesema kwamba Malkia hakuwahi kuomba msamaha kwa uhalifu uliofanywa kwa jina la ufalme. Hata hivyo, alikiri "matatizo" na "matukio magumu", kama vile mauaji ya Amritsar, kaskazini mwa India, mwaka wa 1919. Kabla ya kutembelea eneo hilo mwaka 1997 ambapo jenerali wa Uingereza aliamuru askari kuwafyatulia risasi waandamanaji kwenye bustani iliyozungushiwa ukuta ili wasiweze kutoroka, alitoa hotuba akionyesha majuto.

"Historia haiwezi kuandikwa upya, hata kama tunaweza kutamani kiasi gani wakati mwingine. Ina nyakati zake za huzuni na furaha. Ni lazima tujifunze kutokana na huzuni na kujenga juu ya furaha."