Sayf al-Adl: Tunajua nini kuhusu 'kiongozi mtarajiwa ' wa al-Qaeda?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Na BBC Monitoring
- Nafasi, Essential Media Insight
Kifo cha kiongozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri katika shambulio la ndege zisizo na rubani lililotekelezwa na Marekani katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul, kwa kawaida kimeelekeza umakini ni nani sasa anaweza kuchukua usukani wa kundi hilo la kigaidi lililopigwa marufuk
Sayf al-Adl mzaliwa wa Misri ndiye anaonekana kuwa mtu anayeweza kumrithi kiongozi huyo. Yeye ndiye pekee aliyenusurika katika kundi la maveterani watano wa al-Qaeda waliowahi kutajwa kama manaibu wa al-Zawahiri, na sasa wanaaminika kuwa na uwezekano mkubwa wa kumrithi.
Lakini kunaweza kuwa na tatizo.
Al-Adl inaaminika kwa kiasi kikubwa kuishi chini ya vikwazo nchini Iran - nchi ambayo al-Qaeda inaiona kuwa adui mkubwa.
Mwanajihadi mkongwe
Akiwa mwanachama mwanzilishi wa kundi la al-Qaeda na luteni anayeaminika wa Osama Bin Laden, al-Adl ni mtu asiyeeleweka - na mkongwe anayeheshimika kwa harakati za kijihadi.
Hakika ni mtu anayesakwa na mamlaka za Marekani: akishirikishwa na FBI katika "Orodha ya magaidi wanaosakwa zaidi'', na tayari zawadi ya $10m imewekwa kwa Taarifa zozote juu ya maficho yake.
Anatuhumiwa kuhusika na milipuko ya mabomu ya wakati mmoja ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mnamo Agosti 1998, ambayo yaliua zaidi ya watu 220.
Lakini pia anaripotiwa kupinga mashambulizi ya 9/11 huko New York na Washington.
Katika waraka wa Februari 2021, watafiti kutoka Chuo cha Kijeshi cha Marekani, kinachojulikana kama West Point, walidai kuwa al-Adl na watu wengine waandamizi wa al-Qaeda waliogopa - kwa usahihi kabisa - kwamba shambulio kubwa katika ardhi ya Marekani lingesababisha jibu kali ambalo lingeshirikisha uvamizi wa Afghanistan, taifa ambalo limekuwa maficho salama ya wanachama wa al-Qaeda.u .

Chanzo cha picha, Getty Images
Al-Adl katika siku za nyuma aliwahi kuandika kwa kina juu ya mada mbali mbali zilizojumuisha "usalama na akili", vita na mapinduzi.
Miaka ya mapema
Taarifa ni chache zaidi kuhusu uwezekano wa maisha ya kiongozi mytarajiwa wa kundi la al-Qaeda. Kulingana na FBI, al-Adl alizaliwa tarehe 11 Aprili 1963 au miaka mitatu mapema.
Licha ya hadhi yake ndani ya al-Qaeda, kwa kiasi kikubwa amekuwa na hadhi ya chini na haonekani sana katika propaganda za kundi hilo.
Pia kuna mashaka juu ya utambulisho wake halisi; jina lake Sayf al-Adl (Upanga wa Haki kwa Kiarabu) huenda likawa jina analotumia vitani.
Watafiti katika West Point wanadai al-Adl mara nyingi hutambuliwa kimakosa kama Mohammed Ibrahim Makkawi, kanali wa zamani wa kikosi maalum cha Misri.
Anafahamika kupigana dhidi ya uvamizi wa Kisovieti wa Afghanistan katika miaka ya 1980 pamoja na Bin Laden wakati al-Qaeda ilipokuwa ikianzishwa.
Al-Adl baadaye alihamia Somalia, ambako alisaidia kutoa mafunzo kwa wanamgambo wanaopigana na uingiliaji kati wa Marekani katika Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Somalia. Kampeni hiyo ilipata umaarufu kwa tukio ambalo helikopta mbili za Kimarekani za MH-60 Black Hawk ziliangushwa na roketi huko Mogadishu hatua iliopelekea kuigizwa kwa filamu ya Holywood iliouza sana 2001 Black Hawk Down.
Inaaminika kuwa moja ya roketi hizo zilirushwa na raia wa Tunisia katika kikosi cha al-Adl.
Al-Adl alirejea Afghanistan katikati ya miaka ya 90 wakati ambapo Taliban walikuwa wakiimarisha udhibiti wao wa nchi. Aliondoka tena muda mfupi baada ya uvamizi wa Marekani mwaka 2001 na kuongoza kundi la wanaharakati wa al-Qaeda kwenda Iran kupitia mtandao wa nyumba salama. Inaaminika kuwa alikamatwa na mamlaka ya Irani mwaka wa 2003 na kuripotiwa kuachiliwa pamoja wanachama wengine wa kundi la al-Qaeda katika mabadilishano ya wa wafungwa miaka 12 baadaye.
Licha ya kufungwa kwa muda mrefu, al-Adl alisalia kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani ya al-Qaeda na alisaidia kuimarisha nafasi ya al-Zawahiri kama kiongozi baada ya Bin Laden kuuawa na kikosi maalum cha Marekani nchini Pakistan mwaka 2011.
Hata hivyo, kutawazwa kwake kunaweza kuwa gumu zaidi: Mtaalamu wa masuala ya ugaidi wa Marekani Colin P. Clarke anadai kwamba al-Adl bado yuko nchini Iran, akiishi chini ya "kifungo cha nyumbani".
Hiyo inaweza kuhatarisha kupanda hadhi .
Sio tu kwamba ni jambo lisilofikirika kwamba angeweza kuongoza kikamilifu kundi la wanajihadi duniani huku akiishi chini ya vikwazo katika jimbo la Shia, pia kuna suala la usalama.
Mwanachama mwingine mashuhuri wa al-Qaeda, Abu Muhammad al-Masri, aliuawa mjini Tehran mnamo 2020 katika operesheni inayodaiwa kuwa ya siri ya makomando wa Israel.
Kama si al-Adl, basi nani?
Orodha ya wagombea wengine ni fupi ikizingatiwa kwamba takwimu nyingi za juu za al-Qaeda zimekutana na hatima sawa na Zawahiri kwa miaka mingi.
Inawezekana kwamba al-Qaeda inaweza kumtazama mmoja wa wakuu wa washirika wake wa kikanda nchini Somalia (al-Shabab), Yemen (AQAP) au Mali (JNIM) kuchukua uongozi
Ingawa hili halingekuwa jambo la kawaida, inaweza isiwe mshangao mkubwa kwa shirika ambalo lilizidi kugatuliwa chini ya Zawahiri.
Mnamo mwaka wa 2013, kiongozi wa AQIM, Nasir al-Wuhayshi, aliripotiwa sana kuteuliwa kuwa naibu wa Zawahiri. Hii inaweza kupendekeza kuwa viongozi wa kanda wanagombania nafasi za uongozi mkuu - ingawa sio al-Wuhayshi mwenyewe, kwani aliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani mnamo 2015.
Yeyote atakayechaguliwa kumrithi Zawahiri atakumbana na ugumu huo huo wa kujoficha kwa hofu ya kulengwa na Marekani.












