Uchaguzi Kenya 2022: Siwezi kuwa kibaraka wa mtu yeyote-Raila Odinga

Nchini Kenya, hali ya joto ya kisiasa imepanda kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti. Mwishoni mwa juma Rais Uhuru Kenyatta alimuidhinisha aliyekuwa mpinzani wake Raila Odinga kwa wadhifa huo

Wiki chache zilizopita chama cha Kenyatta cha Jubilee kiliunda muungano na Azimo la Umoja cha Odinga . Aliyeachwa kwenye baridi kali ni mgombea mwenza wa mara mbili wa Bw Kenyatta na Naibu Rais William Ruto.

Leo Bw Ruto aliidhinishwa rasmi na chama chake cha United Democratic Alliance kuwa mpeperushaji bendera wa urais.

Mpinzani wake mkuu Raila Odinga kwa sasa yuko London ameongea na mwanahabari wa BBC Sophie Ikenye na alianza kwa kumuuliza kama ana imani na mchakato wa uchaguzi.

Uchaguzi Kenya 2022:Unaweza pia kusoma