Uchaguzi wa Kenya 2022: Kusafisha vyoo na kukata mboga kulivyowafurahisha wapiga kura

    • Author, Na Evelyne Musambi
    • Nafasi, BBC News, Nairobi

Baadhi ya wanasiasa wameachana na maisha ya starehe wakiwa katika kampeni na kugeukia kusafisha vyoo, kukata mboga na kupika chai katika juhudi za kuwashawishi wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Mmoja wa wanasiasa aliyewafurahisha zaidi Wakenya zaidi ni Polycarp Igathe, ambaye alivalia ovaroli, buti na glavu mpya kabla ya kuchukua ndoo ya maji na kuanza kusafisha vyo katika mji mkuu, Nairobi

Alitumia chini ya sekunde 20 kupiga deki choo kimoja huku wasafishaji wakiangalia kwa mshangao.

"Kwa muda mrefu imeonekana kama kazi chafu lakini hii ni kazi ya kuwajibika," alisema Bw Igathe.

Wasafishaji vyoo katika jiji la Nairobi wanatumia deki ya kuku kuu na ndoo kusafisha maeneo hayo ambayo wakati mwingi hutoa harufu mbaya

Bw Igathe - ambaye anagombea kiti cha ugavana wa Nairobi - pia amepigwa picha akiosha magari na kupeana vinywaji katika vilabu vya burudani nyakati za usiku.

Mbinu yake hiyo imekejeliwa na baadhi ya watu wakisema anafaa kuja kutunza watoto na kuwafanyia kazi za nyumbani

Bw Igathe alikuwa naibu gavana chibi ya Mike Sonko, lakini alijiuzulu chini ya mwaka mmoja baada ya kuchukua wadhifa huo akisema ameshindwa kupata ridhaa ya gavana ya kufanya na kazi.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema hatua hizi ni mbinu ya kujenga uhusiano mwema kwa umma na wapiga kura wanazijua sana na haziwezekani kuwashawishi kupiga kura.

Bw Igathe ni mpinzani mkuu wa Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja. Yeye pia hajaachwa nyuma amekuwa akitumia mbinu kama hizi kuwashawishi wapiga kura, amekuwa akishirikisha mitandaoni picha inayomuonesha akinunua samaki kando ya barabara, tomato na vitunguu sokoni badala ya kwenye maduka makubwa ya kuuza bidhaa kwa jumla.

Bw Sakaja amekuwa Seneta wa Nairobi tangu 2017 na hili ni jaribio lake la kwanza kuwania ugavana.

Mkazi wa Nairobi Anne Wambui alidakia kwamba wanasiasa hawajui masoko yanapatikana hadi kampeni zianze.

"Tunatatizika kuishi katika jiji hili lakini mtu anayenunua bidhaa katika maeneo ya bei ghali anakuja kujifanya anatuelewa anapotaka kura yetu," aliambia BBC.

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa amekuwa akijaribu kuwavutia wapiga kura kwa kupanda teksi za pikipiki, na kuacha gari lake la kifahari.

Pia alipanda toroli ambalo liliwekwa juu ya gari lake. Toroli ni alama ya chama chake na imekuwa ikitumiwa kuwavutia Wakenya vijana wachangamfu.

Bw Barasa pia amepigwa picha akinywa chai pamoja na wenyeji katika kibanda cha kuuza chakula kilichokandikwa kwa udongo.

Picha zingine zinamuonyesha akitumia jiko la kienyeji la mawe tatu kumpikia chai mjane wa miaka 67- lingawa anaonekana akiwa amevalia viatu vya bei ghali.

Hakuwashinda kila mtu na matukio haya ya unyumba, akipata maoni yasiyofaa kwenye mitandao ya kijamii.

Aliyekuwa Seneta Boni Khalwale ambaye anagombea tena ugavana wa Kakamega, magharibi mwa Kenya, alitaka kuthibitisha stakabadhi zake za barabarani kwa kuchagua kung'arisha viatu vyake kando ya barabara.

Alikaa akila mahindi ya kuchoma huku akisubiria asafishiwe.

Aliambatanisha picha hiyo na maneno "Kazi ni Kazi".

Haua ya Bw Khalwale bia iliwakasirisha Wakenya katika mitandao ya kijamii, kuashiria kwamba mbinu hizo za ushawishi hazifanyi kazi kila wakati.

Mbunge wa Embakasi Magharibi George Theuri alishirikisha mtandaoni picha inayomuonyesha akitembea bila viatu na kuambatanisha picha hiyo na maneno: "Napendezwa na mtaa wangu Loving every ".

Bw Theuri pia alivalia kaptura kwenye picha na kumfanya mmoja wa wafuasi wake kusema, "Inahitaji ujinga wa hali ya juu kuwaamini wanasiasa kama hao."

Miezi mitano iliyopita Seneta Isaac Mwaura alijizatiti zaidi kupata tikiti ya chama chake kugombea ubunge Nairobi kwa kuwasaidia wachuuzi kukata mboga.

Bw Mwaura alisema anajaribu kuelewa matatizo ya wafanyabiashara wadogo katika eneo bunge lake la Ruiru lililopo viungani mwa mji mkuu.

"Cha kusikitisha...hukujua mama na baba mboga [wachuuzi wa mboga] wamekuwepo hadi sa. Ilichukua mapambazuko ya mwaka wa uchaguzi kuamshwa na ukweli huu," mtu mmoja alichapisha kwenye mtandao wa kijamii.

Hatua hiyo hata hivyo haikusaidia mwanasiasa huyo kwani alingushwa katika kinyang'anyiro cha kuwania tikiti ya chama chake.

Pia unawezakusoma: